TAKUKURU haiwezi na haina mamlaka ya kubambikizia mtu kesi

TAKUKURU haiwezi na haina mamlaka ya kubambikizia mtu kesi

MdogoWenu

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2009
Posts
554
Reaction score
916
Tangu juzi mitandao na magazeti yamefurika taarifa kwamba TAKUKURU wamefuta kesi 147 walizobambikizia watu.

Watanzania wote tumekuwa kama vipofu bila kuchambua sheria ya TAKUKURU inasemaje kuhusu uwezekano au kutowezekana jambo hilo.

Ukiisoma sheria hiyo utaona kwamba PCCB haina kifungu cha kumpeleka mtu mahakamani.

Hata kama TAKUKURU wakihusika wao huishia kuchunguza uwezekano wa rushwa na kupeleka file kwa DPP.

Mfano ni kesi ya Kangi Lugola iliyoko TAKUKURU haiko mahakama yoyote nadhani ama file halijaenda kwa DPP au liko kwa DPP lakini hajalipeleka mahakamani.

Huu ni mfano mdogo wa jinsi TAKUKURU isivyoweza kubambikizia watu kedi wakajazana mahabusu. Hawana kifungu hicho.

Anayepeleka watu mahakamani ni DPP na siyo Takukuru.

Lakini hata usingeijua sheria hebu jiulize swali dogo kwamba je ni kesi gani au kesi ngapi za TAKUKURU ulishawahi kuzisijia mahakamani, bila kujali ni za kubambika au la.

Mimi sijawahi kusikia hata moja.

Jiulize swali jingine, hizo kesi 147 zilifunguliwa mahakama ipi?

Mimi sijawahi kusikia hata moja labda wewe na kama umedhasikia tujulishe tusiozijua.

Hivyo wengi wakiwemo waandishi wamelivamia hili suala bila kusoma sheria ya PCCB inasemaje.

Madhara ya bangi za usiku kuvutia chooni haya.

Kwa ufupi, kipindi cha utawala wa mwendazake "DPP, TAKUKURU, TRAFIC POLICE, WAKUU WA MIKOA/WILAYA, MGAMBO, MAHAKAMA, WANAJESHI, TCRA" zilikua ni branch za TRA kukusanya mapato kwa njia yoyote ile, iwe kudhulumu au kudanganya au kutapeli au kuiba au kubambikiza makosa kwa wananchi.

Hakuna sheria iliokua inafuatwa.
 
Kesi ndogo PCCB wanazipeleka mahakamani bila kupitia kwa DPP,kesi kubwa kubwa ndio wanazipeleka kwa DPP halafu DPP anazipeleka mahakamani.

Wanavyosema wanabambikia kwa sababu wao ndiyo wanachunguza,wanakamata na kupeleka mahakamani,kwa zile kubwa wanaochunguza halafu wanapeleka jalada kwa DPP.

Halafu kama hawajabambikizia watu kesi kwanini wamezifuta,pia jiulize mpaka Leo hawajapata ushahidi wa kina Ruge na Seth ,miaka zaidi ya 5 watu wapo mahabusu tu.
 
Madhara ya bangi za usiku kuvutia chooni haya.

Kwa ufupi, kipindi cha utawala wa mwendazake "DPP, TAKUKURU, TRAFIC POLICE, WAKUU WA MIKOA/WILAYA, MGAMBO, MAHAKAMA, WANAJESHI, TCRA" zilikua ni branch za TRA kukusanya mapato kwa njia yoyote ile, iwe kudhulumu au kudanganya au kutapeli au kuiba au kubambikiza kwa wananchi.

Hakuna sheria iliokua inafuatwa.
Hapo Umesema Kweli Ila Madame SSH
Anaujua Ukweli Kuwa PCCB Haina Tatizo Isipokuwa Yule Aliyekwenda
 
Afadhali wewe umeelewa mkuu. Jamaa zako hapo juu badala ya kunitajia hizo kesi walau moja wameshindwa.

Mpaka nimeleta hoja hii nimefanya research nikagundu wengi hawaielewi hii issue.

Haa😆😅😄😃😂😁😀
Ukitajiwa Tu Nitajua Kweli
Ila Tumepigwa Hakuna Mahakama Hata Moja
 
Tangu juzi mitandao na magazeti yamefurika taarifa kwamba TAKUKURU wamefuta kesi 147 walizobambikizia watu.

Watanzania wote tumekuwa kama vipofu bila kuchambua sheria ya TAKUKURU inasemaje kuhusu uwezekano au kutowezekana jambo hilo.

Ukiisoma sheria hiyo utaona kwamba PCCB haina kifungu cha kumpeleka mtu mahakamani.

Hata kama TAKUKURU wakihusika wao huishia kuchunguza uwezekano wa rushwa na kupeleka file kwa DPP.

Mfano ni kesi ya Kangi Lugola iliyoko TAKUKURU haiko mahakama yoyote nadhani ama file halijaenda kwa DPP au liko kwa DPP lakini hajalipeleka mahakamani.

Huu ni mfano mdogo wa jinsi TAKUKURU isivyoweza kubambikizia watu kedi wakajazana mahabusu. Hawana kifungu hicho.

Anayepeleka watu mahakamani ni DPP na siyo Takukuru.

Lakini hata usingeijua sheria hebu jiulize swali dogo kwamba je ni kesi gani au kesi ngapi za TAKUKURU ulishawahi kuzisijia mahakamani, bila kujali ni za kubambika au la.

Mimi sijawahi kusikia hata moja.

Jiulize swali jingine, hizo kesi 147 zilifunguliwa mahakama ipi?

Mimi sijawahi kusikia hata moja labda wewe na kama umedhasikia tujulishe tusiozijua.

Hivyo wengi wakiwemo waandishi wamelivamia hili suala bila kusoma sheria ya PCCB inasemaje.
wewe ni mfanyakazi wa takukuru? unabishana na Rais? unahisi una adabu kweli?
 
Nahisi we mleta mada huelewi kes nyingi Takukuru huwa zinapelekwa mahakamani bila idhini ya Dpp hasa zile za kukamatwa na rushwa,lakini pia kesi zote zinazohusiana na polis huwa zinapelekwa moja kwa moja kwa moja mahakamani bila kupitia kwa Dpp na hizo ndio nyingi hubambikia watu kesi za uongo,kesi zinazoenda kwa dpp ni zile ambazo huwa zinahitaji uchunguzi kwanza

Kama huelewi kwamba magereza yamejaa watu wa kubambikiwa kesi za uongo za uhujum uchum na utakatishaji basi we haupo nchi hii labda,utakuwa unaishi sayari ya mars
 
Umeona nimemtaja rais yeyote katka post yangu. Jadili mambo niliyotaja kama huelewi.

Hizo kesi 147 nitajie ni Jamhuri dhidi ya nani? Umeshindwa kutaja hata moja unaleta porojo na ni dhahiri hulielewi jambo lenyewe.

wewe ni mfanyakazi wa takukuru? unabishana na Rais? unahisi una adabu kweli?
 
Back
Top Bottom