Hapana huyu Yeye ndiye mwenye yale ' Malori ' makubwa ya kusafirisha ' Mafuta ' Congo DR, Rwanda, Burundi, Zambia na Malawi yenye ' Nembo ' kubwa ya ZHP lakini pia ana ' Biashara ' zake nyingi zingine ndani na nje ya nchi. Pia ndiye mwenye Bar moja nzuri sana na ' tulivu ' ipo maeneo ya ' Avocado ' mtaa wa nyuma na ilipo Bar ya Tripple 7.
Ameingia katika Biashara baada ya kuamua kuachana na JWTZ ( Jeshi la Wananchi wa Tanzania ) ambapo ameachana na Jeshi miaka ya mwishoni ya 80 akiwa na ' Cheo ' chake Kikubwa tu cha ' Captain '. Ni Mtu mmoja makini tena kutokea katika Kabila la Watu wenye maamuzi ya mwisho la ' Kihehe ' kutoka Mkoani Iringa na hapendi ' masihara ' ya ' Kijinga Kijinga '.
Binafsi nashukuru amerudi ' Kundini ' kwani nina uhakika bila yeye kurudi basi mechi yetu ya Jumamosi ya kumaliza Ligi dhidi ya Mwadui FC najua Simba SC tungefungwa tutake tusitake lakini hata mechi yetu ya fainali ya ASFC dhidi ya Mbao FC nayo pia tungefungwa kwa sababu zangu Kuu tatu ambazo nikijisikia kuzielezea baadae humu nitafanya hivyo.
Ni imani yangu kubwa kuwa juhudi hizo hizo za Kiungwana na Kibusara ambazo zimeweza kumrejesha Klabuni ' Tajiri ' Hanspoppe basi zitatumika pia kuweza kumrejesha na Kubwa la Matajiri Tanzania nzima Mohammed Dewji ' MO ' ili ' Jahazi ' letu liende vyema kwani hakuna asiyejua kuwa Wanaoibeba Klabu ya Simba kwa nguvu zao kubwa na kwa kila kitu ni Zackaria Hanspoppe na Mohammed Dewji ' MO '.