Nimepata taarifa kutoka kwa madogo ninaowaamini kua pale wizara ya Afya wale watu wanaohusika kuwalipa wanafunzi waliopata ufadhili wa mama Samia kusoma nje ya nchi wanawalaghai wanafunzi hao.
Mchezo uko hivi, kwanza inaonekana toka wanafunzi hao wajiunge na masomo yao mwaka jana mpaka sasa hakuna aliyelipwa hata senti kwa kisingizio kua wanachakata taarifa na pesa hazijatoka, ndugu zangu mtajiuliza hawa wanafunzi wanaishije huko ughaibuni, ni miezi takribani 9 mpaka 10 sasa, na hili mimi nimelithibitisha pia hapa ninapoishi kwa kua kuna madogo tuliwasaidia kiasi fulani cha pesa mwaka jana toka ofisini walipokwama kwa makubaliano kuwa wakiwekewa pesa watarudisha, lakini kila tukiwauliza wanasema hawajalipwa mpaka sasa.
Sasa jana kuna mmoja kati ya wanafunzi hao alikuja ofisini kulalamika kua watu wanaoshughulikia malipo yao ya ufadhili licha ya kuwaahidi kua watawalipa malipo hayo kwa mkupuo yaani mwaka mzima wa masomo, sasa jana waliwaambia kua watawapa pesa za miezi nane tu na nyingine watawamalizia kwa muda ambao haukutajwa, huku kukiwa na fununu kua serikali imetoa pesa zote za mwaka mzima lakini wao wanajua namna wanavyotaka kuzifanya kitu ambacho si sawa.
Nikiwa kama mdau ambae wakati mwingine nahusika kuwapokea baadhi ya wanafunzi hao huku ugenini najiuliza hao watumishi wa umma wa wizara ya Afya kuwatesa hawa wanafunzi walioko ughaibuni kiasi hiki na kupelekea kuonekana kana kwamba hizo pesa wanazopewa ni hisani tu wakati ni haki yao, wanafaidika na nini?
Mmoja ambae ni mwenyeji kidogo anasema hata mwaka jana ilibidi wawasiliane na Waziri wa afya ili wawekewe pesa zao zote la sivyo ilikua inakula kwao, kuna mwingine anasema kuna baadhi ya wanafunzi wa mwaka juzi wanadai pesa zao toka wizarani mpaka leo bila mafanikio, kwa mtindo huo huo. Hivyo kuonekana ndiyo michezo yao.
Inanikumbusha kuna wakati nilifuatilia ziara ya waziri mkuu Kassim Majaliwa , alikuwa mkoa wa Mara nadhani, alikuta kuna watumishi wa Wizara wanashirikiana na mhasibu sijui afisa manunuzi kuiba pesa za wizara na kupitisha kwenye akaunti ya halmashauri nadhani ya serengeti then mhasibu hutoa pesa hizo na kuwapelekea mkononi wahusika hao wa wizara, imagine hao ni watu walioaminiwa na serikali, inasikitisha sana.
sasa ombi langu kwa vyombo vyetu vya kiuchunguzi hasa Takukuru makao makuu nimewapa lonja hiyo, fuatilieni, wataalamu mnaowaandaa huku ughaibuni wanashinda na kulala njaa, hatujui hata hayo masomo kama wakifundishwa wanaelewa, halafu ndiyo warudi kusaidia taifa kweli, sawa mmeshawacheleweshea pesa zao na mliwaahidi kuwalipa pesa za mwaka mzima, kwanini wasilipwe pesa zao zote, siamini kama serikali yetu kupitia wizara ya afya wanafahamu haya yanayoendelea. Kama hawaelewi Waziri Ummy na katibu mkuu fuatilieni tafadhali, Nahisi kuna kikundi cha baadhi ya watu pale wizarani hasa wanaohusika na malipo haya ndicho kinachocheza na akili za wataalamu hawa.
hakuna lenye mwanzo likakosa kua na mwisho, hawa watu wabadilike wakishindwa kubadilika wao basi wabadilishwe, naamini nchi yetu ina wataalamu wengi wazalendo wa kufanya kazi kama hizi kwa ufanisi mkubwa sana.
Naomba kuwasilisha.
Ahsanteni ndugu zangu