Taja mkoa ambao hujawahi kufika na Wala huna mpango kabisa wa kuitembelea

Tanzania nimepita mikoa yote, mkoa ambao sitarajii kwenda ni mkoa wa Zanzibar, sipendi kupita kwenye maji. Hela bombardier sina
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nyie wachagua mikoa ndo wavivu na waoga kimaisha maisha popote kila mkoa una fursa zakee

Kuna watu wako Manyovu karibu na Bujumbura ila wana good life kuliko weye unaeleta mashauzi hapaa
 
Hivi unaishije Tanzania kisha unasema wewe ni Mtanzania wakati hujafika Da'slaam?
Sasa kama wanaume wa Dar mnakimbia Panya road, vitoto hata harufu ya maziwa haijatoka vinawalaza saa 9 mchana... Utanishawishi vipi nije dar
 
Dar
Naogopa nisije nikawa napenda kula chipsi viepe na ushalawadu
 
hiyo mbusi katoliki ipo sana bwana ila sio mtaani kama huko bara, kuna hotel ukienda unapata safi kabisa.

jaribu kwenda siku moja...hautajutia.
hahahahahah nilihofia kuikosa bhana ... kwa ukiri wako huu nitajaribu kwenda huko hii december nije nitoe mrejesho
 
Sijawahi kufika Kigoma, Rukwa, Ruvuma, Lindi na Mtwara ila nikipata nafasi nitafika nijionee maisha ya huko.

Wenyeji wa mikoa hiyo mnaweza mkatualika sio mbaya tukipata kampani.
 
Mkuu nakuja jumapili nichukue Mashamba hapo kakese, au igaka, naomba ikiwezekana tuonane tupeane mawazo tofauti kuhusu kilimo cha mpunga huko Kama ni mdau Wa kilimo lakini.
Mkuu me ni mdau wa kilimo sana tu,,,,,,,,,,ila sipo huko kwa sasa nipo mkoa mwingine nasaka maisha hahahaaah.
 
Nilipita njia ya mbugani kupitia liyamba liyamfipa na pia kuzunguka mbuga kupitia Maji Moto kwa Pinda kule...
Mara ya mwisho nilienda 2012 lami ya mpanda starike/stalike ndio inaanza kujengwa.... Nihabarishe maendeleo ya sasa mkuu...
Sasa hivi kupo vizuri, njia ambayo sio nzuri ni ya kupita Tabora tu. Ila ya kupita Lyamba Lya Mfipa ipo vizuri sana, yote ina lami isipokuwa mbugani tu.
 
Sasa hivi kupo vizuri, njia ambayo sio nzuri ni ya kupita Tabora tu. Ila ya kupita Lyamba Lya Mfipa ipo vizuri sana, yote ina lami isipokuwa mbugani tu.
Thanks mkuu, I will be back nikipata wasaa.. Ila mbugani kama kawa lazima gari ipigwe dawa kukimbiza mbung'o...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…