Wana Jf hamjambo???
Hapa Msasani ni siku ya 5 leo taka zimetolewa na Gari halionekani.
Watu wametangaziwa kwamba watoe taka gari linapita jioni kubeba taka, mbaya ni kwamba mpaka Leo zipo na ni taka zenye harufu mbaya, vinyesi pads pampas yaani tafrani tu.
Mbaya ni kwamba hizi taka mnaziziona hapa ziko njiani, na hii njia magari yanapita, bajaji na pikipiki kwahiyo tangu ziwekwe yaani zinaleta foleni ambayo sio ya lazima hapa.
Halafu hapahapa Kuna watu wanapitia chakula, Sasa imagine taka ziko Karibu na sehemu ya kupikia Vyakula na manzi yamejazana mpaka sio poa, na haijulikani zitatolewa lini
Sasa hii imekuwa ni kawaida ya watu kupita wanatangaza toeni taka, na inaweza kupita mwezi taka zipo tu na hela tunalipa na gari haliji, hii sio sawa.
Mamlaka husika shughulikieni hili aisee, sasa ni kama Jiji la Dar hii imekuwa kawaida tu.