Taji Apewe Mshindi wa Tatu


Ww ndio utakua huyo mshindi wa tatu
 
Endapo akipewa mshindi wa tatu lazima yataibuka maneno pia...Mimi naona wale top 5 washindanishwe tena ili tumpate mrembo halali...


Litakuwa jambo la ajabu sana. Kinachozuia mshindi wa pili asipewe ni kitu gani? Nahisi hili suala halina mjadala, Sitti akijivua/akivuliwa, automatically wa pili anachukua nafasi yake.
 
Mbona mbowe alipopiga picha anakula denda mbele ya wanawe mlisema ni mambo ya kawaida!!! Au kunya anye kuku, akinya bata kaharisha? Acheni double standard bana. Mkiamua kukosoa toeni kwanza mahaba na chuki zenu ndio mtakua mnaeleweka.
Punguza mahaba kijana yule bibi bomba alikuwa amevaa nguo za juu tu.
 
Hivi baba wa Kiafrika kupiga picha na binti yako akiwa kwenye mavazi haya hii ni adabu ya wapi?

Tena muislam anayejua maadili yote ya dini, huyu mtemvu ni sheeeeda, kazi yake kupeleka wadogo zetu uarabuni tu, simpendi huyu mzee basi tu
 
Kwa nini mshindi wa pili arukwe? Na huyo mshindi wa tatu wa kuitwa Jihan anapigiwa chapuo sana. Ipo namna....
 
Wasije kumliza tena Hoyce Temu kama alipopewa yule mdosi Richa Adhia

Bora yeye alipewa kwa utaratibu sasa kwa hili tukiruka tarakimu itakuwa sio fair na lazima uibuke mzozo mwingine tena.
 
Sorry wanaJF.
Ninaomba mrejee kwenye mada nimefanya masahihisho.
Kuna makosa yaliyofanywa na baadhi ya blogs kuwa Lilian Kamazima ni mshindi wa tatu.
Nilimlenga Lilian kuwa anastahili kuwa miss Tz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…