Taifa Stars imeshinda kwa kudra za Mungu tu, haikustahili

Taifa Stars imeshinda kwa kudra za Mungu tu, haikustahili

Timu haina mipango ni butuabutua kiukweli namibia walistahili ushindi sema bahati haikuwa kwao
 
Hamna team pale na kama kungekuwa na VAR jana Namibia walikuwa wapewe tuts
 
Huu ndio ukweli unaofichwa, shukrani zimwendee Mwenyezi Mungu pekee, baada ya Stars kufunga goli, dk zote zilizosalia tumepumulia mashine, kuna wakati nimeshangaa wachezaji wa Namibia kukosa magoli ya namna ile mbele ya difensi yetu mdebwedo kiasi cha kushangaza na kuleta maswali ya kutaka kujua walikookotwa mabeki wetu.

Timu haijui kujilinda wala kukaba kiasi kama tukikutana na timu yenye kasi tutapigwa kontena la magoli .

Sijivunii ushindi tulioupata maana ni ushindi wa Bahatisha Ndulute.
Timu hamna kila kitu Ile ,defence ya hovyo sijawah ona , backbass za hovyo na watu wanabutua butua Tu mipira hovyo hovyo..... , nilishangaa mpira upo gorini kwetu mabeki wote wanauruka mpira ,alaf striker za Namibia na wao kimeo et anapiga nje , huu ni ushindi wa Mungu tuu Kwa kweli..... Mtu anatoa passi hatanui anabaki ameganda tuu, winga akipewa mpira haangalii wenzake anaangalia chini af anaanza relay kama nyumbu wa kiangazi ... Kingine wanacheza rafu za kindezi Sana ....kidog Manula na midfielder flan sjui nan Yule ,but the entire team ni hovyoooo
 
Kama mwamuzi angekuwa makini kwa rafu za kiboya tulizokuwa tunacheza kulikuwa na red card 2
 
Yeye na mwajiri wake walimgwaya yule mzee mjuaji wa kila kitu. Binafsi siwezi kuwalaumu, ingawa ni ukweli ulio wazi! Ndairagije uwezo wake ni wa kufundisha tu vilabu.

Kupewa timu ya Taifa, tena kubwa kwa Ukanda huu wa Afrika Mashariki la Tanzania, huku yeye mwenyewe akitokea ka nchi kadogo kama Burundi, hakika ni dharau kubwa kwa Makocha Wazawa. Hawana budi kujitafakari na kuona ni kwa namna gani hawaaminiwi na TFF.
Kabisa braza yaani selection yake ya kuwa kocha wa timu ya taifa haikuwa chaguo sahihi.

Suala la federation za africa kutokuwaamini makocha wazawa limejionyesha ata kwa nchi zingine kama uganda zimbabwe....kwa hii tournament kulikuwa na ulazima gani kuwa na foreign coach kama head coach? Hao makocha wazawa watapata wapi nafasi ya kujiuza kwenye major tournaments ukizingatia kuwaa chan ndio kama worldcup yetu sie watz?
 
Tukifungwa: Kichwa cha mwendawazimu kila mtu anajifunza kunyoa.

Tukishinda: 1. Tumebahatisha wala timu haikucheza vizuri
2. Wametuachia tu kwakuwa wao hawakuwa na pressure na hii match (Eg. TZ vs Ug)

Sijawahi kuwaelewa waTanzania wenzangu.
Japo nakubali timu bado sio nzuri. Ila sijawahi kuona hata siku moja tukaikubali timu hata kama siku hiyo tumeshinda au tumefungwa.
Hata wakati mwingine Saambovu husema kweli.
Hujawahi kuwaelewa watanzania wenzio lakini umekubali timu siyo nzuri, hapo tumeelewana.
 
Yeye na mwajiri wake walimgwaya yule mzee mjuaji wa kila kitu. Binafsi siwezi kuwalaumu, ingawa ni ukweli ulio wazi! Ndairagije uwezo wake ni wa kufundisha tu vilabu.

Kupewa timu ya Taifa, tena kubwa kwa Ukanda huu wa Afrika Mashariki la Tanzania, huku yeye mwenyewe akitokea ka nchi kadogo kama Burundi, hakika ni dharau kubwa kwa Makocha Wazawa. Hawana budi kujitafakari na kuona ni kwa namna gani hawaaminiwi na TFF.
Kwenye muktadha wa Soka kanchi kadogo' Kama Burundi unamaanisha Nini!
Nijuavyo Mimi Burundi wanatuzidi kwenye Menejimenti na utawalawa Soka!!
Sisi tunawazidi kuwa na Wahindi na Waarabu wapenda Soka Basi!
 
Half time tulikuwa tunaongoza kwa possession 55% kwa 45% na mashuti.kipindi cha pili baada ya kufunga goli wapinzani wakaamka sana hata mechi inaisha wakawa wanaongoza umiliki kwa 51-49%,hii hali ndo huwa hivyo karibu kwa game zote ambazo timu zinalingana viwango hata mechi ya Simba vs Yanga ilikuwa hivyo mpaka ikawalazimu Yanga kuzuia tu dakika za mwisho.
Ni kweli hatukucheza vizuri mechi na Namibia lakini tuliwazidi ile tamaa ya kupata ushindi,hata mechi yenyewe haikustahili kabisa sisi kupoteza kwa jinsi timu zote mbili zilivyocheza.
Kitu ambacho wengi wetu tunakilalamikia ilikuwa selection ya wachezaji huwezi kuacha wachezaji ambao walikuwa wanaanza kwenye timu mwezi tu uliopita Mkude,Zimbwe,sureboy kina Idd nado ukaenda chukua watu ambao hawajawahi hata kuvaa jezi ya timu ya Taifa.
Sasa kama kosa limekwishafanyika basi twendeni na hao hao tulionao,tumekuwa watu wa lawama sana wabongo yani.Ukweli ni kwamba tusiaminishane ujinga sisi hatuna timu ya kufikia nusu/fainali ya mashindano ya mpira kwa afrika sio taifa hata klabu pia ndomana ntashangaa sana kama mashabiki wa Simba(wanaojua mpira)watalalamika wasipofika nusu fainali CAF kama wanavyoaminishwa.
 
Kwenye kufanikiwa kuna mambo mawili
JUHUDI na BAHATI
Unaweza ukajituma sana lkn kama bahati sio yako huwezi kufanikiwa sasa chicho ndicho kilichowakuta wapinzani wetu
 
Back
Top Bottom