Taja kipaji chochote unachokiona kwa mwana JF mwenzako

Taja kipaji chochote unachokiona kwa mwana JF mwenzako

Danvers / Da'vinci. There is something about his works that I'm absolutely fascinated with.

I'd say he has such an amazing talent for describing things so you can see them perfectly in your mind. Take a quick glance at his posting history and you'll see.
Surely, He z smart
 
Huyo Kasie ana maneno ya mahaba sana na Mtundu mtundu hazeeki...anapandisha sana nyg

Ila hapo kuna mmoja umemtaja ni kichaa kabisa, yaani ana ule utahira wa kupanda na kushuka
 
Danvers / Da'vinci. There is something about his works that I'm absolutely fascinated with.

I'd say he has such an amazing talent for describing things so you can see them perfectly in your mind. Take a quick glance at his posting history and you'll see.
You are obsoletely correct, Da vinci namkubali sana sana .Hawa watu ningekuwa na pesa ningewakusanya wote tukafanya kitu kikubwa.
 
Hapa jukwaani pamesheheni vijapi vya kila aina na vya kila namna. Kuna vipaji hai na vipo mfu. Kuna vipaji ambavyo vinatuburudisha, na vipo vipaji vinatuelimisha.

Kuna vipaji vinatuonya na kutuadilisha, na pia kuna vipaji vinavyoyaelezea vyema maisha yetu ya usoni ambayo hatujayaishi bado na hatujayafikia.

Huu ni uzi wa kutambua jambo kwa ufupi tu, vipaji tunavyovionesha kupitia maandishi yetu. Karibu na wewe utie nyama kwenye uzi huu. Asante.

  • Mshana Jr ni visionary, ndiye nabii wa jamvi letu. Jicho lake kali linaona miaka kumi elfu nyuma, na miaka mia elfu ijayo. Iwe kwenye siasa, uchumi, utamaduni, matibabu, elimu ya mzungu na elimu ya rohoni amesheni uoni angavu usio na mawaa yoyote.
  • Bill Lugano, huyu ni jamaa mmoja mweledi sana. Nasema mweledi sababu nimekaa naye na ni mtu wangu wa karibu sana. Kijana mpole, mtaratibu, mcheshi, muungwana na ana elimu ya juu sana. Jamaa ana kipaji kikubwa sana cha kusimulia jinsi gani baba yake anavyokasirishwa na Laissez-faire, tabia aliyo nayo kijana wake.
  • Pia anaelezea utajiri wake kwa tambo za kipekee huku akituvunja mbavu kwa bichekesho na akituhurumia. Jamaa ni mwandishi mzuri sana wa riwaya na tenzi za Kingereza (poems) wengi hukasirishwa na aina yake ya uandishi kupitia characters wake Kidukulilo na Bill Lugano.
  • Pascal Mayalla, huyu ni Nabii mzee. Jamaa ameandika makala nyingi sana zenye maslahi kwa taifa, jamaa ni mwandishi mbobezi, aliyepitia misukosuko mingi ikiwemo kuhojiwa na kamati ya maadili ya bunge. Paskali, pia ni mwanasheria na ni kichwa kwelikweli, kwani katika wanafunzi 633, yeye ni miongoni mwa wanafunzi 26 tu waliofaulu.
  • UMUGHAKA, huyu jamaa ni bonge ya story teller, aina yake ya usimuliaji umejaa msisimko usio elezeka, muda wote unatamani kusoma maandishi yake huku ukitokwa na vipele vya msisimko. Maandishi yake yanayosha kabisa kumfanya mama aende nayo Ulaya akatuletea msaada wa matrilioni usio na.masharti yoyote.
  • GENTAMYCINE, huyu jamaa ni wa kipekee. Ndiye anayeongoza kwa kufahamika na mods wote na members wote hapa jukwaani. Jamaa ana akili za kurithi ambazo pia ameziongezea na elimu ya darasani na ya mtaani. Huyu akitoa ushauri hapa jukwaani, wizara zinaufanyia kazi ushauri wake, je ni nani mwingine kama yeye?
  • DeepPond , ukiyataka masimulizi ya mahaba hapa ndio mahali pake. Hii mashine haina mfanowe kwenye hiyo sekta aisee, simulizi zake lazima zikuache mdomo wazi. Hebu fikiria, mchepuko wa rafiki yako umemtia rumande mke wa rafiki yako, unafanyeje hapo?
  • FaizaFoxy , huyu mtu mmoja anaweza kufanya ligi na watu laki moja na akawaburuza. Sio uwongo, FaizaFoxy ni kichwa balaa, mpeleke kwenye dini, siasa, sayansi na teknolojia, kote yuko vizuri sana, hapendi ujinga, wee hata ukosee herufi moja tu, kwa jicho la tai ataona makosa yako.
  • ROBERT HERIEL, mwalimu wa walimu, kuhani mweusi. Atakufundisha kama mwalimu na kukuadilisha kama kasisi. Kupitia makala zake tumekuwa tukiyaona mapungufu yetu, na tulipoweza kujikosoa tukajikosoa, tulipowe kujisamehe tukajisamehe na tulipoweza kujirekebisha tukajirekebisha.
  • Kasie, hili toto chotara la Kimanyema na Kinyamwezi limebarikiwa maneno matamu, akili za darasani na za kitandani. Je una matatizo ya kimahusiano? Maneno yake matatu tu hayatakufariji kabisa, bali yataleta suluhusho la kudumu kwenye mahusiano yako. Je biashara yako haiendi vizuri? Kila unachokishika kinapotea? Umeenda kwa waganga wa kila aina na kwa Mwamposa lakini hujapata jibu? Hebu mcheki Kasie, hutojuta. Je una hela nanhuvijui viwanja classic vyenye watoto wakali na decent? Basi yeye ndio Google Map yetu.
  • figganigga, ana machapisho mengi sana. Habari za kimataifa na kimataifa, updates na breaking news, huyu ndiye Guru hapa jamvini.
  • Asprin, yeye sasa ndio babu wa jamvi na mkewe Sky Eclat. Wanasema kijiji kisicho na wazee kimelaanika. Hawa ndio wazee konki wanaozalisha baraka la jamvi hili.
  • Spartacus boy Wewe ni bonge la entertainer. Mambo ya ngoma kali, ujanja wa club, wewe ndio baba lao, no one like you kwenye hiyo field, au wewe unajionaje Spartacus boy ?
Ukweli wa mambo kila binadamu Allah kamjalia na kipaji chake ikiwa kinaonekana au hakionekani ,Bujibuji tena usije kumdharau bin adamu wa aina yyote hata yule chizi anaekota makopo ujue ana kipaji chake kwa hivyo haina maana kama jina lako halijaandikwa ukajiona wewe huna maana Binadamu sote hatuko sawa .
 
Back
Top Bottom