Taifa Stars Vs Malawi

Taifa Stars Vs Malawi

Nimerudisha uzalendo wangu (ulipotea tangu kufukuzwa kwa Maxmo) kwa timu yangu ya Taifa.

Niliahidi sintoishangilia Taifa stars mpaka kocha awe mzawa.
Naleo zimefanikiwa ndoto zangu.
 
Nilisema yanga akishinda lowassa rais na leo tukishinda lowassa rais
Nimeamink mkwasa mwanamabadiliko
 
Jamani, hivi hawa wachezaji wanatoka club zipi? 3.Haji Mwinyi; 6.Himid Mao; 11.Farid Mussa
 
Hakika vijana wana jitahidi sana wanatakiwa kuto ruhusu goli lolote...
 
Hapa bora game iishe maana ule msemo wa kichwa cha mwendawazimu usije kujirudia kipindi cha pili ...... Sijui wanachezaje huko maana nafatilia matokeo tu
 
We Kitoabu kwani ni mieleka hii hadi wawe wanagombana...teh teh...

Ni mechi ya awali ya kufuzu kuelekea kombe la dunia Russia 2018...
Kombe la dunia au la Africa?

Na ile ya Nigeria tulikua tunagombea nini?
Au ni kundi moja na hili?
 
Kombe la dunia au la Africa?

Na ile ya Nigeria tulikua tunagombea nini?
Au ni kundi moja na hili?

Kombe la dunia kaka, hii haina makundi ni mtoano...

Ile ya Nigeria ni mechi ya makundi kuelekea AFCON, na kundi letu ndio kuna Misri, Nigeria na Chad...
 
Nilisoma blog za malawi,wanakilaumu kikosi chao kilichokuja leo.

so ushindi tuushangilie lakini tuwe alert na timu zinazojielewa tutakazokutana nazo mbeleni

hasa Egypt kwenye AFCON marudiano maana hatuna historia nayo nzuri,Simba yangu ingekuwa kwenye form ningesainisha petititon ili mechi hiyo ya Stars vs Egypt kipangwe kikosi cha Simba,Historia haidanganyi(linapokuja swala la Simba vs muarabu yeyote).
 
Hii mechi wala tusiombee iishe kwa magoli haya mawili tu bali tuwachape hawa jamaa goli nyingi iwezekanavyo...

Kuna mechi ya marudiano kwa hiyo lazima tuwe na akiba kubwa ya magoli...

Hapa bora game iishe maana ule msemo wa kichwa cha mwendawazimu usije kujirudia kipindi cha pili ...... Sijui wanachezaje huko maana nafatilia matokeo tu

Wakuu mechi iishe tuu...maana hatukawii kuharibu
 
Back
Top Bottom