Taja Jina zuri Kwa mtoto

Heshima kwako Mkuu.
Kwanza nakupongeza kwa msimamo wako wa kizalendo wa kulinda tamaduni za kwetu.
Pamoja na kukupongeza nakuomba utuorodheshee majina ya kiafrika yenye kufaa kuwaita watoto wetu.
 
Kwahio mzee unataka kunishurutisha niombe radhi? Hahahahaa afu utawaambiaa mods sioo.....Kazaa yeye au mimi? au kasaidiana na mods kuzaa??...kuzaa mzae nyiee keroo mtupe sisi Hahahaa

Lengo langu si ovu Comrade. Ni katika kusahihishana tu na si kudhalilishana.

Hukutumia uungwana kumuita member mwenzio mpuuzi. Si Lugha nzuri katika Forums, ungetumia uungwana mbona sina tatizo Mkuu?.

Iishi "signature" yako Comrade. Utakuwa philosopher mkubwa sana.

Kumradhi.
 
Heshima kwako Mkuu.
Kwanza nakupongeza kwa msimamo wako wa kizalendo wa kulinda tamaduni za kwetu.
Pamoja na kukupongeza nakuomba utuorodheshee majina ya kiafrika yenye kufaa kuwaita watoto wetu.
Mimi ni Mtanzania Comrade.

Kukutajia majina sina weledi sana katika hilo. Ninachoweza kukushauri ni hili "Mpe mwanao jina la Taifa lako lenye tafsiri bora". Usimpe mwanao jina la kukopa. Ni udunya na upeo mdogo wa uelewa wa mambo.

Majina ya Kiswahili kama Busara, Akili, Hekima, Faraja, Fanaka, Nuru, Tumaini, Baraka, Shangwe, Mzalendo, Bora, Huruma, Waridi, Furaha na kadhalika ni baadhi tu. Ni majina yenye maana nzuri na yenye kuonyesha uzalendo kwa Taifa lako kupitia majina.

Hekima ni Uhuru.
 
Ita mwanao jina la kiafrika Ashanti,Menelik,etc kuwapa watoto majina ya kiarabu na kizungu ni kuendeleza utumwa wa kifikra na kitamaduni.kwangu mimi Palamagamba ni bora zaidi kuliko Smith/Rob/Jackson/Whitney etc
 
We waitwa nani kwa jina la kibantu ( kiswahili??)
 
Kwahio mzee unataka kunishurutisha niombe radhi? Hahahahaa afu utawaambiaa mods sioo.....Kazaa yeye au mimi? au kasaidiana na mods kuzaa??...kuzaa mzae nyiee keroo mtupe sisi Hahahaa
Kwa nini upo JF? Itendee haki Jf.
 
Busara ( wisdom) Akili ( Brain) Wema ( goodheart) Furaha ( happyness) Majina yanatafsirika kwa kila kabila.
 
We waitwa nani kwa jina la kibantu ( kiswahili??)
Heshima Comrade.

Ukisoma The Federalist Papers na kujua kwanini Publilius, Mark Twain, Voltaire, George Orwel, waliitwa hivyo kamwe usingejisumbua kujua jina langu halisi. Kimantiki, haitokusaidia lolote.

Kumradhi.
 
sawaa mkuu kumbe hukuwa na nia mbayaa sorry kwako na kwake pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…