Taifa Stars ya Jana wangepangwa Wachezaji wengi ya Yanga SC tungefungwa hata Goli / Bao 15 Hongera Kocha

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Huwezi ukawa na Timu ya Taifa yenye Wachezaji mahiri wa Klabu ya Simba SC kama akina Manula, Kapombe, Tshabalala, Nyoni, Mkude na Boko halafu ukafungwa Goli / Bao nyingi na Timu yoyote ile. Hongera sana Kocha wa Taifa Stars Ndayiragije kwa Kutupangia Wachezaji wengi wa Timu yangu bora ya Simba SC. Ungewapanga wengi wa Yanga SC jana 'tungekula' hata 15 pale.

Sasa nakuomba mno Kocha wangu Ndayiragije ambaye nakumbuka nilishakaa mahala na Wewe na ukaniambia kuwa kama kuna Timu ambayo si tu unaipenda bali pia inacheza Soka safi na Wachezaji wake wengi wana 'Vipaji' vikubwa nchini ni Simba SC katika Mechi yako ya 'Keshokutwa' ambayo ni ya marudiano 'Kikosi' chako kiwe hivi tafadfhali na wala usikibadilishe kabisa......

1. Aishi Manula ( Kipa bora Tanzania ambaye jana kaonyesha uwezo mkubwa mno wa Kudaka na anastahili pongezi nyingi )
2. Shomary Kapombe ( Beki ambaye hata angeenda Real Madrid au PSG au Liverpool yangu bado angepata namba Kikosi cha Kwanza )
3. Mohammed Hussein 'Tshabalala' ( Mchezaji ambaye hata Lionel Messi akimuona atawaomba FC Barcelona Wamsajili upesi sana )
4. Bakari Nondo ( ambaye kama mambo yakienda vyema huenda akatua Simba SC )
5. Erasto Nyoni ( Mchezaji ambaye tokea aanze Kucheza Soka Akademi hadi leo hajachuja na hatochuja ng'o hadi akistaafu )
6. Jonas Mkude ( Mdogo wangu na Mwanangu Mwenyewe na Kiungo ambaye bado sijaona wa Kumfananisha nae nchini Tanzania )
7. Simon Msuva ( ambaye hakuna asiyemjua kuwa anaipenda Simba SC tokea akiwa Tumboni mwa Mama yake )
8. Salum Aboubakar ( ambaye anajulikana ni Simba SC sana ila Baba yake anamtishia akija tu Simba SC atamuachia Laana )
9. Ditram Nchimbi ( ambaye kama mambo yakienda vyema nae atatua Simba SC muda wowote ule )
10. John Boko ( Mshambuliaji aliyezaliwa tu kuja Kufunga Magoli na kutoa Pasi za Kufunga kwa Wenzake )
11. Farid Musa ( ambaye 99% ya Marafiki zake wa Karibu hasa Wachezaji ni wa Simba SC na muda wowote anatua Msimbazi )

Na kama Kocha Ndayiragije ukiamua Kufanya 'Mabadiliko' basi ingiza Wachezaji hawa tu Wawili Said Ndemla na Muzamiru Yassin wa Yanga SC NO.
 
Umeandika hapa toka usingizini kweli hivi uliangalia hata huo mpira waliocheza hao unasema Simba Sc?

Kama wachezaji wa Simba kila siku wangecheza vile hapa kwenye league ya bongo kwa kweli watani zangu mngeshuka daraja.

Kuangalia mpira wa jana sisi tulikuwa tunaangalia mpira ndio tulikuwa tunatia aibu kuona ujinga ule wa jana.

Kama na hapa bongo watacheza vile hakika naona tutapigwa zaidi ya 15.
 
Sassi jana alipewa uchochoro mzuri sana na Kapombe kabla Manula hajadaka muguu ya Ben Achour.

1. Mapombe
2. Manula


Ni wachezaji wa timu gani?
 
Polisimba sc
 
Sassi jana alipewa uchochoro mzuri sana na Kapombe kabla Manula hajadaka muguu ya Ben Achour.

1. Mapombe
2. Manula


Ni wachezaji wa timu gani?
Kuna 'Wakala' mmoja wa Wachezaji mkubwa jana nilikaa nae mahala tunatizama 'Game' akasema Wachezaji wa Simba SC 'wanauzika' sana Ulaya.
 
Kuna 'Wakala' mmoja wa Wachezaji mkubwa jana nilikaa nae mahala tunatizama 'Game' akasema Wachezaji wa Simba SC 'wanauzika' sana Ulaya.
Naomba tutajie hao wanaouzika
Maana wengine wana misimu zaidi ya mitano hatuoni hata kwenda kwenye majaribio.
 
Kuna 'Wakala' mmoja wa Wachezaji mkubwa jana nilikaa nae mahala tunatizama 'Game' akasema Wachezaji wa Simba SC wanauzika sana Ulaya.
Kwa ule uchochoro alio ujenga Kapombe Jana.

Kwa kitendo cha Manula kudaka miguu badala ya Achour.

Ni kweli hawawezi kukosa timu ya kuchezea huko Ulaya hasa maeneo ya nchi za Scandinavia.
 
Naomba tutajie hao wanaouzika
Maana wengine wana misimu zaidi ya mitano hatuoni hata kwenda kwenye majaribio.

Mchezaji wa mwisho wa Simba SC kucheza nje ya mipaka ya Tanzania ni Mbwana Samatta.

Nikisema niwataje wa Yanga Server ya jamii forum ita-stuck.
 
Naomba tutajie hao wanaouzika
Maana wengine wana misimu zaidi ya mitano hatuoni hata kwenda kwenye majaribio.
Manula, Kapombe, Hussein, Nyoni, Mkude, Muzamiru, Ndemla na Boko. Nilipomuuliza kwa Yanga SC akasema hajaona 'Mchezaji' wa Kuuza Ulaya.
 
Bado tunaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu , kwa sababu ya haya mambo ya simba na yanga .
Sijui watanzania tutabadilika lini.
Timu ya hispania kuna kipindi ilikua wachezaji ni wa Real Madrid au Barcelona na kwa mbali Atletico Madrid.
 
Mchezaji wa mwisho wa Simba SC kucheza nje ya mipaka ya Tanzania ni Mbwana Samatta.

Nikisema niwataje wa Yanga Server ya jamii forum ita-stuck.
Nasikia Yanga SC mnasema ndiyo mlimpeleka Nonda Shabaan Ulaya wakati ukweli ni kwamba Klabu ya Vaal Professionals ya SA ndiyo ilimuuza nje.
 
Kwa ule uchochoro alio ujenga Kapombe Jana.

Kwa kitendo cha Manula kudaka miguu badala ya Achour.

Ni kweli hawawezi kukosa timu ya kuchezea huko Ulaya hasa maeneo ya nchi za Scandinavia.
Vipi Yanga SC 'Chama' mmeshamchukua? Yaani GSM 'wanawadanganyeni' kweli kweli nanyi 'Majuha' mnawaamini. Tonombe na Nchimbi are RED.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…