Uchaguzi 2020 TAKUKURU Mara: Mjumbe atumbukiza chooni Tsh. 70,000 asikamatwe. Tunawashikilia watano kwa kupokea rushwa kutoka kwa wagombea Viti Maalum

Uchaguzi 2020 TAKUKURU Mara: Mjumbe atumbukiza chooni Tsh. 70,000 asikamatwe. Tunawashikilia watano kwa kupokea rushwa kutoka kwa wagombea Viti Maalum

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Mara inatarajia kuwahoji wagombea ubunge viti Maalum sita mkoa wa Mara ambao wanadaiwa kuwa ni vinara waliohusika kutoa rushwa katika chaguzi za viti maalum mkoani humo.

Mkuu wa Takukuru Mara, Alex Kuhanda amesema kuwa hadi sasa wanawashikilia watu watano ambao walipewa fedha kutoka kwa wagombea wa Ubunge Viti maalum. Lakini pia tumekamata Milioni 3 laki 3 ambazo zilikuwa tayari kupelekwa kwa wajumbe, na Elfu 70 ilituponyoka baada ya mjumbe kuitumbukiza chooni

1595587741482.png
TT​
 
Hawa jamaa kichefuchefu kweli wamemkamata Lusinde na Serukamba Baba yao akawalinda kwa utetezi usiokuwa na miguu wala mikono...waache kuwaonea dagaa.....
 
Hawa Takukuru mbon hawakun'gata wabunge wa upinzani waliponunuliwa? au walikosa makucha ya KUNG'ATIA? Lakini ata hawakufuatilia chochote
Uliwapelekea taarifa za hiyo rushwa wakakataa kuwafuatilia hao watu waliotoa au kuchukua hiyo rushwa au unajaza upupu tu server za jf!

Takukuru hawawezi kuwa kila sehemu kwa wakati mmoja ndio maana mimi na wewe tunahitajika sana kushirikiana na TAKUKURU kwa kutoa taarifa za vitendo au viashiria vya rushwa.

(USIISHIE TU KUULIZA TAKUKURU IMEKUFANYIA NINI BALI PIA JIULIZE WEWE UMEIFANYIA NINI TAKUKURU). TAKUKURU peke yake haiwezi na haitaweza kuzuia na kutokomeza rushwa endapo jamii haitashirikiana na TAKUKURU. IT CAN BE DONE LET US PLAY OUR PART.
 
Hawa Takukuru mbon hawakun'gata wabunge wa upinzani waliponunuliwa? au walikosa makucha ya KUNG'ATIA? Lakini ata hawakufuatilia chochote
Kwa akili yako unaweza kujing'ata kidole chako mwenyewe?
 
CCM ambao hawajatoa rushwa kwenye Kura hizi za maoni sijui hata kama wanafika 10. Membe kupigwa Pini Ni some sort of bribery
 
Hawa Takukuru mbon hawakun'gata wabunge wa upinzani waliponunuliwa? au walikosa makucha ya KUNG'ATIA? Lakini ata hawakufuatilia chochote
Ndiyo sababu kuu ya mimi kuwadharau kupita maelezo.

Wanakuwa kama mbwa koko,hawezi kung'ata mpaka apewe amri na bwana wake.

Kama kweli wanafanya kazi,wasimwangalie mtu usoni,awe ni rais,waziri mkuu ama mtu yeyote wamkamate.

Mnyeti alitoa rushwa wao wanabwabwaja tu wakati ushahidi uko wazi.
 
Uliwapelekea taarifa za hiyo rushwa wakakataa kuwafuatilia hao watu waliotoa au kuchukua hiyo rushwa au unajaza upupu tu server za jf! Takukuru hawawezi kuwa kila sehemu kwa wakati mmoja ndio maana mimi na wewe tunahitajika sana kushirikiana na TAKUKURU kwa kutoa taarifa za vitendo au viashiria vya rushwa. (USIISHIE TU KUULIZA TAKUKURU IMEKUFANYIA NINI BALI PIA JIULIZE WEWE UMEIFANYIA NINI TAKUKURU). TAKUKURU peke yake haiwezi na haitaweza kuzuia na kutokomeza rushwa endapo jamii haitashirikiana na TAKUKURU. IT CAN BE DONE LET US PLAY OUR PART.
Ushahidi wa Nasari haikuwahi kuusikia au kuuona?
 
Chunguzeni pia uchaguzi uliofanyia Jimbo la Rorya hasa mgombea aliyeshika namba 2 kwenye kura za maoni. Rushwa imekuwa tatizo sana katika nchi yetu.
 
Back
Top Bottom