Taifa lililojaa wezi wa kila awamu, ni wafanyabiashara waliochoshwa wenye ujasiri wa kusema hapana yenye kishindo

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
18,487
Reaction score
13,611
Awamu ya sita imefanya kikao cha wazi na wafanyabiashara pale Mnazi Mmoja na kamera za runinga zimeweka ushahidi wote hadharani. Hiki ni tofauti kidogo na kile kikao cha hayati JPM alichofanya na wadau wa sekta ya madini pale ikulu mwaka 2017.

Kimeweza kufanyika kwa kutegemea nguvu kubwa ya wafanyabiashara waliochoshwa na uonevu wa mfumo mzima wa kodi kuwa na kila harufu chafu ya rushwa.

Hakikufanyika kwa matakwa au maamuzi ya kiserikali bali ni matokeo ya mgomo wa wafanyabiashara walioona liwalo na liwe hawawezi kuendelea kujaza mifuko ya wafanyakazi wa TRA tena wengi wao wakiwa ni vijana wadogo wenye kunuka bado ile harufu ya magodoro ya vyuo vya fedha walivyotoka kumaliza kusoma.

Hili ni taifa la wezi japo kistaarabu hatupendi kutumia maneno hayo makali, lakini kilicholalamikiwa pale Mnazi Mmoja leo hii hakina tofauti na kile kilichokuwa kikifanyika kule TPA enzi za awamu ya nne. Ni mitandao fulani ya wizi haswa ya wasomi vijana wanaokua na kuingia maofisini wakichukulia kwamba ni haki na wao kuiba kwani waliowatangulia pia ni wezi tu!.

Kila awamu inakuwa na uchafu kama huu ulioundiwa kamati ya watu 14, ni hulka mbovu za kitaifa zinazoanzia juu kabisa. Huwa linaishia kupatikana suluhisho la muda mfupi tu na baada ya mwaka mmoja au miwili tatizo linarudi na ukubwa ule ule na wanaoumia ni mamilioni ya wateja wa hizo bidhaa za kutoka nje.

Wa kupewa pongezi za dhati ni wale wote walioanzisha mgomo, kwani hakuna mamlaka ambayo ingeweza kufunguka macho na kubaini uchafu unaoendelea hapo TRA iwapo uoga ungeachwa ukatamalaki.

Sisi ni watu wa hovyo sana, na kwa kweli napata shida kuwabebesha lawama wazee wetu kwa maana ya kina Nyerere na wote wa kizazi kilichokabidhiwa nchi na Muingereza mwaka sitini na moja. Hizi ni hulka za kishenzi tunazokutana nazo tukiwa watu wazima tayari.

Nasita kumuweka pembeni Rais fulani na mwingine nikaamua kumpigia makofi, wanakuwa ni wanasiasa wanaochafuliwa na hulka mbovu za walio chini yao kimamlaka.
 
Kwa ufupi ni kuwa maadili ya watumishi wengi yameshuka sana. Mfano, nilikuwa nafanya madiriko ya hati ya kiwanja pamoja na kuwa kila ofisi niliyokanyaga nimelipa kodi inayotakiwa, lakini nilipofika kwa kamishina wa mkoa, akaniambia hawezi kunipa hati mpaka aingie kwenye mfumo wa TRA ili ajue kama kodi hizi zimelipwa au la! Na anakwambia uende utarudi baada ya siku 7, kwa sasa mtandao haupo. Kokote nilikopita nilipewa namba ya udhibiti, hata ofisini kwake nilipewa namba ya udhibiti na nimefanya malipo, lakini anasema hana uhakika kama nimelipa.
 
Awamu ya sita imefanya kikao cha wazi na wafanyabiashara pale Mnazi Mmoja na kamera za runinga zimeweka ushahidi wote hadharani. Hiki ni tofauti kidogo na kile kikao cha hayati JPM alichofanya na wadau wa sekta ya madini pale ikulu mwaka 2017.

Kimeweza kufanyika kwa kutegemea nguvu kubwa ya wafanyabiashara waliochoshwa na uonevu wa mfumo mzima wa kodi kuwa na kila harufu chafu ya rushwa.

Hakikufanyika kwa matakwa au maamuzi ya kiserikali bali ni matokeo ya mgomo wa wafanyabiashara walioona liwalo na liwe hawawezi kuendelea kujaza mifuko ya wafanyakazi wa TRA tena wengi wao wakiwa ni vijana wadogo wenye kunuka bado ile harufu ya magodoro ya vyuo vya fedha walivyotoka kumaliza kusoma.

Hili ni taifa la wezi japo kistaarabu hatupendi kutumia maneno hayo makali, lakini kilicholalamikiwa pale Mnazi Mmoja leo hii hakina tofauti na kile kilichokuwa kikifanyika kule TPA enzi za awamu ya nne. Ni mitandao fulani ya wizi haswa ya wasomi vijana wanaokua na kuingia maofisini wakichukulia kwamba ni haki na wao kuiba kwani waliowatangulia pia ni wezi tu!.

Kila awamu inakuwa na uchafu kama huu ulioundiwa kamati ya watu 14, ni hulka mbovu za kitaifa zinazoanzia juu kabisa. Huwa linaishia kupatikana suluhisho la muda mfupi tu na baada ya mwaka mmoja au miwili tatizo linarudi na ukubwa ule ule na wanaoumia ni mamilioni ya wateja wa hizo bidhaa za kutoka nje.

Wa kupewa pongezi za dhati ni wale wote walioanzisha mgomo, kwani hakuna mamlaka ambayo ingeweza kufunguka macho na kubaini uchafu unaoendelea hapo TRA iwapo uoga ungeachwa ukatamalaki.

Sisi ni watu wa hovyo sana, na kwa kweli napata shida kuwabebesha lawama wazee wetu kwa maana ya kina Nyerere na wote wa kizazi kilichokabidhiwa nchi na Muingereza mwaka sitini na moja. Hizi ni hulka za kishenzi tunazokutana nazo tukiwa watu wazima tayari.

Nasita kumuweka pembeni Rais fulani na mwingine nikaamua kumpigia makofi, wanakuwa ni wanasiasa wanaochafuliwa na hulka mbovu za walio chini yao kimamlaka.
Magufuli anaingiaje hapo wew
 
Hapa nakuunga mkono, na matatizo haya tumekuwa tukiyapigia kelele muda mrefu. Unapokuwa na utawala unaopatikana kwa njia zisizo halali ni rahisi mienendo ya aina hii kushika kasi na kuonekana ya kawaida kwenye taasisi nyingine.

Imefikia mahali hadi taasisi hizi za kimamlaka zinatumika kukomoa watu wengine. Matokeo yake watumishi wa taasisi hizo hutumia ombwe hilo la kiuongozi na wao kujipatia mapato yasiyo halali. Hebu fikiria ripoti za CAG zinatoka kila mwaka, wizi ni uleule na hakuna hatua zozote zinachukuliwa, maana wanaosimamia sheria ndio sehemu ya huo uchafu. Fikiria kiongozi aliyeko madarakani kwa kupora uchaguzi, anapata wapi nguvu ya kumwajibisha afisa wa taasisi ya kimamlaka aliyemtumia kupata ushindi haramu?
 
Tena hawana aibu
Halafu wanalindana haswa
Ni nchi pekee mwizi anachekewa na kulindwa

Inasikitisha sana
Mfumo mbaya sana huu
Magufuli alikuwa mkali sana kwa sababu ya huu upumbavu tulioamua kuulea kuanzia katikati ya awamu ya pili mpaka ya ile ya tatu.

Mwendo wetu ulikuwa mzuri tu lakini ghafla tukaanza kukumbatia hulka za kinyama zisizo na huruma wala utu ndani yake, Magufuli katika mapambano ya kijasiri akaanza kuchukiwa na kundi la wapigaji wanaozoea kula kwa kutegemea machungu ya wengine, ni nchi ya kuiombea kwa Mungu kadri mtu unavyopata muda binafsi wa kufanya hivyo.
 
Mkuu tatizo nchi yetu imejaa wanafiki wengi sana na sheria hazifuatwi bali matamko ya mdomoni tu

Kupata mtu mmoja kuisimama nchi sio kazi rahisi lazima wakumalize
Na kuwahamisha hamisha au kuwafukuza haisaidii maana wamekuwa wameisha iba hela nyingi sana

Inatakiwa sheria ziongezwe makali na matamko ya kwenye mic [emoji441] yangeacha na kupitisha kwa maandiko

Sasa unakuta eti mwanamke huko sijui mkuu wa mkoa anasema marufuku kumuacha mwanamke
Imagine anaamka asubuhi na kuropoka tu
Hakuna sheria ya hivyo na wengi wa viongozi wana tabia za hivyo sheria ya siku moja halafu inapotea

Kuhusu Magu angekuwa na mawaziri.au makatibu 10 wanaofanya anavyotaka tungekuwa mbali ila nae kwa sababu ya kuogopa MFUMO hakuweza kuweka sheria ya kuwafunga majizi hayo kwani wanajuana

Hii nchi ngumu sana na tuiombee sana ili watoto wanaozaliwa labda wawe na maadili
 
Magufuli alikuwa mkali sana kwa sababu ya huu upumbavu tulioamua kuulea kuanzia katikati ya awamu ya pili mpaka ya ile ya tatu.

Mwendo wetu ulikuwa mzuri tu lakini ghafla tukaanza kukumbatia hulka za kinyama zisizo na huruma wala utu ndani yake, Magufuli katika mapambano ya kijasiri akaanza kuchukiwa na kundi la wapigaji wanaozoea kula kwa kutegemea machungu ya wengine, ni nchi ya kuiombea kwa Mungu kadri mtu unavyopata muda binafsi wa kufanya hivyo.
Inashangaza mtu alitoondolewa kwenye ukamishana, akapelekwa ubalozini baadae akaondolewa lakini tena bado anarudishwa palepale TRA kama kamishna mkuu na walewale waliokuwa wanamuondoa na ambao wanaujua ubovu wa huyo kamishna. mwingine ni waziri anadai kufunga na kufungua duka ni hiari ya mfanyabiashara na kusahau kuwa kufungwa kwa maduka yote Kariakoo ni tofauti na kufunga duka moja moja kwa utashi wa mwenye duka, nadhani majibu ya waziri huyu yanaonyesha dharau ni kama hajui madhara ya kufungwa kwa soko kuu la Kariakoo, ukiacha Bandari ya DSM, soko la Kariakoo ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato kwa seriakli yetu, nadhani tumeshau kuwa kule Tunduma kuna wafanyabiashara walifunga maduka yao na kuhamia upande wa Zambia na kukawa na kauli za ajabu kutoka kwa viongozi wetu lakini baadae ikaonekana serikali ndio imepoteza zaidi kuliko wafanyabiashara. Ningekuwa mimi ndio mkuu wa kaya huyo waziri alisema bungeni ni hiari kufunga au kufungua maduka angeondoka asubuhi mapema na pia waziri wa fedha nae angeondoka mapema sababu hana uwezo wa kutafuta ba kubuni vyanzo vya mapato yeye anazidi kuwabana tu wananchi wa kawaida, kuna matozo yasiyo na maana, double taxation, pia suala la VAT lingeangalia angalau VAT inazie kwa wale wenye biashaza za zaidi ya milioni mia tano, halafu hizi kodi za huduma ni za nini? kwa kipi kinafanywa na hizi halmashauri zetu hadi kustahili kodi ya huduma?
 
Mkuu huko sahihi lkn VAT iwe kwa kila mtu kama itashindikana kwa kila mtu basi yeyote aliyefikia ngazi ya kufanyabiashara na serikali awe na VAT, hii itasaidia sana kupunguza wale wanaokwepa kutoa rist.Kwa sasa hali ni mbaya kwa mtu mwenye VAT na ndiyo maana umpekelekea mwenye VAT kukataa kutoa rist akijua wasiohitaji risti ni wengi na sina sababu ya kukuuzia wewe unayetaka risti, yapo maduka ukimwambia nataka na risti anakwambia sina hiyo bidhaa unayotaka.
 
Magufuli alikuwa mkali sana kwa sababu ya huu upumbavu tulioamua kuulea kuanzia katikati ya awamu ya pili mpaka ya ile ya tatu.

Mwendo wetu ulikuwa mzuri tu lakini ghafla tukaanza kukumbatia hulka za kinyama zisizo na huruma wala utu ndani yake, Magufuli katika mapambano ya kijasiri akaanza kuchukiwa na kundi la wapigaji wanaozoea kula kwa kutegemea machungu ya wengine, ni nchi ya kuiombea kwa Mungu kadri mtu unavyopata muda binafsi wa kufanya hivyo.
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji915] [emoji915] [emoji915]
 
Inashangaza mtu alitoondolewa kwenye ukamishana, akapelekwa ubalozini baadae akaondolewa lakini tena bado anarudishwa palepale TRA kama kamishna mkuu na walewale waliokuwa wanamuondoa na ambao wanaujua ubovu wa huyo kamishna. mwingine ni waziri anadai kufunga na kufungua duka ni hiari ya mfanyabiashara na kusahau kuwa kufungwa kwa maduka yote Kariakoo ni tofauti na kufunga duka moja moja kwa utashi wa mwenye duka, nadhani majibu ya waziri huyu yanaonyesha dharau ni kama hajui madhara ya kufungwa kwa soko kuu la Kariakoo, ukiacha Bandari ya DSM, soko la Kariakoo ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato kwa seriakli yetu, nadhani tumeshau kuwa kule Tunduma kuna wafanyabiashara walifunga maduka yao na kuhamia upande wa Zambia na kukawa na kauli za ajabu kutoka kwa viongozi wetu lakini baadae ikaonekana serikali ndio imepoteza zaidi kuliko wafanyabiashara. Ningekuwa mimi ndio mkuu wa kaya huyo waziri alisema bungeni ni hiari kufunga au kufungua maduka angeondoka asubuhi mapema na pia waziri wa fedha nae angeondoka mapema sababu hana uwezo wa kutafuta ba kubuni vyanzo vya mapato yeye anazidi kuwabana tu wananchi wa kawaida, kuna matozo yasiyo na maana, double taxation, pia suala la VAT lingeangalia angalau VAT inazie kwa wale wenye biashaza za zaidi ya milioni mia tano, halafu hizi kodi za huduma ni za nini? kwa kipi kinafanywa na hizi halmashauri zetu hadi kustahili kodi ya huduma?
Kusoma theory za uchumi pale Mlimani au Havard ni tofauti na kuujua kwa vitendo namna unavyofanya kazi katika maisha ya kila siku ya hao uliopewa dhamana ya kuwaongoza.

Ulikuwa ni uamuzi wa maana kufanyika kile kikao na hao mawaziri wakawepo mahali pale ili waweze kuijua changamoto halisi ya watu wanaowalipa wao mishahara minono na kuwawezesha kutembelea hayo mavx ya bei mbaya.

Waziri Mkuu anabembeleza kwa kuwasihi wafanyabiashara akirudia ombi lake mara tatu, hii inatosha kabisa kuwa sababu ya Rais Samia kumuondoa Mwigulu na huyu Mama wapelekwe kwenye wizara nyingine zisizo na ugumu kama hii ya fedha.
 
Hapa nakuunga mkono, na matatizo haya tumekuwa tukiyapigia kelele muda mrefu. Unapokuwa na utawala unaopatikana kwa njia zisizo halali ni rahisi mienendo ya aina hii kushika kasi na kuonekana ya kawaida kwenye taasisi nyingine.

Imefikia mahali hadi taasisi hizi za kimamlaka zinatumika kukomoa watu wengine. Matokeo yake watumishi wa taasisi hizo hutumia ombwe hilo la kiuongozi na wao kujipatia mapato yasiyo halali. Hebu fikiria ripoti za CAG zinatoka kila mwaka, wizi ni uleule na hakuna hatua zozote zinachukuliwa, maana wanaosimamia sheria ndio sehemu ya huo uchafu. Fikiria kiongozi aliyeko madarakani kwa kupora uchaguzi, anapata wapi nguvu ya kumwajibisha afisa wa taasisi ya kimamlaka aliyemtumia kupata ushindi haramu?
Kichekesho kikawa ni ile kamati iliyoundwa pale pale jukwaani kuleta utatuzi wa tatizo. Wamo makada wa CCM watu wenye utii kwa mfumo uliopo.

Watatuzi wa kuja na kitu kipya chanya na wao ni sehemu ya washukiwa na wao ni sehemu ya hii michezo ya dhuluma na upigaji.
 
Back
Top Bottom