Taifa Stars waenda Cape Verde bila Dreamliner

Taifa Stars waenda Cape Verde bila Dreamliner

Jiweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee njoo usikie wanavyomsema mtoto wako! Hawana adabu
Hili linalotokea ni sawa na babu kakaa na mjukuu, babu kajamba mjukuu ndio anakula kofi kuwa mbona anajamba hovyo? Ila waungwana wanajua nani hasa!
Inaitwa heshima kwa wakubwa. Mwakyembe vumilia tuu
 
Mimi bado naona mauzauza tu. Ratiba ya mechi inajulikana. Waziri anatangazia Taifa na wapenzi wa soka kuwa kuna usafiri wa ndege ya serikali (dreamliner). Kila anayehtaji kwenda anatakiwa kuchangia "gharama kidogo tu" dola 1500 - 2000. Siku ya safari wameshajitokeza watu 262 wa kujaza Dreamliner, ghafla inagundulika uwanja wa ndege kumbe ni mdooooogo!! Unafaa kutua helkopta na ndege ndogondogo tu. Binafsi nachanganyikiwa sijui abiria zaidi ya 200 waliotoa nauli zao tutawaambia nini? Tingewaambia mapema watangulie na boti za Azam wangeshafika masikini!! Hata hivyo hakijaharibika kitu, kama uwanja ni Mdogo na tumeahindwa kuonesha "Fahari" yetu basi kesho ile meli yetu tuliyohifadhi jeshini kama silaha ya akiba (Mv Dar es salaam) ianze safari Mara moja. Hatuahiiiindwiii!
Meli yetu ile? Acha masihara wewe! Kwa ule mwendo wake sii itafika Cape Verde mwezi February 2019?
 
October 9, 2018
Dar-es-Salaam, Tanzania



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amesema Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania – Taifa Stars kitaondoka usiku wa leo kuelekea mjini Praia, Cape Verde kwa ndege ya kukodi kuifuata timu ya taifa ya huko kwa ajili ya michuano ya kufuzu kwa michuano ya AFCON inayotarajiwa kufanyika mapema mwakani.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kambi ya timu hiyo Waziri Mwakyembe amesema, mabadiliko ya safari hiyo kutoka Dream Liner na kuamua kukodi ndege yanatokana na ufinyu wa uwanja wa ndege wa Mjini Praia ambao hauwezi kutua ndege kubwa.

Aidha Waziri Mwakyembe amewataka wachezaji wa Taifa stars wakacheze kwa kujituma ili kuibuka na ushindi katika mchezo huo huku akiwasihi watanzania kuiombea timu hiyo.

Kwa upande wake Rais wa TFF Wallace Karia na Nahodha Msaidi wa Taifa Stars Himidi Mao wameelezea maandalizi ya mchezo huo.

Habari & Video kwa hisani kubwa ya:
Source: Global TV Online
kwa maana hiyo nikwamba viwanja vya Mwanza na Kilimanjaro ni vikubwa kuliko Uwanja wa Taifa wa Cape Verde?????
 
Mkuu tuliaa basiii... Usiwaseme hadharan Hawa wazeee.... Hahahahahahah aibu yao
Routes
There are 192 flights on 28 different routes from Praia Nelson Mandela International Airport, connecting RAI to 27 different cities in 14 different countries. The most popular routes connect Praia
Aeroporto internacional da Praia Cabo Verde
Icelandair lands at Praia Nelson Mandela airport
 
Tuache kudanganyana hapa!Mimi nimekaa Cape Verde takribani miezi sita.Wenzetu wana ndege kubwa tatu :airbus mbili na boeing 737-800 Next Generation ambayo ina uwezo wa kubeba abiria si zaidi ya 230. na zote zinapiga masafa ya Europe mpaka Caribbeans sasa huyu mzushi anayesema eti "hawana uwanja wa ndege wa kutua dreamliner ya Tanzania anaumwa au ni mgonjwa?"
HIvi visiwa vinapokea watalii zaidi ya mia sita kwa siku.
WATANZANIA ACHENI UZUSHI WA KIJINGA!
MKUU KWA KUONGEZEA NDEGE ZOTE ZA ENGINE MBIL ZINAZOPITA ATLANTIC OCEAN FLIGHT PLAN YAO LAST PONT NI PALE, LAZIMA ZINATUMIA CAPE VERDE INCASE YA EMERGENCY HATA NASA WAMEWEKEZA SPACE SHUTTLE KUTUA KWA DHARURA
HII INATOKANA NA ETOPS REQUIREMENTS HIVYO HATA TAG ANGOLA YA RIO DE JENEIRO INAPITIA PALE
 
Tuache kudanganyana hapa!Mimi nimekaa Cape Verde takribani miezi sita.Wenzetu wana ndege kubwa tatu :airbus mbili na boeing 737-800 Next Generation ambayo ina uwezo wa kubeba abiria si zaidi ya 230. na zote zinapiga masafa ya Europe mpaka Caribbeans sasa huyu mzushi anayesema eti "hawana uwanja wa ndege wa kutua dreamliner ya Tanzania anaumwa au ni mgonjwa?"
HIvi visiwa vinapokea watalii zaidi ya mia sita kwa siku.
WATANZANIA ACHENI UZUSHI WA KIJINGA!

Ukigoogle utaona kabisa uwanja wa Praia Nelson Mandela una urefu wa 2.1KM inabidi ugoogle tena kuangalia minimum length ya uwanja wa Dreamliner kutua ukipata majibu uje sasa kupingana na hoja ya Mhe.Waziri.Dreamliners zinatua Cape Verde lakini si uwanja huo wa Nelson Mandela Praia.Kuna kisiwa kingine kina uwanja mrefu kwa ajili ya dreamliner ambapo wangetua huko wangetakiwa kusafiri (kwa boti? Au Charter) kuja Praia ambako ndiko Mchezo utafanyika wakaona ni usumbufu bora wakatue hapo hapo Praia(Nimemsikia vizuri Mhe.Waziri).Comments nyingi humu ni za kishabiki suala hapa ni je hizo sababu ni za msingi??Nakubaliana na wanaotoa hoja ya kwamba abiria 200+ hawakuweza kupatikana na hii ni kwa sababu pamoja na mambo mengine ya kiuchumi lakini pia muda ulikuwa mfupi mno tangu tangazo hilo litolewe.
 
Mkuu Vyamavingi Acha porojo na siasa za mwakyembe, weka vipimo vya uwanja wa Praia. Hizo ndege mnazoonyeshwa hakuna B787 naona ni A220 za Cote d'void na B737. Mie nahisi sababu kubwa ni TFF kushindwa kufika bei na ATCL wakachomoa which is right. Mengine ni siasa. Cape Verde in visiwa viwili vikubwa. Sal na huko Praia. Kisiwa cha utalii ni Sal na ndiko kwenye uwanja mkubwa kwa ajili ya madege makubwa unayoyasena. Praia ni makao makuu na mpira utachezwa huko.

QUOTE="Vyamavingi, post: 28710099, member: 251105"]Nimejisikia aibu sana kana Mtanzania pale Dk. Mwakyembe alipowadanganya Watanzania ati Dreamliner yetu haiwezi kutua uwanja wa ndege wa Cape Verde! Mwakyembe inaoneka ama haifahamu Cape Verde au ni mwanasiasa anayetumia ghiliba.

Kama umo humu Dk. Mwakyembe, nakufahamisha kuwa Cape Verde uchumi wake unategemea utalii, Watalii wanakwenda Cape Verde kwa maelfu na hawatumii charter na bombadier kufika huko, wanashuka kwa madege makubwa kuliko hiyo dreamliner.

Vv[/QUOTE]
 
Bora wamempa Mwaki awaambie. Wangelinipa mimi wala nisingeli mung'unya maneno ningeliwapasukia waziiii. Mmepewa fursa kuijaribu mwendo Dream yenu mmeshindwa hata kuchangia tumafuta tu. Kweli Bongo ni bongolala kabisa. Mnataka kuisafirisha boeng yetu tupu kwenda na kurudi?? Ihurumieni basi jama. Hata miye nilikuwa nawaza, hao Watz wenye uwezo huo wa kutaapika $2000 nauli, bado ticket, bado chakula wapo Tz kweli au ma diaspora?? Hapa mnatakiwa kuishi ka ma devil halafu mnazo za kumwaga!! Mhhh
Watu hawakugundua tangu mwanzo kuwa ilikuwa danganya toto kwasababu hiyo nauli ni kubwa mno. Walijua kabisa hakuna wataolipa hiyo nauli hivyo ndege haitakwenda. Na jiwe lazima alikuwa anaangalia tu pembeni anasema hiiiiii. Ndege ingejaa lazima jiwe angewachunguza hao watu.

Kuwaambia watu kuwa uwanja wa Praia ni mdogo kwa ndege yetu ilikuwa ni dharau tu ya kawaida ya viongozi kwa wananchi wao ambao wanawajua ni wajinga na wanadanganyika kirahisi, na siyo ishu kabisa.
 
Kwani lazima watue Praia, mbona wana uwanja mkubwa kimataifa unaitwa "Amílcar Cabral International Airport" urefu 3272m ktk kisiwa cha Sai
 
Inalinda kibarua chake, angesema ukweli ingethibitisha kua tuna hali ngumu kifedha jambo ambalo wakubwa hawataki tuseme
Huu ndio ukweli lkn imeshangaza sana Dr. Mwakyembe kuudanganya watanzania, yaani anatuona sisi mazuzu. Angetoa sababu hata za kiufundi kuwa imepata dharura ingawa kusema ukweli kuwa abiria wamekuwa wachache ingemjengea heshima kuliko uongo alioutumia.

Vv
 
Back
Top Bottom