Taifa stars kumenyana na Rwanda-Amavubi CCM Kirumba!

Pwaaaa

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2013
Posts
248
Reaction score
67
Jamani wana JF na wapenda soka, Januari 22 mwaka huu kuna mechi kali ya timu ya Taifa letu, Taifa Stars na Timu ya Taifa la Rwanda, Amavubi. Mtanange huu utafanyikia Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Kwa mujibu wa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), VEDASTUS LUFANO. TFF wanasema VIP 20,000, viti vya kawaida 10,000 na mzunguko buku tat tu! Taifa Stars oyeeeeee!
 
Ni Taifa Stars "Maboresho" ile iliyokuwa kambi Mbeya na sii hii Taifa Stars ya kina Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Hassan Kessy, Joram Mgeveke n.k
 
Tutafungwa tu,pesa za maendeleo ya soka tunajengea maduka!
 
Mie sio mtoa taarifa ila mjumbe wa Kamati ya Ufundi wa Amavubi
 
Jamani wana JF na wapenda soka, Januari 22 mwaka huu kuna mechi kali ya timu ya Taifa letu, Taifa Stars na Timu ya Taifa la Rwanda, Amavubi. Mtanange huu utafanyikia Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Kwa mujibu wa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), VEDASTUS LUFANO. TFF wanasema VIP 20,000, viti vya kawaida 10,000 na mzunguko buku tat tu! Taifa Stars oyeeeeee!
Kikosi cha Taifa cha maboresho tar 22/01,Kitapambana na timu ya Rwanda ya Taifa umri chini ya miaka 23 hapo CCM Kirumba.Majadiliano kati yetu na chama cha mpira mkoa wa Mwanza yanaendelea ili kupanga kupanga kiingilio kidogo kitachowawezesha wadau wengi kuona mechi hiyo.
 
Wasituletee FDP....wakatumalizia Si....mwz
 
Big move JM ,,,nakupa Happy new yr kamanda
 
Tutafungwa tu,pesa za maendeleo ya soka tunajengea maduka!

FIFA wana kitu kinaitwa "income generation projects" huu ni mradi mkubwa wa FIFA kusaidia vyama wanachama vipate vyanzo vya ziada vya mapato ili yasaidie shughuli za maendeleo ya mpira.Malawi wana mgahawa,Mauritania wamejengewa recording studios,sisi tutajenga maduka na budget hotel
 
Ni Taifa Stars "Maboresho" ile iliyokuwa kambi Mbeya na sii hii Taifa Stars ya kina Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Hassan Kessy, Joram Mgeveke n.k
uko sahihi sembo lengo la mwalimu ni kuwajenga vijana ambao baadae watakuwa nguzo ya Taifa stars.Kwa mfano tumesikia Bocco kaenda nje majaribio,Samatta na Ulimwengu wako Kongo sasa tujiulize mchezaji gani wa mbele mzoefu atacheza CHAN qualifiers(Afcon ya wachezaji wa ndani) mwezi June.Hilo inabidi tulihangaikie sasa hivi sio tusubiri mashindano yaanze.
 
Last edited by a moderator:

Jamal Malinzi lengo lako ni zuri maana bocco yupo algeria mda huu, ila nina swali moja.. Hawa vijana wa taifa stars "maboresho" wapo kambi tangu kipindi kile? Au ligi ilipoanza mkawapa likizo?
 
sembo ni muhimu vijana wapate regular games ili wakati wote wawe fit kimchezo.Tunashukuru vijana wa maboresho wamesajiliwa kwenye timu za ligi kuu na daraja la kwanza na wanacheza ligi.Tar 18/01 tutawakusanya kwa ndege tuwapeleke Mwanza na baada ya mechi watarudishwa kwenye vilabu vyao kwa usafiri huo huo.
 
Respect kwako Jamal Malinzi maana vijana wanapata regular games week in week out. Kwa mtizamo wangu wangekuwa pamoja tangu kipindi kile hadi sasa, huku mkiwapatia mechi za majaribio maybe baada ya wiki 2, hivi sasa wangekua bora zaidi [maybe bugdet ndo chanzo ila next time mlifirie hilo].
 
Last edited by a moderator:
Habari kuhusu mechi ya timu ya taifa imeandikwa kwa kifupi tu, na hapo hapo wamesisitiza mpango wa hela(kiingilio), hivi hakuna taarifa nyingine muhimu kuhusu hii mechi ila ni shilingi 20,000 tu.
 
hapana Salamander kiingilio hakitakuwa 20,000.- kitakuwa cha chini ili kuruhusu wadau wengi waone mechi Tanzania vs Rwanda.Tutatangaza viingilio punde.
 
Last edited by a moderator:
Jamal Malinzi

Nyinyi ni viongozi wa ajabu sana ambao macho yenu yana cover ya ndui isiyoona mbali. Mnafanya mambo kipumbavu sana kiasi kwamba hakuna la maana lolote ndani ya nchi upande wa soka. Hakuna lolote tangu uingie ni mavi mavi tu. Samahani nakupa tu ukweli maana vichwa vyenu vimejaa sugu masikio yana gundu hata hamuwezi kusikia, shenzi sana.

Hivi hii nchi nzima yenye mikoa zaidi ya 22 hamuwezi kutafuta wafadhili nje wawape pesa mzitumie kutafuta vipaji kuanzia ngazi ya kijiji kwa mchujo mpaka taifa? hamuwezi kushindwa kupata 11 wachezaji wakali sana kuliko mnavyookota wachezaji wasasa hivi. Yaani usimamizi mkali ufanyike kusaka 11 nchi nzima tukose kweli timu ya kuifunga spain? Kwa taarifa yako kuna vipaji sana nchi hii vya soka tatizo mmeviweka matakoni tu. Mmenikera sana eti timu ya taifa ya maboresho nyoooo, fanyeni kwa kumaanisha acheni utani.
 
Last edited by a moderator:
Asante kwa ufafanuzi mzuri,elimu hii mngekuwa mnatupa wadau wa soka kabla ya kuanza Program zenu zingepunguza haya maneno maneno.
FIFA wana kitu kinaitwa "income generation projects" huu ni mradi mkubwa wa FIFA kusaidia vyama wanachama vipate vyanzo vya ziada vya mapato ili yasaidie shughuli za maendeleo ya mpira.Malawi wana mgahawa,Mauritania wamejengewa recording studios,sisi tutajenga maduka na budget hotel
 
FIFA wana kitu kinaitwa "income generation projects" huu ni mradi mkubwa wa FIFA kusaidia vyama wanachama vipate vyanzo vya ziada vya mapato ili yasaidie shughuli za maendeleo ya mpira.Malawi wana mgahawa,Mauritania wamejengewa recording studios,sisi tutajenga maduka na budget hotel

Mkuu Malinzi, hili wazo lenu si baya sana lakini sisi wapenzi wa soka tunaona sio la lazima kwa sasa. Wekezeni tu ktk mpira wenyewe kama vile kuaanzisha mashindano ya vijana wadogo au kuwa na kituo kama kile kilichopotea cha TSA. Au basi kuzeni zaidi brand ya Ligi Kuu na Ligi daraja la kwanza pesa itakuja tu kupitia viingilio na udhamini.

Bora hata mngelirudisha kombe la Nyerere ili wachezaji wacheze mechi nyingi kuliko kuanziasha maduka. Kama FIFA hailazimishi kuwekeza ktk hicho kinachoitwa 'income generation projects' kuwa ni maduka basi achaneni nayo na wekezeni ktk mpira wenyewe. Ni ushauri tu.

After all, je kuna mifano ya mafanikio yoyote ktk miradi hii huko nyuma? Maana kwa nchi ulizozitaja kama Mauritania naona afadhali ya sisi.
 
Back
Top Bottom