IslamTZ
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 309
- 182
Makocha wanajua zaidi lakini sikuona kabisa mantiki ya kumchezesha Boko wala Farid mechi ya ugenini ya Taifa Stars dhidi ya Tunisia.
Boko alikuwa cut-off kutoka kwa wenzake, akipewa mipira ananyang'anywa kirahisi na mabeki wa Tunisia waliomzunguka. Katika mechi hii Samatta angeweza kuonesha tofauti kubwa. Kukosekana kwake kumekuwa ni pengo kubwa kwani tofauti na Boko, yeye Samatta anaweza kukaa na mpira na kukaa nao muda mrefu na anaweza kucheza wide akawa kama wing attacker.
Nionavyo, ni bora tungecheza na false number 9 kwa kumtumia Msuva ambaye anaweza kushuka, kuchukia mipira na kukimbia nao na anaweza kucheza pembeni kama wing-attacker. Pembeni, badala ya Farid, yule mtoto Nado angeanza na kulia alipokuwa Msuva angecheza Ditram.
Watatu hawa, Ditram, Nado na Msuva wangetosha kabisa kuwasurprise Watunisia kwa counter attacks kwani wote wana kasi.