TAKUKURU Kilimanjaro chunguzeni tuhuma hizi

TAKUKURU Kilimanjaro chunguzeni tuhuma hizi

waziri2020

Senior Member
Joined
May 31, 2019
Posts
197
Reaction score
468
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwamba aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Siha mkoani Kilimanjaro, Ndaki Muhuli ambaye kwa sasa amehamishiwa wilayani Kakonko alianzisha miradi ya ufyatuaji matofali na uchanaji wa mbao kama miongoni mwa miradi ya halmashauri ya Siha.

Taarifa hizi zinaeleza kwamba Ndaki alianzisha miradi hii ili matofali na mbao zitumike katika ujenzi wa majengo mbalimbali ya shule na zahanati ndani ya halmashauri hiyo huku mashine ya kufyatulia matofali ikinunuliwa kwa gharama za halmashauri ya Siha kupitia makusanyo ya fedha za ndani.

Taarifa zinadai kwamba Ndaki alianzisha miradi husika baada ya baraza la madiwani la halmashauri ya Siha kuvunjwa kupisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Taarifa hizo zinaenda mbali zaidi na kudai kwamba matofali na mbao ziliuzwa kwa watu wa kawaida bila pesa zinazokusanywa kuingia kwenye akaunti ya halmashauri bali akaunti yake binafsi kinyume na sheria,taratibu na kanuni za utumishi wa umma.

Taarifa hizo zinaeleza kwamba pamoja na watu mbalimbali kuomba zabuni ya kutoa bidhaa hizo kwa halmashauri lakini waliwekewa vikwazo na Ndaki kwa sababu zake binafsi Mara kadhaa.

Lakini mpaka sasa kuna taarifa kwamba miti na magogo kwa ajili ya uchanaji wa mbao ambayo alikuwa akiichukua katika shamba la miti la West Kilimanjaro alikuwa akiichukua Bure bila kuilipia kwa kigezo kwamba yeye ndiye mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo jambo ambalo ni kinyume na sheria za utumishi wa umma.

Lakini jambo la ajabu lililojitokeza hivi karibuni baada ya Ndaki kuhamishwa aliondoka na mbao nyingi alizozipakia kwenye malori mbalimbali ya kampuni ya Dangote ambayo yalikuwa yameleta saruji wilayani Siha haijajulikana alikuwa akizipeleka wapi mbao hizo.

Ieleweke ya kwamba sisi kama wadau wa maendeleo wilayani Siha hatupingi mtu yoyote kuanzisha miradi kama njia ya kujitafutia riziki lakini tunachopinga ni kwanza kuwanyima watu mbalimbali walioomba zabuni ya kusambaza bidhaa kama matofali na mbao,pili ni kutumia fedha za halmashauri kununua machine ya kufyatulia matofali na tatu ni yeye kama mkurugenzi kutumia cheo chake kuanzisha miradi husika na kisha kuiuzia halmashauri anayoingoza hapa kuna mgongano wa kimaslahi (conflict of interest).

Sisi kama wadau wa maendeleo wilayani Siha tunaomba Taasisi ya kuchunguza na kupambana na rushwa (Takukuru) mkoani Kilimanjaro mchunguze tuhuma hizi kama zina ukweli ama la kwa kuwa tangu taarifa hizi zimekuwa zikileta ukakasi ndani ya wilaya yetu na hakuna ufafanuzi wowote kutoka mamlaka husika na Ndaki mwenyewe.

Mungu ibariki Siha,Mungu ibariki Tanzania.

Kazi iendeleeeee.

Mwisho.
IMG_20210829_225842_110.JPG
 
Wazabuni wengi wapigaji wakiwahusisha watu wa manunuzi kwa vigezo vya kanuni na taratibu
 
Back
Top Bottom