TAKUKURU chunguzeni haraka madai ya uwepo wa rushwa kwa wabunge kuhongwa na Waziri Makamba

TAKUKURU chunguzeni haraka madai ya uwepo wa rushwa kwa wabunge kuhongwa na Waziri Makamba

KUNA TAARIFA ZINASAMBAA KWA KASI SANA ZINAZOMHUSISHA WAZIRI WA NISHATI, JANUARY MAKAMBA KUWAPA RUSHWA WABUNGE YA SHILINGI MILIONI 10 PAMOJA NA RUSHWA NYINGINE YA MAJIKO 300 YA GESI KWA KILA MBUNGE ILI KUMPITISHIA BAJETI YAKE ITAKAYOSOMWA WIKI HII.

MAWAZIRI WOTE WAMESOMA BAJETI ZAO HAWAJATOA RUSHWA YA AINA YOYOTE KWA WABUNGE ILI WAPITISHE BAJETI ZAO, KAMA WANANCHI TUNAOMBA TAKUKURU MSIPUUZE MADAI HAYA KWANI FEDHA ZINAZOTUMIKA KUHONGA WABUNGE NA KUNUNULIA MAJIKO YA GESI KUWAHONGA WABUNGE NI FEDHA ZETU WATANZANIA TUNAZOKATWA KODI KILA SIKU.

TUNAOMBA TAKUKURU SUALA HILI MSILIFUMBIE MACHO LIKO WAZI NA KILA MTANZANIA ANALIFUATILIA KWA KARIBU SANA KWANI KWENYE NCHI YETU HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA.
Endelea na majungu watu wako site
 
Ikiwa:

1. SANDUKU la kura limeshindwa kutenda HAKI.

2. TAKUKURUu imengolewa meno haingati!

3. Bunge limekuwa Rubber stamp.

4. Sirikali imeweka pamba masikioni,

Njia pekee iliyopo, tutapiga KURA ya WAZI viwanjani na mabarabarani,

Tusubiri.
 
Ridhiwane, January, nape, Fred lowasa na baadhi ya watoto wa wakubwa hua wanatuhumiwa mara nyingi Kwa vitu vya kuhisi tu, wanahukumiwa kutokana na trends na baadhi ya matukio yaliyofanywa na wazazi wao na pia wanahukumiwa kutokana na chuki zilizopandikizwa Kwa watu juu yao lkn hamna uhalisia wowote
 
kuna watu wadhadhani coincidence ni lazima usubiri ijitokelezee tuu, waona mbali wana coincidencesisha coincidence!.
P
Mkongwe wewe ni Mwasheria mtu anagawa pesa kwa wabunge na anatoa majiko 300 kila mbunge na kesho ndio bajeti yake unasema ni jambo la kawaida?
 
Mkongwe wewe ni Mwasheria mtu anagawa pesa kwa wabunge na anatoa majiko 300 kila mbunge na kesho ndio bajeti yake unasema ni jambo la kawaida?
Kawaida sana, ingekuwa hiyo gesi na hayo majiko ni ya January, hapo ungesema rushwa, lakini gesi na majiko ni ya Taifa Gas, January hajatumia hata senti tano kuyanunua, mwenye gesi anatoa bure as part of CSR yake, kuna ubaya kuicoincidenceisha na bajeti yake?. Hapo rushwa iko wapi?. Is there any threat bajeti ya nishati ikakwama ila kuhalalisha wabunge wanalainishwa?.

Kama ni CSR ya Kampuni ya TAIFA GAS ingetolewa kwenye Halmashauri husika ambapo wabunge nao ni sehemu ya madiwani wa halmashauri husika na Baraza la Madiwani ndio lingepanga yakatumike maeneo gani na kwa uwazi. sasa kumpa mbunge ni hongo. Hoja yako inakuwa dhaifu sana. Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom