Uchaguzi 2020 TAKUKURU Mara: Mjumbe atumbukiza chooni Tsh. 70,000 asikamatwe. Tunawashikilia watano kwa kupokea rushwa kutoka kwa wagombea Viti Maalum

Ogopa mtu anayetumia pesa ili apate madaraka
Pesa yake atairudisha tu

Ova
 
Hawa Takukuru mbon hawakun'gata wabunge wa upinzani waliponunuliwa? au walikosa makucha ya KUNG'ATIA? Lakini ata hawakufuatilia chochote
Maagizo makali toka juu yalikuwa hayajawafikia hata hivyo yanayotokea sasa ni tip of the Iceberg kwa sababu rushwa kwenye uchaguzi CCM ni tabia ndo maana hakuna anayezhitakiwa na Mahakama ya mafisadi yalifungwa kabla ya kuanza. Kwenye miradi ya ujenzi ndo rushwa tupu kupata tendà, kutokamilisha kwa wakati na na kujenga chini ya kiwango ndo maana miradi mingi ya ujenzi na ya maji mwaka Jana Mwenge na mawaziri kadhaa safarini Mikoani walikataa kufungua. Rushwa ndo inabadili damu kuwa kijani!
 
Uliwapelekea taarifa za hiyo rushwa wakakataa kuwafuatilia hao watu waliotoa au kuchukua hiyo rushwa au unajaza upupu tu server za jf! Takukuru hawawezi kuwa kila sehemu kwa wakati mmoja ndio maana mimi na wewe tunahitajika sana kushirikiana na TAKUKURU kwa kutoa taarifa za vitendo au viashiria vya rushwa. (USIISHIE TU KUULIZA TAKUKURU IMEKUFANYIA NINI BALI PIA JIULIZE WEWE UMEIFANYIA NINI TAKUKURU). TAKUKURU peke yake haiwezi na haitaweza kuzuia na kutokomeza rushwa endapo jamii haitashirikiana na TAKUKURU. IT CAN BE DONE LET US PLAY OUR PART.
Nasari alipeleka ushaidi matokeo yake Mnyeti akapandishwa cheo.
 
Choo gan hicho tukazisake? Tupeni location
 
Kwa akili yako unaweza kujing'ata kidole chako mwenyewe?
Hahahaha! Ukifatilia jinsi alivyokuwa anapita bila kupingwa kuanzia jimboni kwake, ndo utajua kwa nini uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana umevurugwa kiasi hicho.
 
Uliwapelekea taarifa za hiyo rushwa wakakataa kuwafuatilia hao watu waliotoa au kuchukua hiyo rushwa au unajaza upupu tu server za jf! Takukuru hawawezi kuwa kila sehemu kwa wakati mmoja ndio maana mimi na wewe tunahitajika sana kushirikiana na TAKUKURU kwa kutoa taarifa za vitendo au viashiria vya rushwa. (USIISHIE TU KUULIZA TAKUKURU IMEKUFANYIA NINI BALI PIA JIULIZE WEWE UMEIFANYIA NINI TAKUKURU). TAKUKURU peke yake haiwezi na haitaweza kuzuia na kutokomeza rushwa endapo jamii haitashirikiana na TAKUKURU. IT CAN BE DONE LET US PLAY OUR PART.
Pumbavu!
 
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Mara inatarajia kuwahoji wagombea ubunge viti Maalum sita mkoa wa Mara ambao wanadaiwa kuwa ni vinara waliohusika kutoa rushwa katika chaguzi za viti maalum mkoani humo.

Mkuu wa Takukuru Mara, Alex Kuhanda amesema kuwa hadi sasa wanawashikilia watu watano ambao walipewa fedha kutoka kwa wagombea wa Ubunge Viti maalum. Lakini pia tumekamata Milioni 3 laki 3 ambazo zilikuwa tayari kupelekwa kwa wajumbe, na Elfu 70 ilituponyoka baada ya mjumbe kuitumbukiza chooni

Wafikishwe mahakamani,acheni longolongo
 
Hawa Takukuru mbon hawakun'gata wabunge wa upinzani waliponunuliwa? au walikosa makucha ya KUNG'ATIA? Lakini ata hawakufuatilia chochote
Michezo ya kuigiza tu. Hi Taasisi ingefutwa tu.
 
Mbona huyo bosi wa takukuru kachoka hivyo halafu inaonekana anazimezea mate kweli kweli hizo noti
 
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Mara inatarajia kuwahoji wagombea ubunge viti Maalum sita mkoa wa Mara ambao wanadaiwa kuwa ni vinara waliohusika kutoa rushwa katika chaguzi za viti maalum mkoani humo.

Mkuu wa Takukuru Mara, Alex Kuhanda amesema kuwa hadi sasa wanawashikilia watu watano ambao walipewa fedha kutoka kwa wagombea wa Ubunge Viti maalum. Lakini pia tumekamata Milioni 3 laki 3 ambazo zilikuwa tayari kupelekwa kwa wajumbe, na Elfu 70 ilituponyoka baada ya mjumbe kuitumbukiza chooni

Huyu jamaa wa Mara huko vizuri sana.hacheki na nyani.huyu inabidi apate promotion, juzi meko alivyouliza mtu mchapa kazi sijui kwa nini hawakumtaja. Wakapiga kimya
 
Mbona huyo bosi wa takukuru kachoka hivyo halafu inaonekana anazimezea mate kweli kweli hizo noti
Huyo jamaa wiki iliyopita alikamata bil 2 aakazipeleka kwa mkuu wa mkoa.ndio maana anawakamata wanajua ni choka mbaya mwenzao
 
Hawa Takukuru mbon hawakun'gata wabunge wa upinzani waliponunuliwa? au walikosa makucha ya KUNG'ATIA? Lakini ata hawakufuatilia chochote
Gambo katembeza rushwa balaa wako kimya,mwizi hawezi kumkamata mwizi mwenzake ni danganya toto tunachezewa
 
Back
Top Bottom