johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Tajiri wa kirusi Roman Abromavich anayemiliki club ya Chelsea ya England ameikabidhi timu hiyo kwa Bodi ya wadhamini kufuatia vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa nchi yake.
Source: BBC
----
Mmiliki wa Chelsea FC, Roman Abramovich ametangaza kujiweka kando na majukumu ya uongozi ndani ya klabu hiyo kisha kukabidhi kwa Bodi ya Wadhamini ambapo yeye ataendelea kubaki katika nafasi ya umiliki.
Kujiweka kwake kando kuna maanisha licha ya kuwa ni mmiliki lakini hatakuwa na maamuzi ya kila siku katika utendaji wa klabu hiyo badala yake amekabidhi majukumu hayo kwa uongozi wa bodi chini ya Marina Granovskaia na Bruce Buck.
Maamuzi hayo yanakuja kutoka na presha kuwa kubwa kwa baadhi ya wanasiasa wa Uingereza ambao wanashutumu ukaribu wake na Rais wa Urusi, Vladimir Putin ambaye aliagiza majeshi yake kuanza kuishambulia Ukraine, hivi karibuni.
Taarifa rasmi ya Chelsea iliyotolewa kuhusu tamko rasmi la Abramovich inaeleza hivi:
“Katika miaka yangu 20 ya kuimiliki Chelsea FC, nimekuwa nikijiona ni sehemu ya tamaduni ya klabu hii, lengo lilikuwa kuwa na mafanikio makubwa kama ilivyo leo, na kuisaidia jamii.
“Nimefanya maamuzi mengi kwa faida ya klabu, ninaendelea kuwa na nia ileile. Ndiyo maana leo nimeamua kukabidhi mjukumu yangu kwa Bodi ya Wadhamini wa Chelsea.
“Naamini kuwa wao kwa sasa ndiyo wenye nafasi nzuri ya kuendesha klabu kwa faida ya klabu, wachezaji, wafanyakazi na mashabiki.”