Tairi gani za kichina zina afadhali?

Tairi gani za kichina zina afadhali?

Tairi za kawaida nazotumia kwa miaka yote ni Goodride.....hazijawahi nisumbua na naenda safari ndefu mara kwa mara. Tairi nyingine za kawaida nazotumia pia ni "Infinity", hizi tairi niliweka 2016 na mpk leo nazitumia..anaejua zinapopatikana anijuze maana kuna wakati niliulizia sikuzipata huku mikoani. Sijawahi kutumia tairi za bei "mbaya" zaidi ya Dunlop iliyokuja na gari,nilitembelea mpk uzi zikatokeza,nikazivua na kufunga Infinity. Wakati wa kununua huwa nazingatia sana mwaka iliyotengenezwa na kununua kwa dealers. Cheers
Zipo mbona huku kariakoo
 
Mchina Tumia 1. Goodride, 2. Double Star au 3. Linglong
Lkn hapo kati ya Mchina zipo tyre za South Afrika na Japan zinaitwa DUNLOP ni nzuri pia.
Nimetumia sana Linglong na sijawahi kujutia kabisa.
 
Funga Used za japan zinazotka Dubai kwa 45000 utatembelea hata miezi 6 kama uchumi haujakaa sawa ila kama vizuri chana mfuko uchukue Bridgestone.
Wapi mkuu zinapatikana hizo za Dubai ?Mimi Niko ARUSHA mkuu
 
natafuta Dunlop 225 / R65 18.

Nitonye zilipo nikafunge.
 
Hivi kama zile zenye kashata kubwa kubwa R16 au 17 kuna used? Huwa ni how much?
 
Ni kampuni gani ya tairi za china ambayo ni nzuri kuzidi nyingine za china, nimeulizia BF GOODRICH y usa/uk Rim 15,ni sh 280,000/=kwa pisi moja, michelin 180,000/, goodyear 170,000/=, mchina 120,000/=hizo zote ni saizi 15, mchina ni maji usipo kunywa utaoga tu, hata kufulia basi.
Sasa mkuu si bora uchukue tu hiyo Michelin mbona tofauti ya bei ni ndogo sana hapo.
 
Zile zilikuwa zinahimili joto kutoka kwenye rim ambalo linasababishwa na mwendo mkali lkn sasa hivi hata zile zetu general tyre zingekuwepo zingefaa maana ni mwendo wa kobe.
Kwamba general tyres zilikuwa mbovu ama sijaelewa?
 
Unazo size 255/55/18 used from Dubai au nchi nyingine??
 
Back
Top Bottom