Taifa Stars vs Tunisia: Haikuwa game ya Boko wala Farid

Taifa Stars vs Tunisia: Haikuwa game ya Boko wala Farid

IslamTZ

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
309
Reaction score
182
Makocha wanajua zaidi lakini sikuona kabisa mantiki ya kumchezesha Boko wala Farid mechi ya ugenini ya Taifa Stars dhidi ya Tunisia.

Boko alikuwa cut-off kutoka kwa wenzake, akipewa mipira ananyang'anywa kirahisi na mabeki wa Tunisia waliomzunguka. Katika mechi hii Samatta angeweza kuonesha tofauti kubwa. Kukosekana kwake kumekuwa ni pengo kubwa kwani tofauti na Boko, yeye Samatta anaweza kukaa na mpira na kukaa nao muda mrefu na anaweza kucheza wide akawa kama wing attacker.

Nionavyo, ni bora tungecheza na false number 9 kwa kumtumia Msuva ambaye anaweza kushuka, kuchukia mipira na kukimbia nao na anaweza kucheza pembeni kama wing-attacker. Pembeni, badala ya Farid, yule mtoto Nado angeanza na kulia alipokuwa Msuva angecheza Ditram.

Watatu hawa, Ditram, Nado na Msuva wangetosha kabisa kuwasurprise Watunisia kwa counter attacks kwani wote wana kasi.
 
Umeongea fact lakini bado hana kitu yule sijui mmeona nini kwake.
 
Kidooogo nakubaliana na wewe kwa farid,chenga nyingi anapoteza mipira sana,uzuri wa nchimbi na boko team ikizidiwa wanajua kukaba jihadi sana,leo msuva kashindwa mpa sapoti kapombe kwenye kukaba kabisa,hapo mbele bora iwe samata,boko,pembeni msuva kushoto aanze hata nado. Farid ana kipaji sana ila dah simuelewi siku hizi
 
kidooogo nakubaliana na wewe kwa farid,chenga nyingi anapoteza mipira sana,uzuri wa nchimbi na boko team ikizidiwa wanajua kukaba jihadi sana,leo msuva kashindwa mpa sapoti kapombe kwenye kukaba kabisa,hapo mbele bora iwe samata,boko,pembeni msuva kushoto aanze hata nado..farid ana kipaji sana ila dah simuelewi siku hizi
Hivi huyo nado mbona mnamkuza sana mkuu.. ila farid chenga nyingi
 
Kwangu Farid ndiye Mchezaji wangu bora kwa zile dkk 30, hakubutua mpira kamwe na alitulia pindi alipopokea mpira.
 
Jana farid ndio aliyekuwa anaonyesha uhai kidogo,nado anarukaruka tu
 
Farid zero kabisa, hata mechi za home anakosa magoli ya wazi mengi, alienda Spain kula burgers tu, pumbaf
 
Nado ana kipaji ila kuna tofauti ya mpira wa kuanzia academy na ndondo kocha anatakiwa ambadirishe baadhi ya vitu ili awe bora zaidi
Nado na Farid' wote wazembe kwenye kufanya maamuzi kwenye box' pia hata pasi zao wanachelewesha sana' yaani wanapenda kumiliki mpira muda mrefu kitu kinacho fanya wanapoteza mpira mara nyingi

nazani angeanza ditram nchimbi huyu jamaa ni mzuri kwenye mashambulizi.., killer pass, na kudefense..
 
Back
Top Bottom