Taifa lisilo kuwa na Umeme wa uhakika ni Taifa liloamua kuwa masikini

Taifa lisilo kuwa na Umeme wa uhakika ni Taifa liloamua kuwa masikini

Hata hilo bwawa halitasaidia maana linategemea mvua


Siamini kama bwawa la "stigler gorge" litamaliza tatizo la mgao wa umeme nchini
Vipi na mradi wa gesi wa Kinyerezi?
 
Habari wanajamvi!
Kwa muda sasa tatizo la umeme linazidi kumea na hakuna matumaini ya huu mgao kuisha, Najaribu kujiuliza kama Mtanzania hivi serikali imeshindwa kabisa kumaliza tatizo la mgao wa umeme?

Sina haja ya kuelezea Faida za nishati hii muhumu kwa maendeleo ya nchi hilo kila mtu anafahamu sasa kama tutashindwa kudhibiti uzalishaji wa umeme ambao ndio nishati muhimu katika kukuza uchumi vipi tutaweza kukua Kiuchumi wakati umeme wenyewe tu umetushinda?

Itoshe kusema tu taifa ambalo limeshindwa kuwa na umeme wa uhakika ni taifa ambalo limeamua kuung`ang`ania umaskinini na kuukumbatia kabisa na halina future ya kujikomboa kama taifa, Bali maendeleo yatabaki kwa mtu binafsi ila sio kama taifa.

Wakati tatizo hili limeanza zilitoka kauli za Kisiasa kuwa shida maji machache sasa hivi mvua ni za kutosha mbona bado shida ipo?

Miradi kila siku haiishi sasa kwa hali ilivyo watu wakisema kwamba kuna upigaji na biashara zinaendelea nyuma ya huu mgao na serikali imeshindwa kuwadhibiti watakuwa wanakosea?

Kwasabu serikali imewapa watu sababu ya kusema ili tuache kusema udhaifu huu serikali itufanyie jambo moja tu.. UMEME UWE WA UHAKIKA!

Miaka michache nyuma at least umeme ulikuwa wa uhakika na bei za kuusambaza zilikuwa nafuu sana lakini miaka michache mbele Umeme ukawa ni wa kuungaunga na bei za usambazaji kuongezeka yaani tunafanya kazi ya kupiga hatua 7 mbele alafu tunarudi hatua 14 nyuma what a shame!

Vinginevyo tatizo hili la umeme huenda lipo Kisiasa Zaidi yaani Create the problem then solve it, To gain popularity and truth from society ukizingatia tunaelekea 2025 au kuna watu wanaihujumu serikali ya awamu hii ili iwonekane ni mbovu mbele ya raia ukizingatia tunaelekea 2025 au Ni upigaji ambao hata wakubwa huko juu wanafaidika nao na wameamua kutupuuza wananchi au yote kwa pamoja yanawezekana.

Mwisho ni seme kuwa Kuachia tatizo lizidi kuwa kubwa ni kutengeneza chuki kwa jamii dhidi ya serikali yao na itafika kipindi hakuna atakaeweza kuvumilia tena.
bilashaka unaizungumzia Africa Kusini ya mzee Cyril Ramaphosa...
 
Kama Fusso Tipper iliyotupwa Japan hapa ina Kodi ya 45m ni Nchi masikini bado...Bajaji inafika 8.5m daah tunabaki kujisifia meli zimejaa bandarini kwa Mizigo ya Zambia na DRC.
 
Alafu wanawakaribisha wawekezaji, kuja kuwekeza kwenye guza?
 
Tatizo la umeme halisababishwi na mtu mmoja mkuu, Kuna kikundi cha watu ambacho inahitaji ujasiri kukivunja chote, In short ni chain kubwa kwenye wizara kubwa kama ya nishati na shirika kubwa kama TANESCO ni ngumu kwa mtu mmoja kufanya hujuma hivyo ni chain flan hivi ambayo hata ukimuondoa mmoja wengine wanaendeleza hujuma
Hapo Dawa ni ku-format tu ondoa wooooote waliopo safisha shirika zima alafu leta wapya wasio na vinasaba vya wale waliokuwepo kabla
 
Back
Top Bottom