Taja JF member au members ambao una hamu kabla hujatangulia mbele za haki angalau uwe umewajua

Taja JF member au members ambao una hamu kabla hujatangulia mbele za haki angalau uwe umewajua

Naamini kabisa kwamba wote tuliopo humu jf tuna umuhimu wetu kwa namna moja au nyingine ila hata hivyo haiondoi ukweli kwamba kuna baadhi ya wenzetu humu ( members ) ambao michango yao na uwasilishwaji wake huwa na mvuto sana kiasi kwamba inafika muda mtu unakuwa una hamu sana siku itokee tu uweze kuonana nae au umuone mubashara kabisa ili roho yako isuuzike.

Hivyo leo nimeona siyo vibaya nikiwashirikisheni nanyi ili kwa pamoja tuweze kuwataja hao members au member ambaye labda unaombea usitangulie kwanza kwa Mwenyezi Mungu Mbinguni kabla bado hujaonana au hujakutana nae kwani labda unampenda kiuchangiaji wake humu na anakuvutia sana na kila mara hukosi kumfuatilia mabandiko yake au mada zake.

Kwa kuanzia tu mimi natamani sana siku moja niweze kuonana na hawa members wa jf wanaonivutia na kunifurahisha mno hasa kwa aina ya michango yao na hata uchangamfu wao wa kiuchangiaji:
  1. Maxence Melo
  2. Mike Mushi
  3. Asha Dii
  4. Bridger
  5. Active
  6. Reserved
  7. Silencer
Karibu na Wewe Mkuu uweze kutaja members wako unaowakubali sana hapa jf.
Kasie, shunie, miss natafuta & miss chaga
 
Kuna member maarufu sanaaaa hasa kule jukwaa la siasa ni mshikaji wangu sana ila nimegundua juzi tu ID yake tena kwa bahati mbaya...[emoji23][emoji23][emoji23] unavyojenga picha tulivyo ni tofauti na uhalisia.
 
Ha ha ha haaaa.. Yaani mimi hua naimagine nyinyi ni watu flani hivi matajiri sana wanufaika wa mfumo..sometimes nikiona(ga) VX V8 linanipita kimoyomoyo najisisemea usikute huyo ndo MOTOCHINI mwenyewe.
Hahaha Utakuja kumchukia mtu bure na kigari chake ndugu
 
Miss natafuta
Sky elcat
Faiza fox
Miss chaga
Shunie
Jovitha
Mkuu Mimi hapo kati ya hao uliowataja mmoja wao tunafahamiana through JF as a means of knowing each other. Asante mkuu ...uliyepo kwa orodha tajwa.
 
Back
Top Bottom