sifi leo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2012
- 5,182
- 8,948
Ndugu zangu Watanzania natumai hamjambo wote!
Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa niaba yangu na yenu mlio hai, wagonjwa na hata walio tangulia mbele ya haki usiku wa leo hata jana!
Ndugu zangu, mimi Sifi Leo tangu isomwe ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali mbele ya Rais nimeamua kila ifikapo saa kumi za usiku kuamka na kutafakari ripoti Ile kwa kina na kutazama kila siku nini kina julikana katika Taifa dhidi ya ripoti Ile.
Mengi yametokea baada ya ripoti;
Mosi, Mh. Rais amechukia hatua zake zikiwemo kuwataka Makatibu Wakuu wa Wizara zilizotajwa chini ya katibu Mkuu Kiongozi kila mmoja kuchukua hatua, yeye pia alivunja Bodi ya Shirika la Reli na mengine mengi. Mimi Sifi Leo sikukubaliana na hatua hiyo!
Rejea uzi wenye kichwa ccha habari "Sisi umoja wa wizi wa wastaafu wa kuku hatukubaliani na hatua ulizo chukua Mh. Rais." Baada ya hapo tukamwona Waziri mmoja kinara akisonsomola futari uliyoandaliwa na Shirika linalojiendesha kwa hasara!
Tukahoji kupitia uzi wenye kichwa cha habari "Shirika halijajibu ripoti ya mkaguzi kwani linajiendesha kwa hasara lakini limeandaa futari na kumnunulia Waziri Kanzu. Je fedha limepata wapi?"
Ndani ya uzi ule tumetafutwa na waliotutafuta tumewapa makavu ya kuwa Tanzania ni yetu sote sio yao peke yao. Hata watuue tutazikwa Tanzania, watuchome moto tutabakia Tanzania, kwa kifupi tumewaambia wajitafakari.
Baada ya hapo tunasikia Waziri Mkuu akiwa Bungeni ameelekeza ile mikopo ya 10% imesitishwa sijui kutoka lini mpaka lini mie sijui, mpaka waweke mfumo mzuri. Nataka niseme yale majizi yanayotafuna fedha hizo ndiyo yanayoenda kuulizwa mfumo gani mzuri uwekwe ili yakiiba Mkaguzi asiyagundue?
Wenye akili tunajua, ukitaka kujua ukweli nenda Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Mkurugenzi na Mkuu wa wilaya mwaka 2020-2021 kwa kushirikiana na Afisa Maendeleo (wote wameishaondoka baada ya kupiga mpunga), waliamua fedha zaidi ya milioni 300,000,000/= zipitie Saccos ya Umoja ambayo ipo Muleba. Yaliyojitokeza ni vituko, yalipelekwa majambaka kichota fedha zile ni aibu kuandika hapa.
'Ebooooo' ili nalo nimeamka nalo leo eti Spika wa Bunge anasema ripoti ile ya ukaguzi ijadiliwe November! Serous kabisa tunakubali upuuzi huu? Nauliza, kama Bunge haliwezi kujadili hoja nzito zilizoibuliwa na Mkaguzi kwa kipindi hiki, linajadili kitu gani muhimu kwa sasa zaidi ya wizi huu?
Kama Bunge haliwezi jadili ulawit kwa watoto wetu, wabunge wetu na wengine wengi na kutoa mwafaka, linajadiri nini?
Ninafahamu kiuzoefu ya kuwa, ripoti za Mkaguzi mara zote huwa ni mwiba kwa Bunge kwa sababu wanaotuhumiwa kuiba huko ni ndugu wa wabunge ndiomaana mnaanza kiwakingia kifua.
Lakini baya kuliko yote, muda unaotolewa unawapa nafasi wizi kujipanga kutafuta fedha za kuwaonga wabunge machachari kupitia kiti cha Spika ili kuziba majizi yasitajwe.
Katika ili najua hamtonielewa ila nasema ukweli, sasa ni wakati wa kuvuna kwa baadhi ya wabunge na kamati zao, watu wanaandaa murungura ili wasafishwe Ili mkaguzi aonekane alikurupuka.
Kwa andiko ilo nasisitiza TAKUKURU waichunguze Ofisi ya Spika.
Pili, wananchi tuulizwe nini kijadiliwe. Kuna uwezekano mkubwa sana wabunge wanafanya tusiyiyataka wawapo Bungeni kwa viburi vya kura zetu.
Nimalizie kwa kusema;
Tusiwe kama Pascal Mayalla anaemsifie Dkt. Tulia, Spika wa Bunge, tuchunguze kwa kina yawezekana mrungura ulimfikia.
Ni aibu Bunge lenye weledi kupitisha bajeti nyingine mwaka mwingine wa fedha ili hali fedha nyingi zimeibwa. Mtapitisha bajeti lakini hamtopata hizo fedha maana watu kama wa Dar wameishaanza kuambiwa wasilipe Kodi tena mpaka majizi yaliyoiba walizolipa mwaka wa fedha uliopita yamekamatwa.
Kwa hli naungana na Mh. Former Mayor wa ubungo, nami sitokaa nilipe.