Tajirika na Kilimo cha Nyoka: Tuwapende na kuwatumia Nyoka badala ya kuwaua

Tajirika na Kilimo cha Nyoka: Tuwapende na kuwatumia Nyoka badala ya kuwaua

Sipati picha banda likivunjika kwa upepo au mafuriko au msafishaji kusahau kufunga mlango
 
Bei ya sumu hutofautiana kulingana na nyoka.mfano

1.Gram ya puff adder venom ni $202

2.Boomslang bei yake ipo juu kuliko nyoka yeyote yule $4800

3.koboko $500

Hivyo bei ya venom hutofautiana na aina ya nyoka,sasa kazi ni wewe kupata license na kuchagua aina ya nyoka unaowahitaji au kuona watakuletea faida kubwa.

Aidha kuhusu namna ya kutoa sumu ,nyoka hukamatwa kwa ustadi kupitia kifaa special ,fimbo special yenye kibanio na pia nyingine iliyochepuka ambayo husaidia kumbana nyoka shingoni karibu na kichwa ,ukishamkamata nyoka kichwa hatua inayofuata ni kutafuta chombo special cha kuwekea sumu hiyo.mfano umechukua bakuli dogo,au chombo chochote kile unafunga plastic juu yake kama vile mfuniko huku ukiwa umemshika nyoka kichwa na wakati huo mdomo wa nyoka utakuwa wazi usiokuwa na madhara kwako wewe kisha unamuinamisha kwenye chombo husika na fangs za nyoka zitagonga au kuchoma plastic uliyoiweka juu na kumwaga sumu ndani,njia zipo nyingi tu

7fe9c3c06341be68dccedbc5f45c75cc.jpg


6e08da4c7e8100704275964a04cb6520.jpg


Soko ya venom ipo USA ,India ,China ,S.Africa

Lakini wengi hupeleka China sababu huko wengi ndio wanahitaji kwa wingi.

Unapeleka na ufuate utaratibu na sheria mfano December 2016 India waliwakamata smugglers 5 waliokuwa na venom yenye thamani ya $30Million ,walikuwa wanasafirisha kimagendo na walikuwa wanawauzia druglords ambao pia hutumia venom kutengenezea drugs


e5b5e46b4f1318fcd1d37e820a234026.jpg
Mijoka hii hii ambayo ikionekana tu tunakimbiana?

Haa, watu mna ujasiri aloo. O level nilimshikaga chatu nilikimbiwa balaa na watu waligoma hata kula nami.

Mijoka ina sura ka shetani ndo nifuge? Thubutuuu, bora nifuge hata vyura kuliko masneki
 
Lipo mbeya nashukuru Mungu mambo yanakwenda vizuri,nawashukuru watu wa Mali asili kwa ushirikiano na ushauri wanaonipatia

Una roho ngumu sana kiongozi!! Huyu mdudu anavyotisha yaani ukimtaja tu nywele zinasisimka!!!
 
Kabla hujaanza kuwafuga andika USIA na usisahau kwenda kuomba kibali serikali hii haikawii kusema ni nyara zake.
 
Hii ni zaidi ya Kilimo kwanza!Hii inaitwa Kifo Kwanza
 
mkuu, mazao yote haya ya kulima.. unawaza nyoka.. duuh hatarious..!
 
Mkuu undefine nikutakie tu kila la heri katika ufugaji huu, mimi nitahitaji muda mrefu wa kuandaliwa kisaikologia.
 
mkuu me nimepta interest y hki kilimo...naomba unambie soko la hio venom lko wap kw hpa bongo...na bei ikoje ili nijpnge october nianze kazi
 
Hahaa mnataka kufuga na nyoka acheni mchezo nyie fanyeni kilimo kingine

Hao nyoka unawazoeaje kwanza mmh ni issue
 
Siwezi kufuga nyoka wala kuwapenda. Hao ninapo muona ni adui kwangu.
 
Back
Top Bottom