Taifa linahangaika na wasiojulikana waliomshambulia Tundu Lissu! Je, ni hawa?! Mhe. Mwigulu, IGP, anzieni hapa!

Taifa linahangaika na wasiojulikana waliomshambulia Tundu Lissu! Je, ni hawa?! Mhe. Mwigulu, IGP, anzieni hapa!

Moja kati ya vitu ninavyo vipenda sana kwa Mungu ni hiki; Wote tutakufa. Wauaji, wapanga mipango ya kuua watu, wanao ua kwa bahati mbaya, matajiri, masikini, wasomi, mbumbumbu, wenye vyeo na wasio na vyeo, wote tu tutakufa; Hilo ninalipenda na lina usawa ndani yake. Ulindwe na mbwa, bunduki, waganga, majini wote tu tutakufa siku moja. Ningependa binadamu wote tulikumbuke hilo and something very good is, hatujui siku wala saa tutakayo KUFA. Bora kumcha Mungu
Ndio maana nilwahi sema: "the world is fair once you are dead or when someone else is dead."
 
Mkuu pasco tumsifu yesu Kristu

Naomba jibu

Ni wakati gani Ngurumo anakuwa mwanahabari na wakati gani anakuwa mwanasiasa tena kamanda wa chadema kikwelikwelii?

Utamtofautishaje Ngurumo wa siasa na mwanahabari?

Nijibu nirudi kwa mapana
utamtofautishaje mkulu na mwenyekiti wa chama?
Wakati gani anakua Rais na wakati gani anakua mwenyekiti wa chama??
 
Hapa kuna jambo la kujifunza!

Tatizo la wengi wetu hatupendi kujifunza, tunatumia kile tunachokiamini, kilicho ndani yetu kuwa ndio maarifa.

Tutumie milango ya fahamu kupata maarifa mapya kisha tujifunze kitu.

Tutambue, tukiona hali haibadiliki basi hapo hakuna tunalojifunza
 
Kujidungua mwenyewe
Ngulumo ameamua kujilipua ili polisi wahudhurie kwenye tukio na ndipo maswali yasiyo kuwa na majibu yapate kujibiwa.
Unadhani Gulumo hana uelewa na sheria ya mitandao! Na jinsi ilivyo boreshwa ili kuiwezesha serikali kukita kucha zake kwenye kolomeo la yeyote anaebweka kinyume cha matakwa ya waheshimiwa? Vipi kuhusu wimbo wetu mashuhuri wa uchochezi! Nao pia hafahamu na kuwa aweza kuimbiwa wakati wowote?
GULUMO kajilipua makusudi ili wampeleke kwa Pilato huko ukweli wote ukawekwe hadharani na mwinda si ajabu kugeuka kuwa mwindwa!
Si kweli kuwa wasio julikana hawajulikani na si kweli kuwa alietoa zile cctv camera hajulikani anajulikana sana, wala haingii akilini kuwa vyombo vyetu vyote vimeikosa pointi (a) ya mkasa wa Lisu.
Kilichopo ndio hicho Gulumo anakitaka kaingiza kijiti kwenye shimo la siafu ili akichomoa atoke nao.
Kwangu mimi Gulumo kaponda jiwe kichakani, aliemo apime maamuzi kwa busara je alieponda kamaanisha nitoke tupambane au kajipondea tu ili kujifurahisha, nasubili kuona.

Umeona mbali sana....angalia kwa makini maeneo yaliyoguswa.
Lissu paaaaap
Kinondoni paaaaap

Thrn akaendelea na story ya uchaguzi kata moja huko Mwz.
Sasa anagoja aguswe, na ataguswa kwenye lipi

1) kikao cha ukumbi wa BOT Mwz
2) mazungumzo juu ya Lissu
3) kuhusu kinondoni
4) kuhusu mkuu wa nchi kutoa amri
5) kuhusu kupanga utekaji _jinai

Nani anajua Ngurumo anajua hayo mambo kiasi gani.
Kama wqna busara watamwacha au kumpoteza na kama hawana busara watajaribu kumkamata. Labda kumhoji kusikoisha na kesi isiyopelekwa mahakamani.
 
Pascal Mayalla Ngurumo anajiaminije mpaka anatoa taarifa ngumu kama hii? .Hajui kuwa wengi aliowataja ni wateule wa Rais ?

Inamaana Rais anabariki upuuzi huu?Ngurumo jitokeze ueleze vyema tofauti na hapo utaitwa mchochezi
Mbona watazania wagumu wa kuelewa!!! Unaweka maswali sehemu ya kuweka full stop. Unataka ajitokezeje, ameshaandika unataka apige talumbeta mtaani au aende mwenyewe polis?
 
Inawezekana walikuwa recorded? That will make more sense zaidi ya hear say!
Kwakuandika exact muda kikao kilipoanza kunaonyesha kuna details za recorded sound au video. Ngurumo ni mwandishi msomi anajua kutoa hints:

1) muda kikao kimeanza ...kwamba ana details ya kikao
2) random mazungumzo ya washiriki...lissu na kinondoni (inaweza kuwa ni mtego wa panya anaswe paka hapo)
 
Watanzania tatizo wengi hatujui kuwa tunataka nini?

CCM wao wanachotaka ni Madaraka basi.
CCM wakiona kuwa ufisadi unawasaidia kushinda wanaufanya.
Wakiona kuwa kuficha ufisadi usijulikane ili washinde basi watafanya hivyo.
Wakiona kuwa kuvunja haki za binadamu kutawasaidia kushinda basi watafanya hivyo.
CCM hawajali chochote iwe ni sheria za nchi, amri za Mungu, sharia za dini, mila za kitanzania , uhai wa mtu ; kamwe hawatajali alimradi watakachokifanya kitawapa ushindi tu kwenye uchaguzi.

Sasa kwa wananchi wengi na wapinzani hawajui wanachotaka ,wao wanaenda tu kama mazuzu.
Ndio maana unakuta leo wanakuambia tunataariifa za kupigwa ,kitekwa na kukatwa mapanga kwa viongozi wetu ,na wanatoa mpaka ushahidi na walipo watesi wao lakini cha ajabu hawatoi taarifa kituo cha polisi wala hawajilindi matokeo yake wanauawa kama kuku na watu wasiojulikana.

Chadema weshaona kuwa watu wao kuuawa au kupigwa ni sehemu ya kupata umaarufu na kunadi chama kwa huruma za wananchi. Ndio maana wanapata taarifa kabla halafu wanakimbilia online Tv kushitaki badala ya kwenda polisi au kuchukua maamuzi magumu ya kujilinda au kuweka mitego ya kuwakamata watesaji na wauaji.
Chama chenye wanachama wengi vijana kwenye miji yote haiwezekani kishindwe kuwanasa watekaji. Vinginevyo wanajiteka wenyewe kwa sababu wameshaona kuwa ni mbinu ya kupata umaarufu.
Wajifunze kwa CCM ambao wao wanatoa taarifa polisi kwa kila kitu wanachokishuku na wanakua bega kwa bega na polisi kuhakikisha taarifa yao imefanyiwa kazi.
Wapinzani wao wanabaki kulalamika wakati hawatoi taarifa.
Mfano tu wamebiwa mawakala wawe na vitambulisho badala ya kutafuta vitambulosho au kwenda mahakamani kupinga au kuzuia kanuni hiyo kutumika wao wanataka kutunishiana misuli na mkurugenzi kwa kusem kuwa wataingia kwa nguvu wakati hawana nguvu.
Hakika watatolewa kwa nguvu na kura zitapigwa na CCM watatangazwa mshindi na wapinzani uchwara watabaki kulalamika mazuzu.

CCM nao na serikali yake wazuie uvunjifu wa amani kwa kutenda haki na hasa uhalifu dhidi ya binadamu. Ni laana kubwa kuona damu za watu zinamwagwa tena baada ya watu kuteswa sana bila kuona nguvu za kulaani na kuchukua hatua zikitumika.


Nchi hii ni ya mfumo wa vyama vingi na ni wajibu wa chama kinachoshinda uchaguzi kusimamia uhai na haki na sheria za nchi zisivunjwe kwa sababu yoyote ile hata kama inapelekea wao kushindwa.
Huwezi kusema unalinda Twiga ,tembo na nyoka wa porini halafu unashindwa kulinda ndugu zako na wanasiasa wenzako ambao kwa miaka mingi mmekua mkiishi kirafiki halafu ujiite wewe ni binadamu mwenye akili timamu.
Tulinde watu zaidi kuliko vitu.

Viongozi wa dini nao wasikae kimya.
Kuna dini nyingine wanajifanya kuwa urafiki wa viongozi wao na wanasiasa unawafanya wawe salama.
Wanajidanganya. Historia ya nchi kujawa na watawala waroho wa madaraka kwa kuwagawa watu hua haiachagi salama dini .
Leo hakuna ubaguzi wa kidini kwa sababu nguvu za wabaguzi wezielekeza kwa wanasiasa lakini wakiwamaliza wanasiasa watageukia dini. Watasema dini fulani hawafai kutawala nchi hii. Na watawabughudhi wale wenye ndoto za kutawala siku moja.


Watanzania tupendane wakati huu wa mwezi wa toba ya Kwaresma.
Tukumbuke kuwa Yesu aliuawa na serikali ya Kirumi baada ya kusingiziwa na wale walioamini katika itikadi za Kiyahudi .
Huu ulikua ni mfano mbaya kabisa kwa watawala wa kidunia kuua watu wasio na hatia.
Tujifunze maneno ya Yesu Masihi kwa kusema na kuomba Ufalme wa Mungu uje nchini mwetu.Watawala watawale kwa kumheshimu Mungu aliyetuumba wote na kutupa uhai kwa neema yake na mapenzi yake. Hakika tutaishi salama.
Ni rahisi kuua lakini sio rahisi kufuta dhambi na kuipa amani dhamira ya mtu aliyeua mtu asiye na hatia kwake.

Hofu ya Mungu na kujishusha ndiko kunakotufanya tuwaheshimu wengine kuwa nao wameumbwa ili waishi hapa duniani kama tulivyo sisi.
Utawala wa mwanadamu kwenye biblia umepewa namba 666 , ni utawala wa kujikweza na kujiinua juu kama mungu.Ni utawala unaofanana sana na utawala wa wenye kujitanua. Hautofautiani sana na utawala wa shetani kama utamweka Mungu pembeni.
Ni utawala usiopenda mambo ya dini dini mana unajiona kuwa uko juu ya sheriz zote.
Kwa hiyo watanzania tuwausie viongozi wetu wamwogope Mungu mmoja tu. Na wajitambue kuwa wao ni wanadam tu.
Turejee wote kwenye imani zetu zilizotufanya tutendeane mema.
Kila mtu afanye lile ambalo angependa yeye naye afanyiwe .


Kama Wanasiasa wa vyama vya CCM na Chadema watakubaliana na hali ya kuvuruga umoja wetu basi tutaliangamiza taifa letu. Hasa pale ambapo viongozi wa dini, waandishi wa habari na wananchi wasio na vyama wanakosa nafasi kubwa ya kukemea.
Umehubiri vizuri Mr. 1000 Digits Lakini kuwataka CDM waripoti police hasa kwa maswala yenye maelekezo kutoka juu ni kijisumbua!!! Swala la Mawazo, Lissu, marehemu wa Arusha, wa Tarime, la Saanane, la wale wa Mbeya, wale wa Arumeru nk. Maswala yao yapo police Je kimeendelea nini???!!!

Kilichotakiwa ni kuwa na viongozi wanaothamini uwepo wa wananchi, ktk wao kuingia madarakani. Si hawa wanaothamini uwepo wa vyombo vya dola ktk uwepo wao madarakani.

Mwisho haya yote yanaletelezwa na katiba mbovu iliyorundika madaraka makubwa kwa binaadamu badala ya taasisi tulizojiwekea. Na katiba hiyo mbovu, imekuwa chaka la watawala kukandamiza wananchi. Na ndio maana hawako tayari kuijadili na wala kuibadili na kuja na katiba inayowapa wananchi nguvu dhidi ya serikali
 
Moja kati ya vitu ninavyo vipenda sana kwa Mungu ni hiki; Wote tutakufa. Wauaji, wapanga mipango ya kuua watu, wanao ua kwa bahati mbaya, matajiri, masikini, wasomi, mbumbumbu, wenye vyeo na wasio na vyeo, wote tu tutakufa; Hilo ninalipenda na lina usawa ndani yake. Ulindwe na mbwa, bunduki, waganga, majini wote tu tutakufa siku moja. Ningependa binadamu wote tulikumbuke hilo and something very good is, hatujui siku wala saa tutakayo KUFA. Bora kumcha Mungu
Ndo maana huwa najiuliza, kama kifo kisingekuwepo, nadhani wengi wetu tusingeamini Mungu yupo.

“Fear of death and unknowns”, is what make most of us believe in God!

Otherwise we would’ve been braver like them suicide bombers!
 
Kwakuandika exact muda kikao kilipoanza kunaonyesha kuna details za recorded sound au video. Ngurumo ni mwandishi msomi anajua kutoa hints:

1) muda kikao kimeanza ...kwamba ana details ya kikao
2) random mazungumzo ya washiriki...lissu na kinondoni (inaweza kuwa ni mtego wa panya anaswe paka hapo)
Ni kweli. Mimi mwenyewe naipa taarifa hii a benefit of doubt, kwasababu nina imani na Ansbert Ngurumo.
 
Pascal sidhani hicho kama kilikuwa kikao cha ulinzi na usalama japo kilihudhuliwa na wajumbe wa ulinzi na usalama.
Hicho ni kikao cha CCM na wadau wake wanaofanikisha uwepo wa CCM, Uwepo wa CCM ni faida kubwa kwa baadhi ya watu hivyo lazima waulinde uwepo huo kwa namna yeyote hili..
Halafu mtu anaenda mbele ya altare kupakwa majivu dah kweli tumeamua kumchora mungu
 
Kuna kitu kikubwa sana sana kila mtu anakifahamu, Pascal Mayalla acha kupoteza muda, unaujua ukweli, wanaujua ukweli. Huenda unataka nikuelewe the way ninavyofikiria, kama hivyo ndivyo basi uko sahihi....but pamoja na kuwa sahihi ukweli ni kwamba hawataweza kujichunguza wenyewe
Hawawezi kujichunguza, haya mambo yanaratibia na wao wenyewe. Haya yawe reported to the UN, CDM should send a special mission to the world kuieleza kinachoendelea hapa. And this will work!
 
Hebu niambieni ni huyo huyo aliyeamrisha kamanda Mawazo auawe, ndiye aliyeamrisha kurushwe bomu kwenye mkutano wa chadema, ndiye aliyemtishia Zitto Kabwe kifo na mhariri yule aliyekuwa mwananchi Dennsi Msacky na niye aliyempoteza Ben Saanane? Miaka yote hii Hugo huyo tu.

Ndiye aliyemng'oa meno Dr Ulimboka?
Succession! A policy in the party, kill opponents! Now it is a successon
 
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali tuu kuhusu watu watu, kwa kulisaidia jeshi letu la polisi na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kuitumia mitandao ya kijamii positively as source of a security tip ya vital information kuhusu uchunguzi mbalimbali. Usisubiri hadi mtu akaripoti polisi kuhusu uhalifu, wenzetu wakiona chochote kwenye social forum, kama security implications, wanakichukulia very seriously.

Tangu kushambuliwa kwa Tundu Lissu, na watu wasiojulikana, jana kuna bandiko humu, limewataja kwa majina, waliopanga mpango huo, huku wakipanga mipango mingine miovu.

Nawaomba waichukulie taarifa hii hapa if very serious
Ansbert Ngurumo: Taifa linaelekea pabaya sana
Taarifa yenyewe ni hii



Japo mimi binafsi ni kama Tomaso, huwa siziaamini baadhi ya taarifa za wanasiasa kirahisi rahisi, ikiwemo taarifa hii yote hivi hivi ilivyo. Kuna maeneo nakubaliana na Ngurumo, kwa vile licha ya kuwa ni mwanasiasa, pia ni mwana habari, hivyo taarifa hii kihabari ni taarifa muhimu sana kuhusiana na shambulio la Lissu!.

"Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa *walifanya makosa.*", sorry jamani siiamini kabisa kuwa hiki kilijadiliwa, kwa sababu siamini hawa watu wanaweza kuwa vichaa hivi!.

Sababu ya kutoiamini kauli hii ni kwa sababu inabeba criminal liability za aina mbili
Accessories After The Fact: Lissu ameshambuliwa na watu wasiojulikana, Jeshi letu la polisi limeshindwa kufanya chochote kwa sababu limekosa pa kuanzia baada ya kukosa shuhuda yoyote wa kumuhoji, na kuna camera za CCTV zilirekodi, zimetoweka, hivyo hakuna kabisa pa kuanzia uchunguzi!.

Kumbe kuna watu wamejifungia katika ukumbi wa BOT Mwanza akiwemo RC na RPC ambao ndio walihusika na shambulio lile!.They are all, accessories after the fact, wanapaswa kukamatwa na kuhojiwa kuhusu sambulio la Lissu!.

Kwa vile RPC nae ni mhusika, hivyo hakuna mahali pa kuanzia, ila naamini kwa vile Mwigulu ni member wetu humu, atawatuma vijana wake wakawahoji wahusika waliotajwa, tena nawaomba wasimsumbue kabisa Ngurumo kumtaja source wake, kama ameitoa taarifa hii kwa kofia yake ya uandishi wa habari, kwa sababu sisi waandishi tuna kinga ya kihabari ya "the confidentiality of the source".

Kama ameitoa kama Makamo Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa, alipaswa kesho yake kuondoka Mwanza kwa ndege ya kwanza na kufikia mezani kwa Mwigulu, kisha kwenda mezani kwa Kipilimba kuripoti, halafu ndipo ailete humu!.

Criminal liability ya aina ya pili, ni accessories before the fact, ambapo watu wakubwa, wazito wa mkoa wamekutana kupanga kufanya jinai!.

Any good citizen akisikia ni wajibu wake kuripoti, kwa vile RC na RPC ni wahusika, waliosikia wakaripoti kwa Ngurumo, kwa vile Ngurumo sio Mlinzi wa Amani, tariffs hiyo ni very sensitive ilibidi Ngurumo amuongoze mtoa taarifa wake kwa mlinzi wa amani, Waziri aelezwe, IGP aelezwe, na Amiri Jeshi aelezwe, ili wahalifu hawa, watiwe mbaroni haraka kabla hawajatekeleza jinai hii!.

NB, karibu wote waliotajwa ni wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama, ambao wana mamlaka ya kumkaribisha mtu yoyote kwenye kikao chao hata kama sio mjumbe. Hivyo hii isijekuwa ni leakage ya taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, imeleak kwa Ngurumo, naye kaileta JF, taarifa za kamati ya ulinzi na usalama ni siri!. Hivyo this leaves much to be desired, kumbe hizi ndizo kazi za kamati zetu za ulinzi na usalama za mikoa!. Nimemkumbuka Kamanda Mawazo!' RIP Kamanda Alphonce Mawazo, damu yako haitapotea bure, sasa imeanza kuchemka na kuibua madudu yanayofanyikaga!.

Ila pia sisi raia wema wa nchi hii, tufanye responsible blogging kwa self censorship ya sensitive info, tuwe makini na waangalifu sana na hizi taarifa za wanasiasa, nyingine ni political capitalization tuu!, tusije tukalishwa matango pori na kuingizwa ...cha kike!.

Kuhusu madudu ya Kamati za Ulinzi na Usalama, nimewahi kuyazungumza hapa TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali Wachunguzwe, Wafumuliwe!

Ila pia niliwahi kutoa tahadhari, sio kila unachosikia lazima ukiseme Swali la Morality: Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?

Paskali
Wewe mwenyewe anzia hapo Pascal,sio kila unachokijua lazima ukisema.
 
Back
Top Bottom