TAKUKURU nawatafuteni katika ' Vijiwe ' vyangu Mbeya Mjini, Kawe na Kigamboni mbona siwaoni Mkiwajibika?

TAKUKURU nawatafuteni katika ' Vijiwe ' vyangu Mbeya Mjini, Kawe na Kigamboni mbona siwaoni Mkiwajibika?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nikiwa kama ' Mzalendo ' wa nchi hii pendwa na tukuka kabisa ya Tanzania nadhani Kisheria nina Wajibu wa Kutoa Mawazo yangu ya Kimtazamo na ikibidi hata Kuwasaidia Wahusika hasa Mamlaka zenye Dhamana ya Haki na Usawa nchini katika Kutekeleza Majukumu yao mema kwa Ustawi wa Amani na Demokrasia ya Tanzania.

Nitashangaa sana kama Mimi Mtu ' Mdogo ' tu GENTAMYCINE nisiye na chochote cha Umuhimu kama waliona wengine niweze Kupata ' Fununu ' za Utoaji Rushwa wa waziwazi unaoratibiwa vyema na ' Umafia / Ungendembwe ' unaofanyika katika Majimbo ya Mbeya Mjini, Kawe na Kigamboni halafu Wahusika ( Mamlaka ) ya Kisheria TAKUKURU Wao wasiwe na ' Fununu ' hizo.

Nawaomba sana TAKUKURU kupitia TCRA ikiwapendezeni hebu fanyeni ' Mshtukizo ' wa Kukamata Simu za ' Watia Nia ' wote wa Ubunge kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi hasa wa ' Majimbo ' yangu haya Tajwa Matatu ya Mbeya Mjini, Kawe na Kigamboni ambayo nimeyachagua kuwa ndiyo ' Majimbo ' nitakayoyakodolea mno Macho kwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu wa 2020.

Mkimaliza Kukamata Simu zao nawaombeni TAKUKURU upesi sana Kamateni na za Wake zao hadi za Madereva wao wa Magari kwani kuna yanayoendelea huko hasa kwa njia za ' Miamala ' ambapo kuna Fedha zinahamishwa ' Kiholela ' kutoka kwa ' Wenye Tamaa ' zao kwenda kwa ' Wajumbe ' ambao kwa sasa ndiyo wamekuwa ' Miungu Watu ' kwa jinsi wanavyonyenyekewa.

Kuna Watu wangu Watatu wapo Mbeya Mjini, Kawe na Kigamboni kuweni makini sana na huo ' Upuuzi ' wenu nisiwasemee kwa Mwenyekiti JPM.
 
mkuu ingependeza uwataje hapa wanaotoa rushwa ili Rais, Bashiru na Polepole wawakabe!

Takukuru wanahongwa, hawawezi kuingilia, yaani ulichofanya ni kesi ya nyani unapeleka kwa tumbili na hakimu ni ngedere!!

kuna stori ilirushwa humu jukwaani JF ya Gambo kuwapa rushwa wajumbe kwa ulinzi wa Takukuru na ofisa huyo wa Takukuru alitajwa!!
 
Naendelea Kusisitiza na Kuonya kuwa kuna Wajumbe Watatu wa CCM Mbeya Mjini, Kawe na Kigamboni mmeshaweka ' Mifukoni ' kuweni Makini!!!
 
Siasa itaendelea kuwa mchezo mchafu tu hadi pale kitakapobuniwa kitu kingine mbadala wa siasa.

Mkuu ' Miamala ' inaetembea katika Simu za Wajumbe wa CCM huko Mbeya Mjini, Kawe na Kigamboni na ' Kinachonishangaza ' kama siyo hata tu ' Kunisikitisha ' eti Mimi Mtu wa Kawaida mno ' napenyezewa ' huo ' Upuuzi ' wote halafu Wahusika ( hasa hao TAKUKURU ) hawajui. TAKUKURU wasipolifanyia Kazi haraka hili nililolileta hapa ' sitowaheshimu ' na ' kuwaamini ' tena Maishani. Na CCM Taifa iwe Makini sana na hawa Wahuni.
 
Hapa tayari Takukuru wamekupata ila kushughulikia ni jambo jingine!!ingependeza ungeweka hapa namba za cm za wajumbe TAkukuru wazikopi!
 
Nasubiri Kwanza nione TAKUKURU ' wamekwamia ' wapi ili niombe ruhusa ya ' Roho Mtakatifu ' Kwanza akiniruhusu ' niwaanike ' ili JPM awajue.
unawaanika muda upi mkuu wakati ndio huu mchakato wa kuhoji watia nia unaendelea?
Takukuru bosi wao tu ndio wa kumuamini wa chini yake wote wanapiga rushwa kama kawa!
 
Hapa tayari Takukuru wamekupata ila kushughulikia ni jambo jingine!!

Na uone kuwa hao Wajumbe Watatu ambao nimeambiwa wana ' Ushawishi ' mkubwa na ndiyo Wanatumika katika ' Kuzurula ' kwa Wajumbe wengine Usiku na Mchana katika hayo Majimbo Tajwa Matatu ya Mbeya Mjini, Kawe na Kigamboni na ' Kuwahonga ' Pesa walivyo ' Mapopoma / Wapumbavu ' wanasema kuwa bora lawama kuliko fedheha wasipokitumia Kipindi hiki ' Kujineemesha ' basi watakuwa ' Masikini ' hadi Kiama.
 
unawaanika muda upi mkuu wakati ndio huu mchakato wa kuhoji watia nia unaendelea?
Takukuru bosi wao tu ndio wa kumuamini wa chini yake wote wanapiga rushwa kama kawa!

Kwa Kuanzia tu ninawaomba TAKUKURU wakakite Kambi yao sasa hivi Kawe nyuma ya Jengo la CCM kuna Baa iitwayo Open Air kuna yanayojiri.
 
Siasa itaendelea kuwa mchezo mchafu tu hadi pale kitakapobuniwa kitu kingine mbadala wa siasa.
Kuna wakati wabunge wa chama tawala walihongwa na viongozi wao akiwemo Katibu mkuu wa chama chao aliyestaafu,pamoja na msimamizi mkuu wa shuguli za serikali bungeni ili wapitishe mswaada wa kandamizi wa serikali. On top of that,Mnyeti aliwahonga pesa madiwani wa chadema Arumeru ili kuunga juhudi, alitoa wapi hiyo pesa au ulikuwa mshahara wake?
 
Gentamycine umegeuka strong medicine?
Pammoja na hilo umpeep Bashiru na Polepole wanaweza wakawashukia kama paratroopers.
Nimemsikia Polepole akidai kuwa atawafanyia upembuzi yakinifu watia nia wote.
 
Mkuu ' Miamala ' inaetembea katika Simu za Wajumbe wa CCM huko Mbeya Mjini, Kawe na Kigamboni na ' Kinachonishangaza ' kama siyo hata tu ' Kunisikitisha ' eti Mimi Mtu wa Kawaida mno ' napenyezewa ' huo ' Upuuzi ' wote halafu Wahusika ( hasa hao TAKUKURU ) hawajui. TAKUKURU wasipolifanyia Kazi haraka hili nililolileta hapa ' sitowaheshimu ' na ' kuwaamini ' tena Maishani. Na CCM Taifa iwe Makini sana na hawa Wahuni.
Bro acha tu watu wahongwe kwa kuwa hata wakipita kihalali bado hawawatumikii wananchi na badala yake wanajitumikia wenyewe...hii ya uchaguzi nionavyo isiitwe rushwa bali iitwe prepaid kwa wapiga kura kama malipo ya awali.
 
Gentamycine umegeuka strong medicine?
Pammoja na hilo umpeep Bashiru na Polepole wanaweza wakawashukia kama paratroopers.
Nimemsikia Polepole akidai kuwa atawafanyia upembuzi yakinifu watia nia wote.

Na labda niwaombe tu hawa ' Waandamizi ' akina Bashiru na Polepole kuwa ' wakodolee ' Mbeya Mjini, Kawe na Kigamboni kuna Madhambi huko.
 
Bro acha tu watu wahongwe kwa kuwa hata wakipita kihalali bado hawawatumikii wananchi na badala yake wanajitumikia wenyewe...hii ya uchaguzi nionavyo isiitwe rushwa bali iitwe prepaid kwa wapiga kura kama malipo ya awali.

Wakitakiwa Watu ' Wazalendo ' wa Kweli wa nchi ya Tanzania na hasa wa Kizazi chetu cha Kati na cha Sasa ' Wajitokeze ' nawe ' Utatoka ' Mkuu?
 
Wakitakiwa Watu ' Wazalendo ' wa Kweli wa nchi ya Tanzania na hasa wa Kizazi chetu cha Kati na cha Sasa ' Wajitokeze ' nawe ' Utatoka ' Mkuu?
Uzalendo gani kwa wanasiasa wanaotumia umasikini wa wananchi kufanikisha malengo yao kisiasa? Nafikiri okoa muda na wakati nitajie mbunge wa eneo lako,muda gani aliokaa kwenye nafasi yake na kero azizozitatua kwa jamii kisha utupe sababu kwanini unadhani anafaa tena kuaminiwa na kwanini hafai kupewa nafasi tena...Hii unayoita rushwa hata wakuu wa chama chako wanatoa ila kwa namna ambayo imewekwa wakfu kutoonekana rushwa.
 
Gentamycine umegeuka strong medicine?
Pammoja na hilo umpeep Bashiru na Polepole wanaweza wakawashukia kama paratroopers.
Nimemsikia Polepole akidai kuwa atawafanyia upembuzi yakinifu watia nia wote.
Slow times two na Katibu mkuu ndo wa kuwapa taarifa
 
Slow times two na Katibu mkuu ndo wa kuwapa taarifa

Umeambiwa kuwa na Wao pia siyo JamiiForums Members kama tulivyo Mimi na Wewe? Tena basi Wao ndiyo tunao Kutwa hapa JF kama haujui.
 
Naendelea Kusisitiza na Kuonya kuwa kuna Wajumbe Watatu wa CCM Mbeya Mjini, Kawe na Kigamboni mmeshaweka ' Mifukoni ' kuweni Makini!!!

Mkuu huwa tunasema kila siku kuwa rushwa haijaisha nchi hii, ila kuna Katazo la kutangaza uwepo wa rushwa ili kuhadaa umma kuwa rushwa imeisha. Kichekesho ni pale wale wanaoongoza kwa kumsifu rais kuwa kaidhibiti rushwa, ndio hao sasa hivi wanaoongoza kwa kutoa rushwa! Hiyo maanake ni kuwa huwa wanampaka rais mafuta kwa mgongo wa chupa.

Na kwa taarifa yako takukuru nao ni sehemu ya kuendeleza rushwa nchi hii. Usitegemee wazuie rushwa. Sana sana umewapa mbinu ya kujipatia rushwa. Watatumia haya maelekezo yako na wataona mtiririko huo wa rushwa, watakachofanya ni kupewa na wao rushwa wakae kimya. Mimi sina utaalamu wowote wa kupambana na rushwa, ila kinachoendelea kwenye chaguzi za ccm ni rushwa isiyohitaji nguvu kubwa kuiona. Hapa Takukuru wapo kutumikia siasa chafu kwa ajili ya kuwakomoa wakoasoji wa watawala.
 
Back
Top Bottom