GE2025 TAKUKURU Kilimanjaro: Tunafanyia kazi malalamiko 11 ya rushwa dhidi ya watia nia Ubunge CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kilimanjaro, imeeleza kuwa imepokea malalamiko 11 yanayohusu vitendo vya rushwa vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya watiania wa ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani humo.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne Julai 15, 2025 na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kilimanjaro, Musa Chaulo wakati akizungumza na watia nia wa ubunge kupitia CCM kutoka Jimbo la Vunjo na Moshi Vijijini kwenye kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chama hicho.

Chaulo amesema, malalamiko hayo yameanza kufanyiwa kazi, huku baadhi ya watuhumiwa tayari wakiwa wamehojiwa ili kufahamu undani na ukweli wa tuhuma zinazowakabili.

"Tumepokea malalamiko 11 katika ofisi yetu ya Takukuru, yanayohusiana na vitendo vya rushwa kwa baadhi ya watiania ya ubunge ndani ya CCM, tunaendelea kuyafanyia kazi na kuyachakata ili tuone ukweli wa malalamiko hayo," amesema Chaulo.

Ameongeza kuwa; “Tumeanza kuyachakata malalamiko hayo ili kubaini ukweli. Kipindi hiki cha uchaguzi malalamiko mengine ni ya watu kutengenezeana tuhuma ambazo sizo sahihi, lakini tupo makini katika kuhakikisha kila tuhuma tunayoipata tunaifanyia kazi kwa undani zaidi ili tuweze kupata uthibitisho kabla ya kufika kwenye hatua nyingine."

Amesema, Chama Cha Mapinduzi kimeweka taratibu za maadili, lakini wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakikiuka utaratibu huo kutokana na masilahi yao binafsi jambo ambalo haliwezi kufumbiwa macho au kuvumiliwa na Takukuru.

Amesema kiongozi anayeingia madarakani kwa rushwa hataweza kuwasaidia wananchi wake na kudai kuwa wapo baadhi ya viongozi waliokuwa madarakani ambao baada ya kupata nafasi hizo walipotea moja kwa moja na sasa wamerudi kuomba tena kurejea katika nafasi hizo huku wakitangaza wamekuja na fedha.

"Takukuru haitakubali kuona utaratibu unavunjwa. Yeyote atakayebainika kuhusika na vitendo vya rushwa tutamchukulia hatua na mpaka sasa tunao baadhi ya watiania ambao tunaendelea kukamilisha uchunguzi ili tuweze kuwachukulia hatua, tunajua vipo vikao vinafanyika usiku wa saa nane sio kwamba hatujui, tunajua na tunafuatilia. Lakini, niwaombe mtupe ushirikiano ili kudhibiti vitendo hivi," amesema Chaulo.

Amesema baada ya kukamilisha uchunguzi wao, wapo baadhi ya watiania watafikishwa mahakamani na kwenye ngazi ya chama ili kueleza wazi walivyofanya na kuvunja kanuni za chama kabla ya uteuzi kufanyika ili wasiteuliwe na chama kugombea nafasi hizo.

Aidha, Chaulo amesema Takukuru imepanga kukutana na watiania wote wa ubunge katika mkoa huo pamoja na wanaowania nafasi za udiwani ili kuwaelimisha kuhusu madhara ya rushwa na kuwapa onyo dhidi ya kujihusisha na vitendo vinavyokiuka maadili ya uchaguzi.

Baadhi ya watia nia ya ubunge CCM Jimbo la Vunjo na Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro, wakiwa kwenye kikao na Takukuru.

“Rushwa ni adui wa haki na maendeleo. Tumeamua kuwakumbusha wajibu wao kabla ya kuanza kwa kampeni na mchakato mzima wa uchaguzi ili kila mmoja awe na ufahamu wa kile anachopaswa kufanya,” amesisitiza.

Akizungumzia tuhuma hizo, Wilhard Kitaly ambaye ni mtiania Moshi Vijijini, amesema ni vyema wale wanaohusika na vitendo vya rushwa wakatajwa na kuwekwa wazi ili kuwa fundisho kwa wengine.

"Elimu hii ni nzuri tunashukuru sana, lakini umesema wapo watu wameshafikishwa kwenu wakituhumiwa kujihusiaha na vitendo vya rushwa, tunaomba watu hawa watajwe. Lakini, pia elimu hii iwafikie pia wajumbe ili kila mmoja atambue ni kosa kupokea au kutoa rushwa," amesema.

Naye Joseph Mlay mtiania Vunjo ameshauri baada ya CCM kurudisha majina matatu ya watiania watakaogombea katika kura za maoni, taasisi hiyo ikutane nao ili kudhibiti vitendo vya rushwa kuelekea mchakato wa kura za maoni.

Kwa mujibu wa Takukuru, hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya kuhakikisha uchaguzi mkuu ujao unafanyika kwa uwazi, haki na kuzingatia misingi ya maadili ya uongozi.

Katika kikao hicho Takukuru ilitarajia kukutana na watiania 44 wa majimbo ya Moshi Mjini, Moshi Vijijini na Vunjo, lakini waliohudhuria ni watiania 13 kutoka majimbo ya Moshi Vijijini na Vunjo.

Chanzo: Mwananchi
 
IBRA na rushwa,akikosekana nitajua Hatumdai MAMA
 
Na yule anaeingia madarakani kwa hira? mnamfanyanje mfano kiongozi wenu mkuu, kwa mfano swali hilo msije watuma wasiojulikana.
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kilimanjaro imeanza kuchukua hatua dhidi ya baadhi ya watia nia wa nafasi za ubunge na udiwani wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Kilimanjaro, Musa Chaulo, amesema hadi sasa ofisi yake imepokea malalamiko 11 ambayo tayari yameanza kufanyiwa kazi, huku baadhi ya watia nia wakishahojiwa kutokana na tuhuma zinazowakabili.

"Tumepokea malalamiko kadhaa mpaka sasa na tayari tumefanyia kazi malalamiko 11 ili kufahamu ukweli ndani yake, na wapo watia nia ambao tumeshawahoji ambao wanaolalamikiwa kutengenezeana tuhuma ambazo siyo sahihi na majina yao tutayafikisha ndani ya chama chao", amesema Chaulo.
Chaulo alizungumza hayo mara baada ya kuhitimisha semina maalum ya kujengea uelewa watia nia wa ubunge kutoka majimbo ya Moshi Mjini, Vunjo na Moshi Vijijini kuhusu athari za rushwa kisiasa.

Amesema TAKUKURU pia itaendesha mafunzo kama hayo kwa watia nia wa nafasi za udiwani ili kuzuia vitendo vya rushwa vinavyoweza kuathiri mchakato wa uchaguzi.

Katika semina hiyo, baadhi ya washiriki walitaka uwazi zaidi kutoka kwa TAKUKURU. Mtia nia wa ubunge Jimbo la Moshi, Wakili Willehard Kitali, aliitaka taasisi hiyo kuwaweka wazi wanaobainika na tuhuma hizo ili kutoa fundisho kwa wengine.

"Tunataka kusikia ni akina nani wanaojihusisha vitendo vya rushwa sababu mmekuwa mkieleza kuwabaini wala rushwa na wapokeaji ila hatusikii majina yao yakiwekwa wazi", alisema Kitali.

Kwa upande wake, Joseph Mlay, mtia nia kutoka Jimbo la Vunjo, ameshauri kuwa baada ya uteuzi wa majina matatu ya wagombea ndani ya CCM, TAKUKURU ikutane nao mapema ili kudhibiti mazingira ya rushwa kabla ya kura za maoni

503541885_18111043639513179_8812074189668881198_n.jpg
519620223_18111043657513179_846777371486793992_n.jpg

Chanzo Jambo TV
 
Back
Top Bottom