DOKEZO TAKUKURU na Usalama wa Taifa, fuatilieni haya; nchi inahujumiwa. Kuna rushwa, urasimu na ufisadi mkubwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwa hali hii ambayo nchi inapitia, uongozi mbovu, rushwa, ubinafsi, ufisadi, nepotism na vetting mbovu, uonevu nk tatizo ni TISS.
Nimekusoma hadi mwisho bila kupumua! Ahsante sana, mkuu 'TrueVoter'.

Mara nyingi tumekuwa tukipotoshwa sana juu ya taasisi hii ya TSS, ni kama kila mtu anayo hadithi yake kuihusu tofauti na wengine.
Leo, kwa mara ya kwanza kabisa umeleta taarifa iliyo tofauti na yenye maana zaidi.

Sijawahi kukusoma humu JF, nashukuru leo nimepata fursa ya kujifunza jambo jipya toka kwako.

Hii ndiyo faida ya kuwa na JF, kila mara kuna jambo jipya la kujifunza.
 
Soma tena kwa utulivu utaelewa ninachokisogeza mbele ya meza ya mfalme..
Siyo rahisi kuielewa jinsi ulivyoiweka.
Nami nilimezea tu nilipokusoma na kuanza kushangaa leo imekuwaje?
 
Na sasa nasikia humo maofisini watu hawakai ni uzembe uzembe na rushwa , hakuna usimamizi
 
Ni kweli

Mabasi sasa hivi yanatoza nauli zilezile kwa wote wanaoshuka njiani na wanao kwenda linakoishia basi, kwa mfano, mtu anaanzia safari Dar kwenda Singida, akipanda bus la Shinyanga atatozwa nauli ya Shinyanga badala ya Singida,

Ukipanda Shabiby Dodoma kwenda Morogoro unatozwa nauli ya Dar
Ukipanda Abood Morogoro unakwenda Chalinze unatozwa nauli ya Dar
Ukipanda ABC Mbeya kwenda Morogoro unatozwa nauli ya Dar
Ukipanda bus la kutoka Mwanza kwenda Dodoma kama unashuka Singida utatozwa nauli za Dodoma
 
Msimlishe rais wetu maneno, kuhusu kamba haina uhusiano na rushwa
 
Wa juu asipokuwa na sauti wa chini wataishia kulogana tu. Kikubwa ufahamu tu kwa sasa nchi ipo kwenye autopilot..tuendelee kupigia kelele sakata la bandari labda Mungu atasikia pambio zetu.
 
Ni mwaka wa 5 tangu nijiandikishe NIDA. Bado Sijapata Kitambulisho.
Nilidhani ni mimi peke yangu, kumbe wapo wengi!

Something will have to give, it cannot continue this way for ever.
 
KWA NINI UNAANDIKA UONGO, MAJUZI NIMEKWENDA OFISI ZA NIDA UKONGA, WAMEFANYIA PROCESS ZOTE FREE TENA KWA HARAKA WAMENIPA WIKI MBILI NIKACHUKUWE NAMBA, KWANZA ID ITAFUATA.

ACHENI UONGO NA UPOTOSHAJI.
Kwa hiyo hata huku majirani zangu mtaani wanachokisema kuhusu urasimu wa NIDA ni uongo?

Kuwa mzalendo usifiche uovu
 
KUna ule Mradi wa SGR unaoendelea kule Mwanza ambapo Mkandarasi Mchina anachakachua viwango vya ubora vya nguzo kwenye madaraja ya reli.

Usalama wa Taifa wwmejaa kedekede pale na hakuna linalofanyika
 
KUna ule Mradi wa SGR unaoendelea kule Mwanza ambapo Mkandarasi Mchina anachakachua viwango vya ubora vya nguzo kwenye madaraja ya reli.

Usalama wa Taifa wwmejaa kedekede pale na hakuna linalofanyika
Usalama wa Taifa wanatafuta vyeo CCM
 
KUna ule Mradi wa SGR unaoendelea kule Mwanza ambapo Mkandarasi Mchina anachakachua viwango vya ubora vya nguzo kwenye madaraja ya reli.

Usalama wa Taifa wwmejaa kedekede pale na hakuna linalofanyika
Wamekuwa wafanyakazi wa mkandarasi😃
 
Nimeipitia ripoti Yako ni kweli kabisa,mfano juzi niliamua kukata tiketi online bus Shabiby lakini nikaiona ipo ya saa saba na saa nane mchana semi luxury Kwa tsh 25000/= bus za asubuhi hawakuziweka.Ila nikaenda stand Mbezi Kwa Magufuli nikazikuta Shabiby nyingi hazijajaa na ticket bei ni tsh 30000/=
Bei juu na Latra haiwajibiki.Kwa ujumla vyombo vya serikali haviwajibiki na Wala hakuna kiongozi anaechukua hatua.
 
Hili la nauli ni uongo wa mchana,mbona ushahidi haipo? Nimesafiri siku za karibuni mbona sijakutana na Hilo? Mbona watu wasilalamike?

Nida huko Kuna shida Toka kitambo sana Hadi Leo haijulikani shida ni ipi maana Kila Bunge Hawa wanasemwa ila hakuna kinachobadilika,labda Bunge litengeneze azimio.

Kuhusu Petrol ni kawaida kukiwa na uhaba lazima wafanyabiashara watumie fursa hiyo kutafuta faida kubwa,japo binafsi Mkoa wangu hiyo shida haipo Mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini mafuta yapo na bei ni Ile Ile sijui Kwa Vijijini.

Kuhusu Mwendokasi Wala hakuna shida uzuri mkataba uko clear ukijenga chini ya kiwango Kuna kipindi Cha Matazamio ikiharibika mkandarasi atarudia Kwa gharama yake.mfano wale waliopita Barabara ya Mpemba -Isongole na Mpanda-Tabora na Sumbawanga -Kasanga mtaona Kuna sections kibao wakandarasi wamefumua na wanarudia.

Bunge litoe azimio kuhusu nida Ili tujue shida Iko wapi
 
Mtag mheshimiwa Rais moja Kwa moja Ili asikie na kusoma mwenyewe, hizi habari za kupelekewa ni za kidwanzi

Yeye mwenyewe alishasema huwa anapita humu
Maeneo machache yakiwa na shida sio lazima Rais Kuna Waziri wa Ujenzi au PM wanaweza shughulikia.

Rais mpaka aje asome ni issue sana
 
KWA NINI UNAANDIKA UONGO, MAJUZI NIMEKWENDA OFISI ZA NIDA UKONGA, WAMEFANYIA PROCESS ZOTE FREE TENA KWA HARAKA WAMENIPA WIKI MBILI NIKACHUKUWE NAMBA, KWANZA ID ITAFUATA.

ACHENI UONGO NA UPOTOSHAJI.
Majinga kama wewe ndio hasara Kwa Taifa,Kwa hiyo Kila mtu ana ID ya NIDA nchii hii?Kila aliyeenda kwenye ofisi zao amepata hicho kitambulisho au namba?
 
Labda hii kampuni Ina mkono wa viongozi wa Serikali, Viongozi wa Mkoa wapige kelele zaidi ,Yale Yale ya Mayanga Construction.

Mbona kampuni zingine zinaogopa sana kurudia kazi?
 
LATRA kuna uozo, ushahidi ninao mwingi tu.

Hongera kwa ushahidi huu.

Pole kwa madhila hayo
 
Labda hii kampuni Ina mkono wa viongozi wa Serikali, Viongozi wa Mkoa wapige kelele zaidi ,Yale Yale ya Mayanga Construction.

Mbona kampuni zingine zinaogopa sana kurudia kazi?
A very serious problem but no one cares
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…