Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Awamu ya sita imefanya kikao cha wazi na wafanyabiashara pale Mnazi Mmoja na kamera za runinga zimeweka ushahidi wote hadharani. Hiki ni tofauti kidogo na kile kikao cha hayati JPM alichofanya na wadau wa sekta ya madini pale ikulu mwaka 2017.
Kimeweza kufanyika kwa kutegemea nguvu kubwa ya wafanyabiashara waliochoshwa na uonevu wa mfumo mzima wa kodi kuwa na kila harufu chafu ya rushwa.
Hakikufanyika kwa matakwa au maamuzi ya kiserikali bali ni matokeo ya mgomo wa wafanyabiashara walioona liwalo na liwe hawawezi kuendelea kujaza mifuko ya wafanyakazi wa TRA tena wengi wao wakiwa ni vijana wadogo wenye kunuka bado ile harufu ya magodoro ya vyuo vya fedha walivyotoka kumaliza kusoma.
Hili ni taifa la wezi japo kistaarabu hatupendi kutumia maneno hayo makali, lakini kilicholalamikiwa pale Mnazi Mmoja leo hii hakina tofauti na kile kilichokuwa kikifanyika kule TPA enzi za awamu ya nne. Ni mitandao fulani ya wizi haswa ya wasomi vijana wanaokua na kuingia maofisini wakichukulia kwamba ni haki na wao kuiba kwani waliowatangulia pia ni wezi tu!.
Kila awamu inakuwa na uchafu kama huu ulioundiwa kamati ya watu 14, ni hulka mbovu za kitaifa zinazoanzia juu kabisa. Huwa linaishia kupatikana suluhisho la muda mfupi tu na baada ya mwaka mmoja au miwili tatizo linarudi na ukubwa ule ule na wanaoumia ni mamilioni ya wateja wa hizo bidhaa za kutoka nje.
Wa kupewa pongezi za dhati ni wale wote walioanzisha mgomo, kwani hakuna mamlaka ambayo ingeweza kufunguka macho na kubaini uchafu unaoendelea hapo TRA iwapo uoga ungeachwa ukatamalaki.
Sisi ni watu wa hovyo sana, na kwa kweli napata shida kuwabebesha lawama wazee wetu kwa maana ya kina Nyerere na wote wa kizazi kilichokabidhiwa nchi na Muingereza mwaka sitini na moja. Hizi ni hulka za kishenzi tunazokutana nazo tukiwa watu wazima tayari.
Nasita kumuweka pembeni Rais fulani na mwingine nikaamua kumpigia makofi, wanakuwa ni wanasiasa wanaochafuliwa na hulka mbovu za walio chini yao kimamlaka.