Kikosi cha Taifa cha maboresho tar 22/01,Kitapambana na timu ya Rwanda ya Taifa umri chini ya miaka 23 hapo CCM Kirumba.Majadiliano kati yetu na chama cha mpira mkoa wa Mwanza yanaendelea ili kupanga kupanga kiingilio kidogo kitachowawezesha wadau wengi kuona mechi hiyo.Jamani wana JF na wapenda soka, Januari 22 mwaka huu kuna mechi kali ya timu ya Taifa letu, Taifa Stars na Timu ya Taifa la Rwanda, Amavubi. Mtanange huu utafanyikia Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Kwa mujibu wa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), VEDASTUS LUFANO. TFF wanasema VIP 20,000, viti vya kawaida 10,000 na mzunguko buku tat tu! Taifa Stars oyeeeeee!
Tutafungwa tu,pesa za maendeleo ya soka tunajengea maduka!
uko sahihi sembo lengo la mwalimu ni kuwajenga vijana ambao baadae watakuwa nguzo ya Taifa stars.Kwa mfano tumesikia Bocco kaenda nje majaribio,Samatta na Ulimwengu wako Kongo sasa tujiulize mchezaji gani wa mbele mzoefu atacheza CHAN qualifiers(Afcon ya wachezaji wa ndani) mwezi June.Hilo inabidi tulihangaikie sasa hivi sio tusubiri mashindano yaanze.Ni Taifa Stars "Maboresho" ile iliyokuwa kambi Mbeya na sii hii Taifa Stars ya kina Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Hassan Kessy, Joram Mgeveke n.k
Big move JM ,,,nakupa Happy new yr kamanda
Jamal Malinzi lengo lako ni zuri maana bocco yupo algeria mda huu, ila nina swali moja.. Hawa vijana wa taifa stars "maboresho" wapo kambi tangu kipindi kile? Au ligi ilipoanza mkawapa likizo?uko sahihi sembo lengo la mwalimu ni kuwajenga vijana ambao baadae watakuwa nguzo ya Taifa stars.Kwa mfano tumesikia Bocco kaenda nje majaribio,Samatta na Ulimwengu wako Kongo sasa tujiulize mchezaji gani wa mbele mzoefu atacheza CHAN qualifiers(Afcon ya wachezaji wa ndani) mwezi June.Hilo inabidi tulihangaikie sasa hivi sio tusubiri mashindano yaanze.
Jamal Malinzi lengo lako ni zuri maana bocco yupo algeria mda huu, ila nina swali moja.. Hawa vijana wa taifa stars "maboresho" wapo kambi tangu kipindi kile? Au ligi ilipoanza mkawapa likizo?
sembo ni muhimu vijana wapate regular games ili wakati wote wawe fit kimchezo.Tunashukuru vijana wa maboresho wamesajiliwa kwenye timu za ligi kuu na daraja la kwanza na wanacheza ligi.Tar 18/01 tutawakusanya kwa ndege tuwapeleke Mwanza na baada ya mechi watarudishwa kwenye vilabu vyao kwa usafiri huo huo.
Habari kuhusu mechi ya timu ya taifa imeandikwa kwa kifupi tu, na hapo hapo wamesisitiza mpango wa hela(kiingilio), hivi hakuna taarifa nyingine muhimu kuhusu hii mechi ila ni shilingi 20,000 tu.
FIFA wana kitu kinaitwa "income generation projects" huu ni mradi mkubwa wa FIFA kusaidia vyama wanachama vipate vyanzo vya ziada vya mapato ili yasaidie shughuli za maendeleo ya mpira.Malawi wana mgahawa,Mauritania wamejengewa recording studios,sisi tutajenga maduka na budget hotel
FIFA wana kitu kinaitwa "income generation projects" huu ni mradi mkubwa wa FIFA kusaidia vyama wanachama vipate vyanzo vya ziada vya mapato ili yasaidie shughuli za maendeleo ya mpira.Malawi wana mgahawa,Mauritania wamejengewa recording studios,sisi tutajenga maduka na budget hotel