Kuna id inaitwa
mkwepu jr hahaha huyu simchukii. Naikubali sana hii id inavyojiendesha yaani ikiingia kwenye uzi yenyewe ni kumwaga like tu na haulizi.
Mfano wewe utasema paka ni mnyama anakupa like, means anakubaliana na wewe, kisha akitokea mwingine akisema paka ni mmea na huyo pia anampa like, kwamba sasa hiv kakubali paka ni mmea, akija mwingine akiwatukana nyinyi kua mnaongea utumbo, atampa like na huyo pia.
Sasa akitokea mwingine akamcrush huyu kwa kutukana wenzake na kumwambia aache watu wawe free, na huyo pia atampa like.
Hii id chiboko.