Taifa Stars aongezwe Manula, Kibabage, Sureboy na Mkude

Taifa Stars aongezwe Manula, Kibabage, Sureboy na Mkude

Aliyeeita hiyo timu kichwa cha mwendawazimu alikuwa sahihi. Maana hakuna timu pale.

Kocha mwenyewe wa timu ya Taifa uwezo wake ni wa kufundisha timu za Namungo, Coastal Union, Mlandege, nk! Halafu ndiyo tutegemee maajabu!!
Naamini mbinu za Baresi yule wa mashujaa na Ahmad Ally japo ni kijana. Hata mgujda sio mbaya sana lakini Morocco na Mkwasa hapana.
 
Wachezaji wote wa Yanga wanahitajika sana katika timu ya Taifa ili iweze kufika mbali, kwasababu wa Teamwork safi na ni wabobevu na wana damu ya Ushindi

Mapovu ruksa na hayabadilishi ukweli
 
Wachezaji wote wa Yanga wanahitajika sana katika timu ya Taifa ili iweze kufika mbali

Mapovu ruksa na hayabadilishi ukweli
Nilitaka kusema hivyo hata mm ila niliogopa mapovu. Pale Yanga hata denis Nkane anaweza kujisaidia taifa hili
 
Mnazidi kuongeza wachezaji ambao hata kwenye timu zao wanasugua benchi na wengine hawana timu kabisa eti ndiyo wakalisaidie taifa. Timu inahitaji washambuliaji nyie mnataka kuongeza walinzi na viungo wakabaji.

Nitaanzisha kampeni Bocco arudishwe timu ya taifa. Bocco ana hekaheka kuliko hata Samatta na anakupa matumaini anaweza kufunga hata kwa papatu papatu.

ilibidi tuwaze AFCON ya 2027 tutakayokuwa wenyeji kwa hiyo ilibidi tuanze kuwatumia kina Chasambi, Shekhan na Karabaka ili kujenga timu ya ushindani siyo kutegemea maji ya jioni halafu tukija kuandaa tunakula hatuna timu tunatolewa hatua za makundi.
 
Back
Top Bottom