TAKUKURU kuweni wazalendo, chunguzeni zawadi walizopewa viongozi na watumishi waliokwenda Dubai.

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2020
Posts
4,437
Reaction score
13,836
Moja ya mbinu ambazo hutumika na 'wawekezaji' wenye nia ovu ni kuandaa safari za nje ya nchi za 'kuwaelimisha' wafanya maamuzi wa nchi husika.

Safari hizi huambatana na ukarimu wa hali ya juu kwenye mahoteli ya kisasa na utalii wa maeneo mbalimbali ya kuvutia kwenye hizo nchi.

Pamoja na hayo, viongozi hupewa 'zawadi' binafsi za aina mbalimbali kama vile fedha, kompyuta mpakato, simu na kadhalika.

Sasa basi, kwa mujibu wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma kifungu cha 12 kifungu kidogo cha 2 (a & b), kiongozi yeyote apokeapo zawadi yenye thamani inayozidi kiasi cha shilingi laki mbili anawajibika kufanya yafuatayo:
a) kuweka wazi kwa mamlaka husika kuwa alipokea hiyo zawadi
b) kuiwasilisha hiyo zawadi kwa 'acounting officer' anayehusika na ofisi yake ambaye ndiye ataamua matumizi ya zawadi hiyo.

Viongozi wote nchini ikiwa na pamoja na wabunge, mawaziri, wakuu wa taasisi n.k wanakula kiapo cha maadili kwa viongozi wa umma ambacho msingi wake ni sheria hiyo.

Kwa upande wa watumishi wa umma, wao hupaswa kuandikisha na kukabidhi zawadi inayozidi thamani ya shilingi elfu hamsini. Na wao pia hula kiapo cha maadili kwa watumishi wa umma.

Sheria hizi zilitungwa mahususi kwakua serikali inatambua mbinu mbalimbali zinazotumiwa na wafanyabishara katika kuwahadaa viongozi wa nchi, hii imewekwa ili kuepusha kiongozi kushawishiwa kufanya maamuzi baada ya kupewa rushwa iliyovikwa koti la 'zawadi'.

PCCB wachunguzeni haraka delegation yote iliyokwenda na mama Dubai ikiwa ni pamoja na wabunge, kama walipokea 'zawadi' na kama walizikabidhi hizo zawadi kwa mamlaka husika.

Hizi ni nyakati za giza kwa taifa, kila mmoja anapaswa kuwa mzalendo bila kuyumba.
 
Moja ya mbinu ambazo hutumika na 'wawekezaji' wenye nia ovu ni kuandaa safari za nje ya nchi za 'kuwaelimisha' wafanya maamuzi wa nchi husika.

Safari hizi huambatana na ukarimu wa hali ya juu kwenye mahoteli ya kisasa na utalii wa maeneo mbalimbali ya kuvutia kwenye hizo nchi.

Pamoja na hayo, viongozi hupewa 'zawadi' binafsi za aina mbalimbali kama vile fedha, kompyuta mpakato, simu na kadhalika.

Sasa basi, kwa mujibu wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma kifungu cha 12 kifungu kidogo cha 2 (a & b), kiongozi yeyote apokeapo zawadi yenye thamani inayozidi kiasi cha shilingi laki mbili anawajibika kufanya yafuatayo:
a) kuweka wazi kwa mamlaka husika kuwa alipokea hiyo zawadi
b) kuiwasilisha hiyo zawadi kwa 'acounting officer' anayehusika na ofisi yake ambaye ndiye ataamua matumizi ya zawadi hiyo.

Viongozi wote nchini ikiwa na pamoja na wabunge, mawaziri, wakuu wa taasisi n.k wanakula viapo vya kuitii sheria hii.

Kwa upande wa watumishi wa umma, wao hupaswa kuandikisha na kukabidhi zawadi inayozidi thamani ya shilingi elfu hamsini.

Sheria hizi zilitungwa mahususi kwakua serikali inatambua mbinu mbalimbali zinazotumiwa na wafanyabishara katika kuwahadaa viongozi wa nchi, hii imewekwa ili kuepusha kiongozi kushawishiwa kufanya maamuzi baada ya kupewa rushwa iliyovikwa koti la 'zawadi'.

PCCB wachunguzeni haraka delegation yote iliyokwenda na mama Dubai ikiwa ni pamoja na wabunge, kama walipokea 'zawadi' na kama walizikabidhi hizo zawadi kwa mamlaka husika.

Hizi ni nyakati za giza kwa taifa, kila mmoja anapaswa kuwa mzalendo bila kuyumba.
Wamchunguze nani? Top down wote wana mgao
 
Sio pekeyako, wengi tunavyoona jinsi nchi inavyochakazwa inasikitisha na kuhuzunisha sana.
so sad kwa kweli kamanda mwenda zake nae alibaka katiba alituachia ule ugonjwa wa kijani kule bungeni wote ni mkondo mmoja kumpinga mwenyekiti wa chama na raisi sio simple naona tugawane njiti ndo tunapoelekea
 
dp-world-vector-logo-2021 (1).png

Karibuni wageni Karibuni sana.
 
Nakumbuka Hayati Ben Mkapa alipewa Tofari la dhahabu na Barrick Buly.

Je sheria zetu na katiba yetu inasemaje kuhusu zawadi kwa viongozi hebu nijuzeni wadau?
Sheria inamtaja hata rais kuwa anapaswa kuitii hiyo sheria. Lakini wakati huohuo anayo kinga ya kikatiba. Ni vigumu ku enforce hiyo sheria kwake.
 
Back
Top Bottom