TAKUKURU mko wapi? Mbunge Musukuma asema wavuvi Kanda ya Ziwa walioombwa rushwa na Luhaga Mpina wako tayari kutoa ushahidi

TAKUKURU mko wapi? Mbunge Musukuma asema wavuvi Kanda ya Ziwa walioombwa rushwa na Luhaga Mpina wako tayari kutoa ushahidi

Mbunge wa Geita Vijijini Mh. Musukuma amehojiwa na chombo cha habari na kueleza kwamba wavuvi wa Ziwa Victoria waliombwa rushwa na Luhaga Mpina, wakati akiwa Waziri wa Uuvuvi, walipomnyima, basi alivunjavunja mitumbwi yao na kuchoma nyavu zao.

Baadhi wanakiri kumpa rushwa Luhaga Mpina ....TAKUKURU, hivi hili halitoshi kumuhoji na kumpeleka Mahakamani ili ikakate kiu ya haki ya wavuvi hawa?

Musukuma mbunge mpumbavu kupitiliza​

Msukuma nae mnafiki mkubwa tu Tena chawa wa kiwango Cha PhD alikuwa wapi siku zote kusema hayo?!!. Nchi hii haiendelei sababu chawa wamezidi.
 
Mpina akiwa Waziri aliwatesa sana watu wa kanda ya Ziwa.

Namkumbuka jamaa wa Mwanza aliyelazimika kuiuza hotel yake aliyoijenga kwa bilioni 6, akaiuza kwa bilioni 3 ili apate hela milioni 300 za kulipa kwa kile kilichotajwa faini ya uhujumu uchumi kwa vile kwenye underground floor ya hotel yake yalipatikana makokoro.

Baada ya kukaa mahabusu kwa zaidi ya mwezi, akaona aheri awape hiyo hela ili awe huru.
Mpina ni muhalifu namba moja nchi hii
 
Luhaga mpina alitakiwa awe jera, ametesa sana watanzania huyu mtu,, we fikiria hadi akaitwa kichaa na mwendazake[emoji16]
 
Ndugu yangu alikamatwa na furu,, nasikia hizi ni tunu ya taifa, mpaka leo haijulikani aliishia wapi
 
Mbunge wa Geita Vijijini Mh. Musukuma amehojiwa na chombo cha habari na kueleza kwamba wavuvi wa Ziwa Victoria waliombwa rushwa na Luhaga Mpina, wakati akiwa Waziri wa Uuvuvi, walipomnyima, basi alivunjavunja mitumbwi yao na kuchoma nyavu zao.

Baadhi wanakiri kumpa rushwa Luhaga Mpina ....TAKUKURU, hivi hili halitoshi kumuhoji na kumpeleka Mahakamani ili ikakate kiu ya haki ya wavuvi hawa?
Kwaaan wao kama ccm kwann wasimfukuze uanachama kama c mwadilifu hadi takukuru
 
Kwani kama kuna rushwa klitembezwa na alilijua hilo alikuwa wapi asiseme mud wote huo? Tena akiwa kama mbunge na alijinyamazie basi naye ni mshiriki ana la kujibu!
Kweli kabisa, na yeye ni mshiriki kwenye rushwa inabidi akajibu ni kwa nini alinyamazia information ya rushwa muda wote huo.
 
Issue hapa siyo Msukuma vs Mpina, bali ni nguvu ya Kipara wa Nishati kujilinda. In short Mpina komaa!. Nawe Msukuma inabidi watu wakutail usikute ulishapigwa mpunga na akina flan ili umtetee Kipara kwakuwa Kipara mwenyewe anawafavor sana hao akina flani. Think outside the box bros and sis
 
Kweli baadhi ya wabunge na wawakilishi wa wananchi ni mambulukenge! Tusameheane tu kweli!
Kwani kama kuna rushwa klitembezwa na alilijua hilo alikuwa wapi asiseme mud wote huo? Tena akiwa kama mbunge na alijinyamazie basi naye ni mshiriki ana la kujibu!
Shoda ni hoja ya ukweli alokuja nayo Mpina? Kwa nini wasishughulikie hoja iliyoko mezani? Kutafuta ukweli kwa manufaa ya waTanzania na sio mtu mmoja!?
Tekelezeni wajibu wenu acheni kutisha watoa hoja!.

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
Hii nchi ya ajabu sana, Mpina ametimiza wajibu wake kama mbunge ameibua hoja yake imekuwa nongwa, kisa amemsema Makamba!! Huyu mbunge Msukuma anavyoropokaga angesikia Mpina amekula rushwa angenyamaza!!
 
Mpina akiwa Waziri aliwatesa sana watu wa kanda ya Ziwa.

Namkumbuka jamaa wa Mwanza aliyelazimika kuiuza hotel yake aliyoijenga kwa bilioni 6, akaiuza kwa bilioni 3 ili apate hela milioni 300 za kulipa kwa kile kilichotajwa faini ya uhujumu uchumi kwa vile kwenye underground floor ya hotel yake yalipatikana makokoro.

Baada ya kukaa mahabusu kwa zaidi ya mwezi, akaona aheri awape hiyo hela ili awe huru.
Sio kweli.... na wewe unatumia ubongo wako kuamini hilo kabisa... uuze hotel kwa 3b kulipa deni la 300m ....hakuna taasisi ya kifedha ambayo ingeshindwa kumpa mtu 300m mwenye Collateral ya 6b... acheni kuwa wajinga wajinga wakati mnaakili timamu.
 
#mpinaAwajibishwe
Naunga mkono Mpina awajibishwe. Na wakimmaliza Mpina, wamfuate Ridhiwani aliyebatilisha hati ya umiliki wa ardhi kumpa GSM ndani ya masaa 24 tangu aapishwe kuwa Naibu Waziri. Hapa napo kuna harufu ya rushwa kali sana!

Naripoti kutoka Rubambangwe karibu na Hifadhi ya Taifa maarufu sana nchini Tanzania ya BURIGI - CHATO!
 
Issue hapa siyo Msukuma vs Mpina, bali ni nguvu ya Kipara wa Nishati kujilinda. In short Mpina komaa!. Nawe Msukuma inabidi watu wakutail usikute ulishapigwa mpunga na akina flan ili umtetee Kipara kwakuwa Kipara mwenyewe anawafavor sana hao akina flani. Think outside the box bros and sis
Issue ni kuwa makundi hasimu ya Msoga na Chato aka Sukuma Gang yanajaribu kupimana nguvu kupitia watu wao. Kundi Msoga ni dhahiri limeshikilia mpini wa panga, na kama figisu wanazijua kweli, hao wengine wapo upande wa makali ya upanga.

Katika vita ukishindwa kupambana na kumthibiti hasimu wako, ni heri ukaungana naye ili mambo yaishe.
 
Mbunge wa Geita Vijijini Mh. Musukuma amehojiwa na chombo cha habari na kueleza kwamba wavuvi wa Ziwa Victoria waliombwa rushwa na Luhaga Mpina, wakati akiwa Waziri wa Uuvuvi, walipomnyima, basi alivunjavunja mitumbwi yao na kuchoma nyavu zao.

Baadhi wanakiri kumpa rushwa Luhaga Mpina TAKUKURU, hivi hili halitoshi kumuhoji na kumpeleka Mahakamani ili ikakate kiu ya haki ya wavuvi hawa?
Huyu ni mlamba Asali hana Jipya!
 
Msukuma alikuwa wapi? Ushujaa wa kijinga, unamlinda mtu, ukikosana nae uanze kusema madhaifu yake. Mie nashauri wa kwanza kuhojiwa na takukuru ni Dr Msukuma kwa kukalia taarifa, alikalia taarifa kwa maslahi ya nani. Ukimchunguza Msukuma anamambo ya kijinga, ilitokea kwa Lowassa, mtu amekuamini baadae kama jasusi unapeleka habari nje kwa kujipendekeza, ni ujinga!
 
Sio uongo aliosema msukuma hata huku kashagulu Kata ya kalya wilaya uvinza mkoa kigoma ziwa Tanganyika tuliombwa rushwa tuliokataa nyavu zilichomwa na kuchukua mashine zetu hadi lleo tunaamniwa tukazikomboe licha yakuwa na leseni na uvuvi halali tunamuomba mama aturudishie hakizetu mpina achunguzwe uonezi ulitumika iundwe tume
Ulikuwa wapi, Msukuma na jiwe walikuwa karibu kwa nini akumripoti hatua ichukuliwe, mbona aliweza kumripoti mkurugenzi wa kahama, huyu alishindwa nini? Unafiki.
 
Back
Top Bottom