Nikiwa kama ' Mzalendo ' wa nchi hii pendwa na tukuka kabisa ya Tanzania nadhani Kisheria nina Wajibu wa Kutoa Mawazo yangu ya Kimtazamo na ikibidi hata Kuwasaidia Wahusika hasa Mamlaka zenye Dhamana ya Haki na Usawa nchini katika Kutekeleza Majukumu yao mema kwa Ustawi wa Amani na Demokrasia ya Tanzania.
Nitashangaa sana kama Mimi Mtu ' Mdogo ' tu GENTAMYCINE nisiye na chochote cha Umuhimu kama waliona wengine niweze Kupata ' Fununu ' za Utoaji Rushwa wa waziwazi unaoratibiwa vyema na ' Umafia / Ungendembwe ' unaofanyika katika Majimbo ya Mbeya Mjini, Kawe na Kigamboni halafu Wahusika ( Mamlaka ) ya Kisheria TAKUKURU Wao wasiwe na ' Fununu ' hizo.
Nawaomba sana TAKUKURU kupitia TCRA ikiwapendezeni hebu fanyeni ' Mshtukizo ' wa Kukamata Simu za ' Watia Nia ' wote wa Ubunge kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi hasa wa ' Majimbo ' yangu haya Tajwa Matatu ya Mbeya Mjini, Kawe na Kigamboni ambayo nimeyachagua kuwa ndiyo ' Majimbo ' nitakayoyakodolea mno Macho kwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu wa 2020.
Mkimaliza Kukamata Simu zao nawaombeni TAKUKURU upesi sana Kamateni na za Wake zao hadi za Madereva wao wa Magari kwani kuna yanayoendelea huko hasa kwa njia za ' Miamala ' ambapo kuna Fedha zinahamishwa ' Kiholela ' kutoka kwa ' Wenye Tamaa ' zao kwenda kwa ' Wajumbe ' ambao kwa sasa ndiyo wamekuwa ' Miungu Watu ' kwa jinsi wanavyonyenyekewa.
Kuna Watu wangu Watatu wapo Mbeya Mjini, Kawe na Kigamboni kuweni makini sana na huo ' Upuuzi ' wenu nisiwasemee kwa Mwenyekiti JPM.