Tairi gani za kichina zina afadhali?

Tairi gani za kichina zina afadhali?

Inategemea na mtu ba mtu kuna wangapi humu nimewauzia na hajaleta malalamiko?
Sawa nataka Brigdestone 215/55R16 mpya kabisa sio used, ikikosekana hiyo Dunlop ya Japan, Sanamu la michelin nimelitafuta halipatikani hata superdol hawana
 
Used zimeruhusiwa lini Bongo? Hizo ni used za hapa hapa kuna watu wanavua tairi kutoka magari yaliyoingia kutoka Japan wanavisha mpya. Juzi nimevua dunlop zilizokuja na gari baada ya kuzitimba mieze 6 na nimeziuza kwa muuza matairi used!

Jamaa anasema zinatoka Dubai ,possible wanaozibadili kwa hapa hapa bongo.
 
Used zimeruhusiwa lini Bongo? Hizo ni used za hapa hapa kuna watu wanavua tairi kutoka magari yaliyoingia kutoka Japan wanavisha mpya. Juzi nimevua dunlop zilizokuja na gari baada ya kuzitimba mieze 6 na nimeziuza kwa muuza matairi used!
😀😀😀 Na mie najua hivyo, mie mwenye huwa nikiendaga badirisha tyre sikosi hela ya maji.. huwa wanakuja wanawauzia wengine
 
Usiogope zitumie tu ni nzuri.
Hapana mkuu. Hizo zinafaa matumizi ya hapa hapa mjini si kwa mtu anaepiga masafa mikoani. Mfano zangu zilizokuja na gari nimetumia miezi 6 ukiziangalia kashata imejaa ila kuna siku nimeikuta ina pacha ule mkujo wa pancha kuangalia tairi ina cracks kibao! ikijaa cracks hazionekani.
 
Tyre ya mchina yenye akili ni Triangle tu! Nje ya hapo kwangu naona ni upuuzi tu hata ile Goodride ambayo nilidhani ina nafuu imentesa kupiga jeki kila saa na kutoa vijipu pembeni
Majuzi nusura inimwage kwenye ile lami ya Chalinze-Moro baada ya ubena Zomozi Hapo nimefunga mpya imepasuka usiku mnene porini
 
Ni kampuni gani ya tairi za china ambayo ni nzuri kuzidi nyingine za china, nimeulizia BF GOODRICH y usa/uk Rim 15,ni sh 280,000/=kwa pisi moja, michelin 180,000/, goodyear 170,000/=, mchina 120,000/=hizo zote ni saizi 15, mchina ni maji usipo kunywa utaoga tu, hata kufulia basi.
Tairi za kawaida nazotumia kwa miaka yote ni Goodride.....hazijawahi nisumbua na naenda safari ndefu mara kwa mara. Tairi nyingine za kawaida nazotumia pia ni "Infinity", hizi tairi niliweka 2016 na mpk leo nazitumia..anaejua zinapopatikana anijuze maana kuna wakati niliulizia sikuzipata huku mikoani. Sijawahi kutumia tairi za bei "mbaya" zaidi ya Dunlop iliyokuja na gari,nilitembelea mpk uzi zikatokeza,nikazivua na kufunga Infinity. Wakati wa kununua huwa nazingatia sana mwaka iliyotengenezwa na kununua kwa dealers. Cheers
 
Ni kampuni gani ya tairi za china ambayo ni nzuri kuzidi nyingine za china, nimeulizia BF GOODRICH y usa/uk Rim 15,ni sh 280,000/=kwa pisi moja, michelin 180,000/, goodyear 170,000/=, mchina 120,000/=hizo zote ni saizi 15, mchina ni maji usipo kunywa utaoga tu, hata kufulia basi.
Mie kwa uzoefu nimetumia Black Lion, Goodride na MPS. Nilikaa nazo zaidi ya miaka mitatu, na nilikua na trip kibao.
 
Back
Top Bottom