Taja kipaji chochote unachokiona kwa mwana JF mwenzako

Taja kipaji chochote unachokiona kwa mwana JF mwenzako

Yes.
Isingekuwa hivo majambazi, malaya, mafisadi nao tungeita wana vipaji

Kuna kipaji na kazi.
Kazi LAZIMA iwe productive lakini kipaji sio lazima.
Ingawaje kipaji wakati mwingine huwa kazi.
Ila wengine vipaji huweza kuvitumia kama hobby tuu yaani hata isipozalisha Kwa watu lakini Kwa Mhusika inamzalishia furaha.

Mfano, kuna watu wanakipaji cha kuimba na wanaimba lakini sio Productive kifedha Ila wanaburudisha watu makanisani.
Wakati huohuo kuna waimbaji wenye vipaji wamejiajiri au kuajiriwa kupitia kipaji cha kuimba na kujipatia Fedha.
 
Kuna kipaji na kazi.
Kazi LAZIMA iwe productive lakini kipaji sio lazima.
Ingawaje kipaji wakati mwingine huwa kazi.
Ila wengine vipaji huweza kuvitumia kama hobby tuu yaani hata isipozalisha Kwa watu lakini Kwa Mhusika inamzalishia furaha.

Mfano, kuna watu wanakipaji cha kuimba na wanaimba lakini sio Productive kifedha Ila wanaburudisha watu makanisani.
Wakati huohuo kuna waimbaji wenye vipaji wamejiajiri au kuajiriwa kupitia kipaji cha kuimba na kujipatia Fedha.
Kipaji lazima kiwe productive au kiwe na potential ya kuproduce, ila mtu anaweza kuwa nacho na asikitumie kuzalisha.
Mfano mzuri ni wako huo huo, mtu anaeweza kuimba ana kipaji, lakini hata kama hajaamua kukitumia kutafuta hela, haimaanishi akiamua kukitumia kupata hela anakosa.

Mfano mwingine, mtu anaweza kuwa na kipaji cha mpira ila hajapata chance ya kukitumia kupata hela.
Vipaji vyote lazima viwe na potential ya kuzalisha.

Sio eti mtu anaweza kutukana matusi makubwa makubwa ndio ukaita kipaji.

Kuchekesha zamani haikuwa kipaji, ila walipoanza kupata hela comedians ikawa career inayoeleweka. ndio hapo kuchekesha ikawa kipaji.
 
Hapa jukwaani pamesheheni vijapi vya kila aina na vya kila namna. Kuna vipaji hai na vipo mfu.
Kuna vipaji ambavyo vinatuburudisha, na vipo vipaji vinatuelimisha. Kuna vipaji vinatuonya na kutuadilisha, na pia kuna vipaji vinavyoyaelezea vyema maisha yetu ya usoni ambayo hayujayaishi bado nanhatujayafikia.
Huu ni uzi wa kutambua jambo kwa ufupi tu, vipaji tunavyovionesha kupitia maandishi yetu. Karibu na wewe utie nyama kwenye uzi huu. Asanye.

  • Mshana Jr ni visionary, ndiye nabii wa jamvi letu. Jicho lake kali linaona miaka kumi elfu nyuma, na miaka mia elfu ijayo. Iwe kwenye siasa, uchumi, utamaduni, matibabu, elimu ya mzungu na elimu ya rohoni amesheni uoni angavu usio na mawaa yoyote.
  • Bill Lugano, huyu ni jamaa mmoja mweledi sana. Nasema mweledi sababu nimekaa naye na ni mtu wangu wa karibu sana. Kijana mpole, mtaratibu, mcheshi, muungwana na ana elimu ya juu sana. Jamaa ana kipaji kikubwa sana cha kusimulia jinsi gani baba yake anavyokasirishwa na Laissez-faire, tabia aliyo nayo kijana wake.
  • Pia anaelezea utajiri wake kwa tambo za kipekee huku akituvunja mbavu kwa bichekesho na akituhurumia. Jamaa ni mwandishi mzuri sana wa riwaya na tenzi za Kingereza (poems) wengi hukasirishwa na aina yake ya uandishi kupitia characters wake Kidukulilo na Bill Lugano.
  • Pascal Mayalla, huyu ni Nabii mzee. Jamaa ameandika makala nyingi sana zenye maslahi kwa taifa, jamaa ni mwandishi mbobezi, aliyepitia misukosuko mingi ikiwemo kuhojiwa na kamati ya maadili ya bunge. Paskali, pia ni mwanasheria na ni kichwa kwelikweli, kwani katika wanafunzi 633, yeye ni miongoni mwa wanafunzi 26 tu waliofaulu.
  • UMUGHAKA, huyu jamaa ni bonge ya story teller, aina yake ya usimuliaji umejaa msisimko usio elezeka, muda wote unatamani kusoma maandishi yake huku ukitokwa na vipele vya msisimko. Maandishi yake yanayosha kabisa kumfanya mama aende nayo Ulaya akatuletea msaada wa matrilioni usio na.masharti yoyote.
  • GENTAMYCINE, huyu jamaa ni wa kipekee. Ndiye anayeongoza kwa kufahamika na mods wote na members wote hapa jukwaani. Jamaa ana akili za kurithi ambazo pia ameziongezea na elimu ya darasani na ya mtaani. Huyu akitoa ushauri hapa jukwaani, wizara zinaufanyia kazi ushauri wake, je ni nani mwingine kama yeye?
  • DeepPond , ukiyataka masimulizi ya mahaba hapa ndio mahali pake. Hii mashine haina mfanowe kwenye hiyo sekta aisee, simulizi zake lazima zikuache mdomo wazi. Hebu fikiria, mchepuko wa rafiki yako umemtia rumande mke wa rafiki yako, unafanyeje hapo?
  • FaizaFoxy , huyu mtu mmoja anaweza kufanya ligi na watu laki moja na akawaburuza. Sio uwongo, FaizaFoxy ni kichwa balaa, mpeleke kwenye dini, siasa, sayansi na teknolojia, kote yuko vizuri sana, hapendi ujinga, wee hata ukosee herufi moja tu, kwa jicho la tai ataona makosa yako.
  • ROBERT HERIEL, mwalimu wa walimu, kuhani mweusi. Atakufundisha kama mwalimu na kukuadilisha kama kasisi. Kupitia makala zake tumekuwa tukiyaona mapungufu yetu, na tulipoweza kujikosoa tukajikosoa, tulipowe kujisamehe tukajisamehe na tulipoweza kujirekebisha tukajirekebisha
Kwahiyo mimi babu sukari ya warembo kupitia mafao ya kustaafu hujaniona?
 
Kwanza kwa jina lako la Bujibuji nakuona kama mwalimu flani wa stadi za kazi. Mbali na ivyo mnoko mnoko tu hata nyumbani ukitoka unaficha remote watoto wako hutaki waangalie TV usipokuwepo nyumbani na ukirudi hata kama unaenda kuoga hutaki wabadilishe station 😬😬
Na sasa ni marufuku kutazama maigizo ya tamthilia
 
Kuna wenye vipaji vya kujibadilisha jinsia wao niwanaume ila nyuma yapazia wanajiita majina yakike sielewagi wanatakaga kitugani
 
Back
Top Bottom