Jamani wana JF na wapenda soka, Januari 22 mwaka huu kuna mechi kali ya timu ya Taifa letu, Taifa Stars na Timu ya Taifa la Rwanda, Amavubi. Mtanange huu utafanyikia Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Kwa mujibu wa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), VEDASTUS LUFANO. TFF wanasema VIP 20,000, viti vya kawaida 10,000 na mzunguko buku tat tu! Taifa Stars oyeeeeee!