TAKUKURU mchunguzeni Mkuu wa Wilaya Morogoro, anaitumia ofisi yake vibaya

TAKUKURU mchunguzeni Mkuu wa Wilaya Morogoro, anaitumia ofisi yake vibaya

Kusema, “TAKUKURU mchunguzeni …” ni rai?

Wewe ni mgeni kwenye jukwaa hili kiasi cha kutokujua political vengefulness ya watu waliomo humu?

Mimi sasa hivi nikianzisha campaign dhidi ya Ally Hapi au Dr. Mashinji hapa ndani, kwa kisingizio chochote kile, unadhani sitaungwa mkono na supermajority ya wachangiaji wa uzi wangu?

Mbona kama unahofia sana DC kuchunguzwa? Kwani kama watu wana mashaka nae akichunguzwa si ndio vizuri kuwaondolea hayo mashaka na yeye kubaki msafi on record?

Narudia kwa msisitizo; Takukuru waangalie visingizio nilivyovitaja kisha wachukue hatua za haraka ili kuepusha hasara na upigaji, sababu haya anayotajwa nayo DC sio mepesi kama unavyotaka kuyachukulia mkuu.

Ukiendeleza ubishani usio na tija nitakupuuza.
 
Hakuna cha bure kila siku huwa tunasema humu mpaka tunamnanga Rais kwamba anakopa na kutafuta misaada ajue hakuna cha bure
Sasa nyie mnatala Msando atoe bure ili iweje? Uchumi gani wa kibwege namma hiyo?
Serikali ndo Serikali lakini wananchi wanalipia kupita daraja la Kigamboni, Pantoni za Serikali lakini wananchi wanalipa kuvuka.

Nyie vipi yaani Msando afanye bure baba yenu au nini? Acheni ubwege. Msando ni lawyer hawezi kuwa fala kiasi hicho.

Tuelezane ukweli tu mtu akope 106M akatwe salary kabisa alaf asidai? Mtakiwa mmerogwa nyie.

Alipwe chake kwani machinga siwanafanya biashara wanaingiza hela kwanini yeye ajenge bure?? Uchumi wa kiboya huo haupo duniani hapa
Tatizo sio kulipwa tatizo ni yeye kuutangazia umma kwamba kajitolea. Kama alitaka baadae aje alipwe angefuata taratibu za kiserikali toka mwanzoni. Alichofanya ni kama kutoa tu sadaka. Au alikuwa anatafuta kiki.
 
Huyo msando ni mwizi anashirikiana na mgambo kukamata bajaj zinazopakia maeneo waliyopiga marufuku kusimama na wakikukamata wanapiga faini wanayoitaka wao kati ya 50000 na 30000 na ukizingua wanakuweka polisi na bajaj inaandikwa asitoke kwa amri ya mkuu wa wilaya, kuna jamaa yangu ilimtokea hii akagoma kulipa hadi msando mwenyewe akaenda pale sentro akamuuliza jamaa kwanini hutaki kulipa ni nani anakupa jeuri?
Huyo jamaa yako kauzu 😄😄
 
Mwalimu wa Afrika mashariki mimi huwa namuita masikini na nitaendelea kumuita hivyo! Na hata akijaribu kula hekaluni kwake atashikwa tu afungwe kirahisi kabisa.

Mkuu wa Wilaya mshahara na hayo unayoyaita malupulupu hayatoshi hata kidogo kama una akili za kitajiri
DC analipwa tsh ngapi kwa mwezi?
 
Back
Top Bottom