Mr Sir1
JF-Expert Member
- Sep 23, 2018
- 1,749
- 7,945
Najim jamaa hakuwahi kuwa ndugu yangu wala rafiki lakini alinisaidia bila hata ya kunijua zaidi ya kuonana tu eneo moja kila siku.
Kipindi ambacho nilikuwa ugenini na wale waliopaswa kuwa marafiki na ndugu wote walinitosa kama hawanijui.
Najim alikuwa anazuga kunialika kwake na mkewe mida ya chakula kuzuga tupige story kumbe alijua hata mlo wangu ulikuwa wa tabu.
Nilipokosa pa kukaa Najim alikwenda kulipia store na kuibadilisha kuwa chumba na kuniambia kuwa ana chumba hakitumii nijishikilize mpaka nikikaa sawa.
Jamaa akanifundisha mbinu za biashara yake na mwisho kunifanya partner kwenye biashara kiasi cha kugawana faida nusu kwa nusu bila ya kuchangia hata shilingi.
Ila ndio vile chema hakidumu. Ila usihofu bro, sikuwahi kwenda kinyume na ahadi yangu kwako. Binti yako mkubwa nimemuozesha mwaka jana. Nilisimama kama baba. Na ambayo hakuwahi kutimiza lakini ulitaka yatimie nakuhalkikishia yametimia na ziada juu.
Sijalipa hata robo ya fadhila zako kwangu ila sitoacha kukuombea daima Allah akupe pepo ya daraja la juu kabisa.