Taja misemo ya wahenga isiyo na tija

Taja misemo ya wahenga isiyo na tija

Kuchamba kwingi, kuondoka na mavi. hapa wahenga sijui waliwaza nini jamani
 
Pambana na hali yako

sent from my Nokia kidole juu (mshindi) using jamiiforums Mobile app
 
Haraka haraka haina Baraka
Ina maana hata ukiunguliwa nyumba, usijenge nyingine haraka!!!
 
mzigo mzito mpe mnyamwez... Nafikir zigo kama msamb..wanda
 
Kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake...Mimi nakataa, atakula kwa huruma ya mchungaji...
Huu msemo humanishi mbuzi mbuzi tu aluyekwenye hali yoyote,

Anaongelewa mbuzi aliyefungwa kamba shingoni kisha kamba ikafungwa kwenye kisiki, sasa hapo mbuzi atakula majani kwenye ukubwa wa eneo kuendana na urefu wa kamba aliyofungiwa nayo kama ni refu eneo kubwa atalila, sio mbuzi tu hata ng'ombe au punda
 
Aliyeko juu mngojee chini ....
MIMI nakupandia huko huko juuu.....

Ova
 
Kisicho riziki,hakiliki.
Je wewe sio riziki au hauliki?
Ukisema wewe,sio riziki,mhhh,ni hatari!!!!kumbe mtoto sio riziki wewe!!!
Ukisema hauliki,maana wewe sio riziki(shoga).Ukisema unalika,hii nayo ni hatar!!!Unalika??
"mtoto sio riziki" imemaanisha mtoto hasara aitha mtoto amefariki katika harakati za mama kujifungua.

Au mtoto wa kiume amekua shoga, anakua sio riziki sababu shoga haoi mwanamke akazaa nae akaitwa Baba au ni kama mfu sababu hakuna mwenye furaha nae kwenye familia kutokana na tabia yake hiyo
 
Huu msemo humanishi mbuzi mbuzi tu aluyekwenye hali yoyote,

Anaongelewa mbuzi aliyefungwa kamba shingoni kisha kamba ikafungwa kwenye kisiki, sasa hapo mbuzi atakula majani kwenye ukubwa wa eneo kuendana na urefu wa kamba aliyofungiwa nayo kama ni refu eneo kubwa atalila, sio mbuzi tu hata ng'ombe au punda
sawa lakini bila huruma ya mchungaji huyo mbuzi atakaa sana
 
mzigo mzito mpe mnyamwez... Nafikir zigo kama msamb..wanda
Huu msemo unaakisi biashara ya utumwa, wanyamwezi kutoka tabora walikua wakibebeshwa pembe za ndovu na waarabu kutoka huko mpaka bagamoyo/zanzibar kwa mguu.
 
Back
Top Bottom