covid 19
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 8,355
- 20,792
Inawezekana vipi katika hali kama hii ya sasa, mkuu wa nchi upo kimya na unaendelea na majukumu yako kama kawaida kana kwamba hakuna kinachoendelea,
Ilhali nchi ipo kwenye tension kubwa, malalamiko ni mengi kila kona, makundi tofauti tofauti yanakupinga kwa namna unavyoongoza nchi, ila umekaa kimya kama haupo vile.
Wakatoliki ni dhehebu kubwa zaidi la Kikristo hapa nchini, kwa kauli zao na viongozi wao ni wazi kabisa wamekunawa.
Wananchi wa hali za chini, wanyonge, ndio kabisa hawataki hata kusikia jina lako. Sasa imefika kipindi hadi askari wetu wanasema hadharani na kushawishi mapinduzi — jambo ambalo si zuri hata kulifikiria tu.
Mkuu wa nchi, unashindwa vipi kutuliza hali ya hewa kwa kauli zako na hotuba zako? Hii ni maajabu kabisa. Wasaidizi wako ni watu wabaya sana na hawakutakii mema kabisa.
Nini kimekupata rais wetu? Mbona hukuanza hivi ulivyopata hayo madaraka? Jamani, nani anayekushawishi hadi tumefika huku?
Mbona mwanzo kila Mtanzania aliona fahari kuongozwa na mama, lakini mama umegeuka na umetugeuka watoto wako.
Inakuwaje unaruhusu na kudhamini askari wetu wa polisi watese na kuua watu ambao hata hawana hatia — yaani wamekupinga tu basi unaruhusu wauwiliwe? Hii mbona inatisha sana. Kwa nini mnatengeneza hali ya taharuki kwa lazima? Mnataka wananchi tupanic na kuogoba, halafu iweje tuwaogope nyinyi kama nani, miungu watu?
Mtawanyamazisha watu, lakini hamtanyamazisha haki karika taifa hata siku moja — na haitatokea.
Mungu yupo upande wetu daima. Tawala zenu zimefitinika mbele za Mungu na hamtambulikwi tena; mmefutwa kama alivyofutwa shetani na kundi lake huko mbinguni.
Kwa polisi mnaotumiwa na watawala na hao mafia kufanya mnayofanya, basi ngoja niwaambie — mwisho wenu hauwezi kuwa mzuri hata kidogo.
Mnamkumbuka John Okelo au mlishawahi kusoma historia yake? Basi hakuna mtu jasiri aliyewahi kuishi hapa Tanzania, huko Zanzibar, kama Okelo. Aliongoza mapinduzi kwa sauti ya kutisha na ukatili mkubwa uliowaogopesha Waarabu na kuwafanya wakimbie huku akiuwa mamia kwa maelfu. Mnajua mwisho wake ulikuwaje? Basi kasomeni historia vizuri mjue tabia za watu mnaowatumikia.
Mimi ni mwana CCM, nitasema ukweli — uwongo kwangu ni mwiko.