TAIFA STARS Vs SUDAN-2nd Leg

TAIFA STARS Vs SUDAN-2nd Leg

sio vile mimi nataka wewe jibu hayo maswali tu halafu uone point yako!kwanini basi hiyo timu yetu ya yanga haijawahi fika kokote?au hao kina ngasa na shadrack nsajigwa wameanza cheza msimu huu hawakwepo msimu uliopita?

naona na kule wawakilishi wetu wa africa kwenye world cup ya clubs wamisri wale wameshafungashwa virago na timu ya mexico..
tungojee man utd tukajichukulie kombe letu tu
 
Jamani, kuna ntu mwenye dataz, timu gani zinaenda kodivwaa!!!!!

Nadhani tuanze kuangalia mbele, SIMBA na YANGA yao ni tusker Cup tu!!!!!
 
We Balantanda, nadhani hunielewi. Ni kweli kabisa maneno yako na ni kweli Stars imeshinda na tunafurahia sana. Ila unasahau point muhimu kwenye maelezo yako. Kuwa wachezaji wa Yanga ndiyo waliofunga. Hii ina maana kubwa sana. Huwezi kuwa na wafungaji ambao hawana mafunzo mazuri huko kwako. Kondic amewafunza vema. Na team yoyote ile, ushindi huwa ni magoli na si chenga wala kuunganisha pass. Ukiwa Ulaya hata ukiunganisha pass elfu moja, kama hujafunga wewe huna thamani kabisa na unaweza kuuzwa kwa mkopo kwa team yoyote, tofauti na wengine wanaouzwa kwa cash.

Sasa wewe hapa huelewi nini?

Yaani ndo wazidi kutulisha 'sumu' mkuu,,wachezaji wa Yanga tu ndo waliofunga!!!!!!.nahodha Henry Joseph(aliyefunga goli la kwanza) kahamia lini Yanga????....mhhhhh haya bwana
 
Hongera MAXIMO kwa kutupeleka Kodivaa
Hongera TAIFA STARS
 
Taifa stars ina wachezaji wengi Yanga but Stars wakishinda wa2 wanamssifu Kondic
Huyo kocha ananiboa anavyomweka benchi Tegete na kuwapanga wakenya
Hakuna cha Simba wala Yanga but TAIFA STARS
MAXIMO katusaidia now tunacheza mpira wa kueleweka hata goli lapili la jana ile krosi ya Ngasa ilikuwa balaa but bado tuna tatizo la STRIKER kila siku magoli wanafunga defender na midfielder
 
Sasa subirini muone Wahishimiwa wanavyojifanya wao ndio walezi wa Taifa stazz!!!!!!

Lazma waitwe Dom, Kisha wapitishwe ukumbini na wachangiwe vijisent!!!!
Muda wote wa maandalizi walikuwa kimyaaa!!! WANANIBOA!!!!!!
 
Sasa subirini muone Wahishimiwa wanavyojifanya wao ndio walezi wa Taifa stazz!!!!!!

Lazma waitwe Dom, Kisha wapitishwe ukumbini na wachangiwe vijisent!!!!
Muda wote wa maandalizi walikuwa kimyaaa!!! WANANIBOA!!!!!!

Mara hii wavae vizuri walau basi maana last time wengine waliingia na kandambili! ( nadhani walikuwa wachezaji wa Yanga wale )
 
hahahaha hilo tu wala msiwe na shaka fweza za epa maadamu zisharudishwa na wenye change zao kuchukua..adogo watashonewa sutiz kabsaa na kupitishwa bungeni,ikulu na kila mahala yaani week hii nzima no mo kesi zozote zile!lets relax guys gurudumu la maendeleo lazidi songa!

n by next week tutaanza sikia rais anaenda likizo yake ya mwaka...so shughuli zoote za kiserikali zitago likizo kama ilivyo kwa wizara yetu ya mambo ya ndani pindi masha akiwa nje!

so ndo twafunga funga mwaka 2008..issue nyingine zozote zingojee mwakani
 
Mara hii wavae vizuri walau basi maana last time wengine waliingia na kandambili! ( nadhani walikuwa wachezaji wa Yanga wale )

Wewe nawe,,kila kitu Yanga Yanga,ama ndo mambo flani ya 'mzimu' wa tarehe 26 October,2008
 
Mara hii wavae vizuri walau basi maana last time wengine waliingia na kandambili! ( nadhani walikuwa wachezaji wa Yanga wale )

Tena wengine walikuwa wanasinzia ukumbini. Sijui kwakuwa walichoshwa na safari (maana walilazimishwa waende Dom bado wa-reo-reo) au walikuwa wanawaiga wazee wa mbonji ukumbini!!!!!! Vere disgusting!!!!!!!!!

Serikali imetimiza wajibu wake, hatuna haja kuwasifia kwakuwa ni sehemu ya majukumu yao. lakini kwakuwa wamefanya tofauti iliyo bora basi twawapongeza kwa hilo. hususan muheshimiwa JK!!!

Nashauri, wanasiasa waache kutumia ushindi wa Stars kwa manufaa yao binafsi!!!

Hao vijana, wakifika wapewe likizo fupi!!!
kisha wapelekwe kambini. ziandaliwe international friendlies au ikiwezekana wapewe overseas trio matches.
Mwezi kabla ya michuano warudishwe bongo. Patafutwe mahali ambapo angalau hali ya hewa yake inafanana na kodivwaa, kisha wawekewe kambi huko.

Muheshimiwa Rais pekee, kwakuwa tunathamini mchango wake kwa Stars aruhusiwe kufanya ziara mara moja tu kwa hiyo kambi. Wanasiasa wengine na wanyabiashara wadandiaji wakatoe pongezi zao kupitia vyombo vya habari!!

Tukisema waanza kutembezwa, basi wataanza Ikulu, Bungeni, Kwa waziri Mkuu, sijui waziri wa miundo mbinu, wa maji, ushirika na masoko, ccm makao makuu, wakimaliza kwa wanasiasa bado wafanya biashara, kwa manji, dewji, serengeti breweries, IPP, Barick, opfuuuu!!!! mpaka wakija maliza mashindano kesho!!!!

Tunathamini sana michango ya wote waliofanikisha ushindi wa Stars, tunaomba waridhike na hilo. wasije waaribu vijana kwa kutaka misifa!!!!!

Ianzishwe akaunti maalumu, kwa wanaopenda kutoa michango zaidi kwa stars. Ikiwezekana michango itolewe kwa siri. Kwa wanaotaka kujitangaza kibiashara, basi waingie udhamini wa stars. MAXIMO awe na kauli ktk matumizi ya pesa za hiyo akaunti. sio mtu tu anakurupuka, nitawajengea nyumba wachezaji, matokeo yake hajengi, wachezaji wanaacha kucheza mpira wanaanza kufuatilia ahadi za kitapeli!!!!
WIZI MTUPU!!!!!!!!
 
Tena wengine walikuwa wanasinzia ukumbini. Sijui kwakuwa walichoshwa na safari (maana walilazimishwa waende Dom bado wa-reo-reo) au walikuwa wanawaiga wazee wa mbonji ukumbini!!!!!! Vere disgusting!!!!!!!!!

Walikuwa wamechoka mkulu,,walivotoka Ougadougou walipitia Mwanza kisha wakaenda Dodoma so hawakupata hata muda wa kupumzika maana kama ulivosema walilazimishwa so kusinzia ukumbini halikuwa kosa lao
 
Kuna tetesi kuwa Mkuu JK kaagiza vijana wafuatwe leo hii kwa kutumia ndege yake iliyonunuliwa wakati wa Mwalimu ili akitoka Dom akutane nao kabla ya kwenda zake nje. Mwenye kujua ukweli naomba atuhabarishe. BRAVO STAAAAAAAAAAAAAZ.
 
Walikuwa wamechoka mkulu,,walivotoka Ougadougou walipitia Mwanza kisha wakaenda Dodoma so hawakupata hata muda wa kupumzika maana kama ulivosema walilazimishwa so kusinzia ukumbini halikuwa kosa lao

Hivi, walipelekwa pale kufanya nini????? hao wabunge si wana kamati ya michezo na utamaduni?? kwanini hiyo kamati isiwatembelee kambini wakiwa tayari washapumzika????
 
Taifa stars ina wachezaji wengi Yanga but Stars wakishinda wa2 wanamssifu Kondic Huyo kocha ananiboa anavyomweka benchi Tegete na kuwapanga wakenya Hakuna cha Simba wala Yanga but TAIFA STARS
MAXIMO katusaidia now tunacheza mpira wa kueleweka hata goli lapili la jana ile krosi ya Ngasa ilikuwa balaa but bado tuna tatizo la STRIKER kila siku magoli wanafunga defender na midfielder

Tanzania ina vipaji vingi sana vya soka. Wachezaji wa kigeni hawana kitu kipya. ni vyema timu zetu zikaliona hilo na badala ya kupoteza fedha nyingi kwa wachezaji wa nje basi, wafundishwe vizuri hawa wa kwetu na pia walipwe vizuri.

Jana usiku kulikuwa na shamra shamra nyingi sanaa huku mtaani, baada ya goli la pili, tulikuwa tunasikiliza kupitia TBC TAIFA (RTD) Taifa Stars HOYEEEEEEEEEEEEE
 
Bravo Taifa Stars,

Huu ni mwanzo wa mabadiliko na kuwapa comfidence wachezaji kwamba Tanzania tunaweza kuwa kama Nigeria, cameroon, Egypt na wengine kikubwa ni wachezaji waamini wanaweza, Bravo Taifa Stars
 
Back
Top Bottom