Ilikuwa siku ya juma 5 ya mwezi wa 3 mwaka 2018, asubuhi mapema najiandaa kwenda mishe mara simu inaita..
Ssuti upande wa pili: (Bila salamu),njoo kwa bro wako hapa Temeke fasta Kuna tatizo.(Simu ikakata Bila Mimi kujibu chochote).
Ilenimeshatoka home Huku nimepagawa naelekea uelekeo wa kwa bro,njiani nakutana na mtu ninayemjua. Kabla ya salamu jamaa ananiambia pole sana Satoh hirosh,Mimi naelekea kazini kuomba ruhusa kisha tutakuwa pamoja. Dah ile siku ilibaki kidogo nizimie mana mpaka hapo sijajua nini kimetokea ingawa hisia za kifo zilishaniingia. Mdomo mzito unaogopa kumuuliza jamaa,Kuna nini kwa kaka?
Nafika home kwa bradha napokelewa na vilio vya wanawake uani. Shemeji yangu ananiona akaongeza kulia na kuniambia kwa sauti ya uchungu "kakaako hatunae Tena nitaishi vipi Mimi na huyu mtoto mdogo pekeyangu shemeji"
Ile siku nililia kama mwanamke. Imekuwaje kaka amefariki ghafla wakati Jana usiku niliongea nae kwenye simu.
Wazee wakaniita waniambie kilichotokea.
"Kijana jikaze maana wewe ndiye unategemewa sasa hivi kuongoza shughuli ya msiba na kupokea wageni wa mikoani.
Kilichotokea ni kuwa;
Jana jioni kakaako alitembelewa na rafiki yake mkubwa ambaye ni askari pale ukonga. Leo asubuhi akamcheki bodaboda wake (bro alikuwa ana pikipiki akamkabidhi jamaa aendeshe kisha amletee pesa kwa wiki,yeye ana mishe zake zingine). So kwa heshima ya rafiki yake,ile Jana yake jioni akamcheki jamaa wa pikipiki aje kuilaza home(kwa bro) ili asubuhi bro mwenyewe awahi kumpeleka mshikaji wake kazini ukonga kisha akirudi anarudisha pikipiki kwa boda wake na yeye kuendelea na mambo yake.
Asubuhi ya umauti,wakajiandaa vizuri na safari ikaanza hadi ukonga. Wakati anarudi home .. Daah!!
Dereva wa Fuso akitokea kisarawe akamgonga Bradha kwa nyuma na kumrusha service road kifo kikamkuta hapo hapo na kisha gari ikaiburuza pikipiki mita kadhaa. Konda wa Fuso ndiyo alimstua dereva.
"Oya umemgonga mtu wa pikipiki mwanangu alafu pikipiki ipo chini ya gari unaiburuza"
kumbe dereva alikuwa anaendesha gari Huku amelala( inaonekana alikesha usiku). Akastuka na kufunga breki...
Inaita uchungu kusimulia. Ila nakumbuka Mimi na yule askari mshikaji wake tulilia kama watoto mana kifo cha ghafla kinauma asee!!
REST IN PEACE KAKA,mwanao D ulimwacha darasa la 6 ule mwaka 2018,juzi TU hapo matokeo ya form 4 yametoka. Hajafanya vizuri sana kutokana na changamoto za kulelewa na single mama,Mimi nikiwa kama baba ila baba mdogo,ila nakuahidi nitajitahidi kadili ya uwezo wangu aende chuo.