Wewe kila siku unamlaumu tu mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani wakati kila mtanzania mwenye akili timamu ameona namna mh Rais wetu mpendwa alivyofanya kazi kubwa ya kuwatumikia watanzania, kila mmoja na mtanzania ameona namna mh Rais wetu mpendwa alivyopambana na suala la mfumuko wa Bei hapa nchini,
Mfano katika kilimo mh Rais wetu mpendwa alitoa billion Mia moja hamsini, Jambo lililopelekea kushuka kwa Bei za mbolea hapa nchini ukilinganisha na mwaka Jana, Jambo litakaloongeza na kuchochea uzalishaji msimu ujao,
Mh Rais wetu mpendwa pia amekuwa akitoa Ruzuku ya mabillioni katika Nishati ya mafuta, hata mwezi huu serikali imetoa billioni 65 Kama Ruzuku , Jambo lililopelekea kushuka kwa Nishati hiyo ya mafuta ambayo Ni injini ya uchumi,
Pia katika kugusa maisha ya watanzania mh Rais wetu mpendwa amekuwa akisogeza huduma karibu ya mwananchi Alipo, lakini pia amefanya kazi kubwa ya kusambaza huduma za maji Safi na salama, umeme Hadi vijijini huko Jambo lililopelekea kuibua fursa mpya za ajira kwa vijana na akina mama makundi ambayo Ni makubwa
Hata katika suala la kuvutia wawekezaji na watalii mh Rais wetu mpendwa amefanya kazi kubwa Sana kutokana na kuimarisha diplomasia yetu,Jambo linalosaidia pia upatikanaji wa fursa za ajira kwa vijana na kuongeza wigo wa mapato,
Mambo aliyofanya mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani Ni mengi Sana na huwezi ukayamaliza kuyaainisha hapa, kikubwa punguza na ondoa chuki zako kwa mh Rais wetu mpendwa