Taifa lililopiga kambi kwenye bonde la kashfa!

Taifa lililopiga kambi kwenye bonde la kashfa!

Tatizo watanzania wengi tunaanza kulizoea hili bonde na kuliona kama makao yetu ya kudumu. Ndiyo, na aliyetupeleka bondeni anajua fika kuwa nje ya bonde atapoteza nguvu kwa kuwa huko kuna hewa safi isiyoruhusu ustawi wa uvundo. Bunge limegeuzwa kuwa baraza la kutunga sheria kudhibiti na kuzima mawazo yoyote ya kuhama bondeni. Serikali inalinda huu uvundo kwa nguvu zake zote kwa kisingizio cha amani na utulivu bila kujua inatafuna watu wake pole pole kama kansa. Wengi baada ya kuathirika na uvundo wamepoteza kabisa uwezo wa kunusa, kusikia wala kuona na wanachapa usingizi bila wasiwasi. Wachache ambao hawajaathirika sana wamefungwa kamba miguuni na kuzibwa midomo wasije wakawakosesha wenzao usingizi.

Pamoja na Utawala bora umesahau mkuu.
 
Na vitendo vyako wewe ni ......?

Kuwahubiria nyinyi mnaopenda kuchonga bila kutenda. Utakuta hii mijitu inayochonga sana mingi kati yao haikai TZ iko nje inachonga. Njooni viwanja vya mapambano muone joto ya jiwe.
 
Kuwahubiria nyinyi mnaopenda kuchonga bila kutenda. Utakuta hii mijitu inayochonga sana mingi kati yao haikai TZ iko nje inachonga. Njooni viwanja vya mapambano muone joto ya jiwe.

Mkuu,

Kuna tatizo gani mtu kukaa nje na kupigana akiwa huko? Nilisoma katika vitabu vya dini kuwa kila mtu anatumia karama yake. Wengine ni kalama, mkono, mdomo, kichwa na miguu. Wengine wanaimarisha JF, wengine wanaandika kama akina MM, mimi nasambaza ujumbe na kuelimisha huku kijijini kwetu, wewe unakosoa, wangine wakisoma na kusikia wanaelimika na kuhamasika. Kama hujui kama wameelimika lianzishe alafu utaona.

Wewe tatizo lako ni lipi mkuu?
 
Tujaribu kujadili mada, na sio kutoka nje ya mada. Tujaribu kuelimishana positively na sio kwa kejeli na vijembe. Nashukuru kwa utashi wako wa kujaribu kumuelimisha Dar es Salaam na wengine wenye mawazo hasi kama yeye. This is supposed to be a forum!
 
Mzee MWanakijiji umenena Vyema sana,Na Heko kwa hilo ila toka jana kuna jambao ambalo linanisumbua sana kichwani mwangu.Ndiyo wapinzania wameweza kuvumbua mambo mengi kuhsiasan na mafisadi,Je sisi kama wananchi tumefaidika na nini?Matatizo yetu yametatuliwa?

Jambo hili linaniuma sana ,toka mwaka 2005 mpaka sasa hakuna mbunge yeyote aliyesubutu kueleza matatizo ya jimboni mwake na jinsi yatakavyo tatuliwa.Limekuwa bunge la kuibua kashfa na kujadili mambo yasiyoisha kwa pesa ya walipa kodi!

wabunge wamekuwa wakitafuta mbinu za kuchafuana wao kwa wao(hasa wabunge wa chama cha mapinduzi wakishirikiana na wabiunge wapinzani).wamekuwa wakifanya vikao vingi vya kumuangusga flani bila ya kujadili jinsi ya kutatua matatizo ya wananchi.Nchi imefika kubaya sababu inaendeshwa kwa majungu na fitina kila kukicha.

Mpaka sasa hakuna anayejua ni watanzania wangapi wanokosa huduma za Afya,Shule na maji safi.Nahdni wabunge wanatajkiwa kubadilika sasa.wajadili na mambo muhimu ya taifa hili.watatue shida za watanzania na siyo kila siku ni kashfa tu bungeni.

Nchi hii sas ainendeshwa kwa mkumbo na hakuna mstakabali wa taifa,na nakuapia ukimuuliza mkulu leo ni nini anaweza kujivunia kwa kipindi cha mwaka mmpja hawezi kusema!
 
Gembe, ndiyo maana nimesema sisi "kama taifa". Wabunge wetu included.. kwa sababu wangeamua kumaliza mambo ya kashfa hizi kubwa tukaziacha nyuma labda wangekuwa na kingine cha kuzungumza (natumaini haitakuwa kuchafuana).
 
Umeng'aka sana katika maelezo yako marefu ambayo nadhani kwa mzoefu wa kuwasilisha mada, angeya kusanya kwenye sentensi tano au kumi na angeeleweka vizuri.

Kwanza, uandikapo hebu jaribu kwenda moja kwa moja kwenye unalokusudia na sio kuzunguka mbuyu kama ufanyavyo.

Pili, baada ya kulalama sana kwenye nukuu zako za matakataka, jee ufumbuzi ni nini? Sijauona kwenye nukuu zako! au unataka ushauri? hujaeleza kusudio haswa la nukuu zote za takataka, au na nukuu zenyewe ni taka taka za kutupwa kwenye debe la taka? au ndio debe tupu haliishi kutika-tika?

Nimeshindwa kuelewa Dar es salaam analalamika nini? Anataka kulazimisha mtindo wake wa kutoa maoni kwa watu wengine? Ieleweke kwamba kufikisha ujumbe kunaweza kuwa kwa stahili tofauti, lakini lengo ni kwa wahusika kuupata huo ujumbe. Ndio maana hii mada ipo hapa kwa ajili ya watu kutoa michango yao, suluhisho linaweza kutoka kwa wasomaji wengine pia kama wewe, kama pia hujafanikiwa kuona suluhisho ni kuwa na watu wenye upeo wa kuongoza kwa ajili ya maendeleo sio kujivunia vitu ambavyo ni obvious.
 
Dar es salaam,
Mkuu umenikumbusha tukio moja,..Kuna binti mmoja alikuwa na Mimba na ktk taratibu za mimba hiyo ilibidi kumwona daktari kila mara..Sasa siku moja daktari alipomwambia, mimba sio ugonjwa nenda kazini kama kawaida, jaribu kufanya mazoezi na kadhalika maadam asiwe mvivu wa kula na kulala tu.
Bibie hakupenda mawazo ya daktari - jibu lake lilikuwa Ungeibeba wewe hii mimba usingeyasema yote haya!
Kwa hiyo mkuu nakuelewa sana...
 
Gembe,

Hapo umenena pia mkuu. Tuko upande mmoja. Ila kuna kitu kidogo unakichukulia kama hakina maslahi kwa nchi. Kuibua kashfa za ufisadi ni mojawapo ya kazi kuu za bunge letu. Bunge liko pale kuisimamia serikali. Na kama wabunge wameweza kuona kwamba kuna baadhi ya viongozi wa serikali wanafuja kodi za wananchi, basi ni jukumu lao kuwaripoti bungeni na hatua za kinidhamu zikachukuliwa. Hili limesaidia kwa kiasi flani japokuwa si sana. Bilioni 69 zilizorudishwa (kama kweli zimerudishwa) kupitia EPA ni changamoto tosha kwamba tukiamua tunaweza. Fedha hizi zitapelekwa vijijini kusaidia sekta ya kilimo kama Rais wetu alivyoahidi. Hapa utaona kwamba bunge limefanya kazi yake na jamii itafaidika.

Nimesema nakubaliana na wewe kwa kuwa hata mimi ningependa kuona bunge likifanya zaidi ya hayo. Ningependa kuona wabunge wanawakilisha wananchi wao waliowatuma bungeni kwa niaba yao. Wabunge wawakilishe kero za wananchi wao. Wabunge waache kuhoji budget za wizara mbalimbali na mwishoni wanazipitisha budget hizo (i have never seen such ridiculous acts). Yaani mbunge anaongea for half an hour akiwa anachambua mapungufu ya budget ya wizara fulani, then mwishowe anasema "Naunga mkono budget kwa asilimia 100". Thats very stupid. Ningependa kuona bunge linafanya zaidi ya hapo. Wabunge wapinge budget zenye mapungufu. Wabunge wakatae hoja na sheria ambazo hazina maslahi kwa umma. Wabunge ndio wenye nguvu ya kututoa bondeni. Na wewe mwananchi ukitumia nguvu yako ya kura kwa busara, basi hili tunaweza kulifanikisha.
 
Wakuu zangu... Jamani twendeni mbele tukitazama nyuma..
Hivi kweli mnafikiria Ufisadi ni jambo dogo sana!
Hivi kweli mnafikiria Mbunge anaweza au no bora asimame na kulilia maendeleo ya jimbo lake wakati anafahamu kabisa fungu la maendeleo atakayo yadai litaliwa kabla halijafika jimboni kwake..
Hii ni sawa na kubeba ndoo ya maji inayovuja ukielewa wazi hutafika na tone la maji nyumbani bado watu wanataka bora ubebe hivyo hivyo uonekane busy..responsibility bila accountability ndio way to go - kweli tutafika wakubwa!
Jamani Ufisadi nchini umefikia mahala hakuna kitu kinachowezekana isipokuwa kupitia wizi na dhulma..na nimeshasema hatuwezi kuendelea hata siuku moja kama tutashindwa kuziba mirija (tobo) ya Ufisadi.
Tanzania ni sawa na nchi iliyoko vitani isipokuwa vita yetu ni ya kiuchumi mwenye silaha ya kuua ni yule aliyeko madarakani...Jitihada zote za kuvunja vita hii haiwezi kuonekana kwa sababu imekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku kama Somalia..life goes on!
Inasikitisha sana..
 
Mzee Mwanakijiji kama ulivyoona jinsi watu walivyo tafsiri article yako ndio hivyo watanzania tulivyo . Ubinafsi mwingi. We have a lote to say but means little. Do not let them discourage you .You are a great treasure to this country. If we would have 50 people like you we would not be stuck in the mad.
 
Gembe, ndiyo maana nimesema sisi "kama taifa". Wabunge wetu included.. kwa sababu wangeamua kumaliza mambo ya kashfa hizi kubwa tukaziacha nyuma labda wangekuwa na kingine cha kuzungumza (natumaini haitakuwa kuchafuana).

Kwa mtazamo wangu msululu wa lawama unakwenda kama ifuatavyo
1.Serikali ndio wakulaumiwa kwa kuendeleza mtindo "kuzifuga" kashfa, suala kama la Richmond(mfano) wabunge wetu walishafanya kazi yao kwenye tume ya Mwakyembe na tunasubili matekelezo ya maagizo yao ila mpaka leo waziri mkuu anakuja bungeni na kutwambia bado linashughulikiwa, linashughulikiwa mpaka lini? Je hii ndio kasi mpya tulioahidiwa? Wabunge kama wawakilishi wa wananchi wana jukumu la kulifuatilia suala hili mpaka mwisho wake,au waliache tu hewani wakati maagizo yao hayajafanyiwa kazi?

2.Wabunge wameonyesha kutokua makini kwenye majukumu yao ya kuiwajibisha serikali na wachache wamekili hili,wanauma na kupuliza! Nasema wanauma na kupuliza kwakua wanashindwa kuibana serikali moja kwa moja yaani kua consistent kwasababu ya maslahi ya kichama, serikali inapoona inazidiwa, Makamba(The dentist) anawaita wabunge wa CCM wanakaa na kutoka na msimamo ambao utaipa ahueni serikali kwa maana nyingine ni kuling'oa meno bunge! nahapo ndipo marktime zinapoanza (kama ulivosema MMMK)

3.Watanzania ambao tunajua kabisa kua na wabunge wengi wa chama kimoja ni kansa mbaya kwa Bunge na ustawi wetu kwa ujumla lakini tunaendelea kukichagua chama hichohicho kinachotudidimiza kwenye lindi la ufisadi,kutokuwajibika,kulindana na mengine mengi mabaya. Tunauza shahada zetu za kura,tunapokea takrima za pilau t-shirt na pesa uchwara kumpa mtu dhamana ya mustakabali wetu kwa miaka 5 ijayo(hii ni aibu) huu ni umaskini wa kifedha ama ni umaskini wa fikra?

HII NI AIBU KUBWA! HAKUNA ANAETEKELEZA WAJIBU WAKE

MWANANCHI WAJIBISHA MBUNGE WAJIBISHA SERIKALI WAJIBIKA KWA MWANANCHI.
 
Last edited:
Back
Top Bottom