Gabeji
JF-Expert Member
- Sep 10, 2024
- 1,530
- 1,903
Wananchi wa mkoa wa Dar es salama wameandamana mpaka kwenye ofisi zao, wakilalamika juu ya Rushwa, na kuiba kura kwa baadhi ya watinia nia ya uchanguzi wa serikali za mitaa.
Swali je, TAKUKURU hawana meno kwa CCM? Chanzo East Africa Tv.
=======
Wanachama wa chama cha Mapinduzi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam wamendamana wakiwa na mabango katika ofisi za makao makuu ya chama kwa kile wanachodai kuwepo kwa wizi wa kura na rushwa katika uchaguzi wa kura za maoni.
Wanachama hao kutoka Chanika, Buguruni, Tandika, na Ukonga nje ya Ofisi za makao makuu ya chama Mkoa wamesema fujo zimekithiri sana katika uchaguzi kutokana na wagombea ambao muda wao umeshapita na kukosa ushawishi kutaka kurudi kwenye madaraka pamoja pamoja na rushwa iliyokithiri.
“Fujo zimekithiri sana kwa sababu ya wagombea walio tangulia walishakosa sifa za kurudi kwenye madaraka yao ambayo wao wameyang’ang’ania lakini kitu cha pili ni rushwa kwanzia ngazi ya tawi kata mpaka wilaya. Imefika wakati wagombea hawa wamepewa nguvu bila sababu za msingi”
Amesema mwanachama wa CCM Aidha itakumbukwa kwamba fujo hizo katika kura za maoni zimekuwa zikiripotiwa mara kwa mara katika mikoa mbalimbali nchini ikiwepo Mkoani Manyara pamoja na Mkoani Kigoma