Taifa Star kufungwa, tatizo ni uwezo mdogo wa kocha?

Jaji Lubuva wapiii? Tanzania tutashinda kwenye kura tu hizo tunaweza pindisha ukweli. Lakini sehemu nyingine kuchapwa ni muhimu.
 
Kwani hawakupeleka jaji wa kuhesabu magoli?
 
Rais alishasema hakuna kusafiri bila kibali chake au ombeni sefue halafu nyie mnasafiri bila ruhusa au mlitarajia nini?
lazima mtii sheria bila shuruti lakini kwa habari zilizonifikia ni kwamba Jecha wa ZEC anafuta yale matokeo ya seven o clock na mechi itarudiwa ndani ay siku 90.
Huo ndo uzuri wa kuwa na wazee kama Jecha wenye busara sana na wanaoifanyanya tanzania iendelee kuwa nchi ya amani , mshikamano na yenye watu wanaopendana kwa dhati.
 
Hapa kazi tu. Nasema kutoka sakafu ya moyo wangu nitaboresha Taifa Stars. Narudia tena sitawaangusha.Selema Selema selema!
 
Kama dawa ni kubadili makocha basi nadhani sasa hvi tungekuwa tumeshashiriki fainali za AFCON achilia mbali WORLD CUP!

Tatizo siyo kocha bali tatizo ni mfumo wetu wa michezo hususani soka. Hatuna mipango wala mikakati ya ya muda mrefu na ya makusudi ya kuinua soka ila tunakwenda kwa mihemuko tu na kuokoteza wachezaji bila kuwa na maandalizi ya maana. Maandalizi hayatakiwi kufanyika unapokuwa na mechi tu bali yanatokana na sera nzuri ya michezo na uwekezaji wenye tija kwenye michezo husasani timu za taifa. Mambo ya zima moto kila kwenye jambo ndiyo yanayo tu cost

Ukifuatilia kwa undani mataifa yote ya afrika yanayofanya vizuri yalifanya uwekezaji wa kutosha kwa kipindi kirefu kuanzia sera zao za michezo na kuiwezesha timu yao kiamaandalizi. Hata michezo mingine kama ndondi, riadha, basket ball n.k tatizo ni hilohilo hakuna tofauti na soka. Kwa hiyo tatizo siyo makocha tatizo ni TFF na Serikali kwa ujumla wake katika kuipa kipaumbele michezo. Tunaupa kipaumbele UFISADI tu kila mahali. HICHO NDICHO WATANZANIA TUNAWEZA. Na laiti kungekuwa na mashindano ya UFISADI AFRIKA basi tungekuwa tunatinga hata Fainali.
 
Wamepigwa wiki (tukafanye nini wakati wachezaji maccm )
 
Hakuna noma it is just a matter of time Jecha will do the needfull na hao waarabu hawataamini kilichotokea
 
Kwanza ilikuaje tukafungwa chache vile tumejitahidi kwel kwel
 
mmeviona viwanja vinavyochezewa ligi kuu na ligi zingine? ccm ni ileile viwanja ni vya ccm halafu we mwenyekiti wa TFF nenda kafungie kiwanja cha ccm uone kama utakaa kwenye kiti chako.

viwanja wananvyofanyia mazoezi mmeviona? uta-slide vipi?

chakula wanachokula watoto wetu ambao kesho tunategemea wawe wachezaji hodari mmekiona? full utapiamlo na ccm haiboreshi hali za maisha yetu (kama unapata milo mitatu maridadi hii haikuhusu utakuwa huna uzoefu na rhumba)
 
Taifa stars kushindwa mimi naona ni kawaida na nilijua tutafungwa japo sikufikiri kufungwa magoli mengi vile, 7-0?
Ila nani anaweza kututajia kitu ambacho Tanzania tunaeza kushindania tukashinda.
Hata tukimpata Wenger, Morinho au Huyo unaemjua wewe bado tu!
Cha msingi Serikali nzima imeshindwa hatuna malengo ya kufanikisha kitu chochote kwa njia nyoofu, tumezoea ujanjaujanja tu.
Kama hata viongozi wanapatikana kwa njia zisizo sahihi unategemea nini?
 
Kama club kubwa kama Simba hata uwanja haina inadowea pale chuo kikuu inafukuzwa kufanyia zoezi unadhani kuna mkakati wa soka hapa kweli?
Hapa hata ulete Arsene Wenger au au Mourinho hakuna kitu..kocha sio tatizo bali miundombinu na misingi mibovu ya soka letu.....mambo mengine inabidi tujitoe tu kwani ni aibu mno.....
NB: Hata mchezo wa kitandani nadhani tunaweza shindwa kama ukichezwa live...shame on you all Tanzanians
 
kWANI MECHI ILIKUWAJEE JAMANII???

Algeria 7- 0Tanzania ...
Na kwa ujinga wa Watanzania they expected to win the game in a foreign country ...if they couldnt dare in Malawi, how did they expect on such a big team in Africa?
Nadhani tatizo ni hiyo figure ambayo ni 7 ...ingekuwa less than five nadhan hata hizi comments za hasira tusingeona
 
Timu yetu ya taifa leo imefundishwa mpira na Algeria kuwa kuipgwa 7-0! Hii ni rekodi.Sijawahi ktk akili zangu timamu kuwahi kusikia Tz ikipata kisago cha aina hii. Sote tunawajibika lakni wewe ni zaidi.

Kwa mtazamo wangu wewe mwalimu wetu, pamoja na ubora wa Algeria, umeonesha udhaifu mkubwa sana ktk michezo yote miwili. Kama ungekuwa makini zaidi tungeweza kupunguza aibu hii ya milenia kwa mchi yetu.

Udhaifu wako mkubwa unatokana na kuendana na matakwa ya mashabiki hasa wanaoendekeza unazi wa Simba na Yanga. Ukiendelea kufanya hivi utaipoteza timu haraka na utajikuta unakalia kiti cha moto.

Udhaifu wako pamoja na benchi lako la ufundi unatokana na kile ulichodai kuwa sub ulizofanya taifa ndio ziliigharimu timu kitu ambacho si kweli. Ulifanya hivi kuwarishisha watu fulani ili kuficha udhaifu wa kweli wa timu ambao ni kupoteza umakini kwa defence yetu(loss of concentration). Unajua kuwa magoli yalirudishwa sio kutokana na timu yetu kuzidiwa na mashambulizi, la hasha! Ilitokana na ukosefu wa umakini wa walinzi wetu hususani Ngwali na Cannavaro. Unajua goli la kwanza lilifungwa wakati walinzi wetu wakimiliki mpira na kupigiana pasi za hapa na pale na walipopokonywa goli likafungwa. Unajua pia kuwa morali ya timu ilishuka sana baada ya goli hilo kiasi cha kurudia makosa yale yale yaliyopelekea goli la pili. Wewe ni shahidi kuwa Algeria walikuwa wameshapoteana kabisa baada ya kufungwa magoli 2, na kwamba magoli yao ilikuwa ni sawa na kuokota embe jangwani. Narudia tena, pamoja na sub zetu Ndemla na Ngassa kushindwa kufanya jipya ktk timu, lakini Mkwasa na benchi lako mnajua magoli waliyopata Algeria hayakutokana na pressure yao kuwa kubwa kwenye lango letu, laa bali udhaifu wa ulinzi na utumiaji wao bora wa nafasi.

Hapa ulijiweka ktk mtego wa kujiaminisha kuwa timu ile ya kwanza iliyoanza Taifa ndio ilikuwa bora zaidi na kwa maana nyongine ulitaka icheze hiyohiyo tu, nadhani tena bila sub!!!!! Inaweza kuwa kweli lkn hukupaswa kukariri. Hukupaswa kuwaza kishabiki, wewe ulitakiwa kuzingatia weledi wako kuelewa tatizo ilikuwa nini kiufundi. Ulipaswa kuangalia mazingira ya mechi.

Na ni kosa hili tena ndio limepelekea timu kupigwa kipigo cha milenia leo huko mjini Blida, Algeria. Tatizo sio kuwa kikosi chetu ni wabaya, hapana, tatizo ni kukariri na mazoea bila kujali mazingira ya mechi.Ulishindwaje kujua kuwa ni makosa kuanza na fowadi watatu hadi wanne ugenini kupishana na timu kama Algeria? Hebu fikiria wao walipokuja taifa pamoja na ubora wao lkn waliweka washambuliaji wawili tu na wakati mwingine akawa anabaki 1. Lkn wewe kwa sifa za Dar ukaona uweke 3!!!

Kutokana na ubora wa Algeria lkn ulipaswa kubadilisha mbinu kidogo tu ili kuwachanganya ambapo ktk nafasi ya Maguli, ungemwanzisha Malimi Busungu, kucheza kama winga mwongo wa kulia lkn mwenye majukumu makubwa ya ukabaji na kumsaidia Kapombe na hapo hapo kutengeneza nafasi kutokea winga ya kulia.

Samatta alipaswa kuanzia kushoto kwenye nafasi ya kijana Farid Mussa na mshambuliaji wa kati angekuwa Thomas Ulimwengu wakati kiungo cha ukabaji wangecheza Mkude na Himid Mao huku ukimpunguzia kazi ya ukabaji kijana mdogo Mudathir Yahya ambaye angeweza kusaidia kulainisha mipira na kuipandisha timu.

Kutokana na tamaa ya kushambulia, umewapa kazi sana Himid Mao na Mudathiri kuwakaba Algeria kiasi cha kusababisha timu kufa katikati, huku muda wote mipira ikiwa miguuni mwa Algeria na kuwapa wakati mgumu sana walinzi wetu. Narudia tena pamoja na ubora Algeria lkn Mkwasa nabenchi lako umewarahishia sana kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…